Rais Magufuli atakubali kuachia ngazi muda wake madarakani ukiisha?

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
32,924
2,000
Nasema haya kwa hasira kali sana juu ya unafiki na ujinga unapendelea nchi hii.

Nasema haya huku nchi ikiwa na mihimili miwili tu ya serikali&bunge na mahakama

Nasema haya huku kukiwa na kundi kubwa linaloendeshwa na mihemko na lisilo na mda wa kutafakari kwa kina,kundi CCM

Nasema haya huku kukiwa na kundi kubwa linaloamini kuwa Magufuli yupo juu ya katiba na lolote analosema ni sawa,hata kama wao hawalikubali.

Nasema haya huku watanzania wengi wakiwa wanaamini anachokifanya Magufuli sio wajibu wake bali ni hiyari au hisani

Nasema haya nchi ikiwa imebakiwa na watu jasiri mfano wa Tundu Lissu, wawili au watatu

Nasema haya huku viongozi watangulizi wakiwa ni watuhumiwa wakubwa wa ufisadi.

Nasema haya baada ya kumsikia rais mstaafu mwenyewe kuheshimiwa sana Ali Hasan Mwinyi akipendekeza Rais Magufuli aongezewe mda ikibidi atawale milele

Ni dhahiri sasa Magufuli atatumia ujinga wetu kujiongezea mda na wala hatahitaji nguvu kubwa,ni hizi hizi kiki za makinikia na Escrow zimeshafanikisha hilo. Kura itapigwa na Magufuli atajiongezea mda kwa mujibu wa katiba

Hongera Magufuli
 
Chiwa

JF-Expert Member
Apr 17, 2008
2,904
2,000
tehe..teh... hivi mlielewa vizuri alivyokuwa anawakimbiza mchaka mchaka? hamkuelewa tafsiri yake? alieeleza kabla ya kuchukua fomu atafanyaje? na upole wa kikwete mliuona hauna maana mkamwingilia mpaka maisha yake binafsi yeye akacheka tu na watu wakawa wanasema na kutamani kama wangepata rais dictor na yeye kama rais mpendwa akawasaidia kumpata sasa leo tunalalamika nini?
tukubali tusikubali hata mataifa yaliyoendelea na wanaotuonyesha eti wao wanademokrasia zaidi kuna kipindi kuna watu walikufa na kuteseka kwa maendeleo waliyonayo leo.
sasa we kazi utaki kufanya au unafanya chini ya kiwango unategemea nini?
 
ELX

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
328
500
Mmmmh kwanini ajiongezee? Je, Mzee Mwinyi kalisema toka moyoni au namna ileile ya sasa kila mtu kutaka kucheza mziki na mdundo uliopo. Hakuna anayetaka kupitwa, hats kama ni MTU wa regge maadamu kwa sasa Singeri ndo habari ya mjini, kila mmoja ni msingeri. Mungu atuhurumie tuu, tujitambue
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
39,480
2,000
HUU MZIKI WA HUYU JAMAA JPM NI SHIDA, bado miaka nane ila watu jasho tayari!

Mkuu hatukatai hata akitawala miaka 200 sio shida kwani sio wote tunapenda kuwa marais. Ila tunahoji unafuu ni upi katika maisha yetu mpaka tutake atawale zaidi ya miaka 5 na iwapo atafanikiwa basi atawale 5 mingine ya mwisho? Hayo madini mpaka sasa hatujaona mafanikio zaidi ya kulianzisha. Ilibidi tusubiri tuone matokeo chanya ya maisha yetu hapo ndio tufikirie hilo mnalotaka nyie. Nakupa mfano mdogo tu. Kabla ya yeye kuingia madarakani alikuta sukari ni 1,800-2,000@kg. Akalianzisha kama alivyolianzisha sasa kwenye madini, matokea ya vurugu ile sukari sasa imepanda mpaka 3,000@kg na amekaa kimya!! Sasa kama suala hilo dogo tu liko hapo tukimuongezea miaka zaidi ya 10 si ndio tutanunua sukari 50,000@kg. Ile 50m kila kijiji sasa hivi wala haiongelewi tena.

Ni kipi kimekuwa nafuu ambacho tunaweza kweli kutembea kifua mbele kwamba sasa kweli tunajivunia? Ni kweli kuanza kufuatilia hao mafisadi wa mali zetu ni jambo jema. Je hiyo pekee italeta unafuu kwenye maisha yetu au ni yeye atapata sifa binafsi na kwa sasa anataka sifa hiyo pia chama chake kizipate. Ilibidi tusubiri wangalau akiwa amefikisha miaka 8 madarakani hapo tungeweza kuwa kwenye nafasi ya kutaka aongezewe muda.
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
30,490

yeye kasema atagombea hiyo miaka yenu au nyie ni waathirika wa hofu zenu??
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom