Rais Magufuli atakubali kuachia ngazi muda wake madarakani ukiisha?

ndege wafananao huruka pamoja
tulijua tu toka alipoanza urafiki na PK and Co
JPM-kagame.jpg

Leo sinto ongeza neno, bikozi aiam noti richabo in 7m....
 
Mzee mwinyi hakupaswa kuongea hayo haradhan. Amejidharirisha sana hata kama anampigania mwanae apewe urais znz amebugi.
 
Mkuu watu wengi hatupendi mambo ya CCM ya hovyo hovyo.Mambo kama yaDC wa Ubungo ya kuweka watu lock up bila sababu za msingi hatukubaliani nayo.Badala ya kuweka "lockup" fikra za kijinga yeye anahangaika na watu wanaotoa fikra mbadala.

Lakini hili la Magufuli kuongoza zaidi ya muda wake wa Kawaida ni jambo la mjadala wa kiafya sana.Tujengeni hoja vizuri na kwa ustadi kwa wale tusiokubaliana na hoja hiyo.

Jengeni hoja kuonyesha ni kwa namna gani kujaribu jaribu uongozi kuna tija badala ya kuendelea na mtu ambaye tumemjaribu na kweli "amelipuka" kama tulivyotaka.

Jengeni hoja vizuri kuonyesha ni kwa namna gani muda unaweza kututawala sisi hadi tukimbizane nao na kushindwa kuendelea kumtumia mtu wa kufanya mambo mema kwa sababu tu muda wake umeisha.

Jengeni hoja vizuri ni kwa namna gani ukomo wa uongozi wa uraisi hauwezi kutenguliwa ikiwa tunaye mtu aliyeonyesha uwezo wa kulisaidia Taifa.

Jengeni hoja kwa nini sasa tusiwe na Katiba inayosema kuwa kuanzia sasa kusiwe na ukomo katika Uraisi Bali ukomo utokane na performance ya Raisi husika.Kwamba ukiwa madarakani hata miezi mitano na wananchi tukaona na kujiridhisha kuwa raisi fulani aliyeko kwenye "usukani" wa Lori ameshindwa kumudu majukumu yake basi anakomea hapo hapo Mara moja.

Mkuu kwanza nikupongeze kwa kukubali ombi langu la kurudi kuona mchango wangu. Ni kweli hata mimi sina shida kwa rais mwenye uwezo kuongezewa muda wa kukaa madarakani kwani mimi sihitaji kuwa rais. Je ni kweli kutoka wananchi 45m na wakati atakapomaliza muda wa 5+5 iwapo atafanikiwa, watu huenda tukawa 55m+, hakuna mwingine anayeweza isipokuwa yeye tu!!

Kingine ambacho mimi ninasimamia, hivi je kwa sasa ni wakati muafaka wa kuanza kuzungumzia kumuongezea muda ama ni uchuro tu? Je ni lipi hasa ambalo limeleta unafuu wa dhahiri kwenye maisha ya wananchi kiasi kwamba tuone kwamba anahitaji miaka zaidi? Je amefanikiwa katika kilimo ambacho kinabeba watu wengi? Jibu ni hapana na hata bajeti yake ya kilimo inadhihirisha hilo. Hizi hatua anazochukua leo ni kama zimechelewa japo ni nzuri. Je tuna uhakika wa kupata lolote la maana pindi atakapomalizana na hao anaowachukulia hatua sasa? Wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba tunaongozwa na hisia kiasi kwamba tunaona ndio uhalisia. Kwanini tusitoe muda, wangalau miaka 8 ili tuone ufanisi wake hapo tuone kama kuna haja ya yeye kuongezewa muda?

Wasiwasi wangu viongozi wetu sisi waafrika tunawajua tabia zao na udhaifu wao. Leo hii mgema anaweza kusifiwa kisha tembo akalitia maji. Atatengeneza sheria mapema kwa hizi hisia zetu, kisha mbele ya safari hata tukiona hafai ikawa ngumu kumtoa. Mifano ni mingi ya hiki ninachokisema, wala hatuenda mbali Mugabe hapo, ana zaidi ya miaka 30 madakani, uchumi umeanguka lakini hataki kutoka madarakani kwa gia la uzalendo. Wote tumeona juzi suala ambalo liko ndani ya ilani yake akilikataa tena hadharani na wala chama chake hakijaweza kumzuia, na kibaya mno waziri Mwigulu anakazia taasisi yoyote itakayoonyesha mtazamo tofauti basi ataifuta!!! Tunaweza kufanya ushabiki lakini tusishangae iko siku tukalia kilio cha mbwa mdomo juu.
 
Mkuu hatukatai hata akitawala miaka 200 sio shida kwani sio wote tunapenda kuwa marais. Ila tunahoji unafuu ni upi katika maisha yetu mpaka tutake atawale zaidi ya miaka 5 na iwapo atafanikiwa basi atawale 5 mingine ya mwisho? Hayo madini mpaka sasa hatujaona mafanikio zaidi ya kulianzisha. Ilibidi tusubiri tuone matokeo chanya ya maisha yetu hapo ndio tufikirie hilo mnalotaka nyie. Nakupa mfano mdogo tu. Kabla ya yeye kuingia madarakani alikuta sukari ni 1,800-2,000@kg. Akalianzisha kama alivyolianzisha sasa kwenye madini, matokea ya vurugu ile sukari sasa imepanda mpaka 3,000@kg na amekaa kimya!! Sasa kama suala hilo dogo tu liko hapo tukimuongezea miaka zaidi ya 10 si ndio tutanunua sukari 50,000@kg. Ile 50m kila kijiji sasa hivi wala haiongelewi tena.

Ni kipi kimekuwa nafuu ambacho tunaweza kweli kutembea kifua mbele kwamba sasa kweli tunajivunia? Ni kweli kuanza kufuatilia hao mafisadi wa mali zetu ni jambo jema. Je hiyo pekee italeta unafuu kwenye maisha yetu au ni yeye atapata sifa binafsi na kwa sasa anataka sifa hiyo pia chama chake kizipate. Ilibidi tusubiri wangalau akiwa amefikisha miaka 8 madarakani hapo tungeweza kuwa kwenye nafasi ya kutaka aongezewe muda.

Mkuu nimekuelewa sana.Hoja yako iko vizuri.Hivi ndivyo watu "wanavyokong'okotana" kisomi.Sio kupiga watu kwa magongo na kuwaitia watu polisi wawapige madaruga Bungeni wenye hoja kinzani.

Mkuu kinachoendelea kwa sasa ni proposition tu.Kwamba huyu Magu akiendelea "kulisongesha" namna hii basi ni vizuri muda wake ukimalizika basi ipo haja ya kumuongezea muda.

Mintarafu "nyayo" za aliyofanya mpaka sasa zipo.Nataja chache japo si kwa uzito wake: "Fisi" waliokuwa wanashambulia Uwajibikaji na nidhamu wameondoshwa."Mbweha" waliokuwa wamegeuza nchi kuwa ya kufoji foji na waliotaka kuigeuza nchi iwe ya ili mradi vyeti tu katika utendaji wameshatafunwa.

Suala la Sukari kweli kalisongesha na limefikia hapo uliposema.Kama ulisikiliza mpango wa maendeleo wa miaka 5 ukiwasilishwa Bungeni Dawa yake iko jikoni.Kuna mfuko wa jamii mmoja utajenga kiwanda na nina imani tatizo la waliokuwa wanaagiza sukari na kuificha wakifanya hivyo tena wakati huo watatumia wao na familia zao.Nami nionavyo pamoja na madhara yaliyojitokeza kufuatia mshike mshike ule ulilenga kwanza kutoa funzo dhidi ya ushenzi tuliokuwa tunafanyiwa.Ni afadhali kwamba bei imepanda na sukari ipo na ya viwango kuliko ilivyokuwa hapo awali kwamba tunaipata kwa bei nafuu lakini ikawa ni ya kudhoofisha uhai wetu siku za usoni.Kumbe kilichokuwa kinafanya tuone unafuu wa bei ni rehani ya maisha yetu.

Kwa hiyo hoja ya kuongezewa muda ni proposition tu na inakolezwa na mambo ya "mbolea" yanayotokea.
 
Kauli ya Rais mstaafu Mwinyi imelidhalilisha Taifa na nafsi yake.
Uzee unamsumbua na uwezo wake wa kupima mambo umapungua! Na au anaogopa kufutiwa posho kwa ajili ya loliondo scandle iliyoonyeshewa kidole! Anaipooza kimrindo.
 
Kwa uwingi w wa bunge wa fisiemu wakikubali kunyamaza na kusema fikra sahihi za mwenyekiti zdumu,,,, nakuishia tu kwa, kwa kwa, kwa, kwa,, ,,,,,huo utakua ni ujinga na upumbavu uliokomaaa na kuvuka mipaka
 
Mkuu nimekuelewa sana.Hoja yako iko vizuri.Hivi ndivyo watu "wanavyokong'okotana" kisomi.Sio kupiga watu kwa magongo na kuwaitia watu polisi wawapige madaruga Bungeni wenye hoja kinzani.

Mkuu kinachoendelea kwa sasa ni proposition tu.Kwamba huyu Magu akiendelea "kulisongesha" namna hii basi ni vizuri muda wake ukimalizika basi ipo haja ya kumuongezea muda.

Mintarafu "nyayo" za aliyofanya mpaka sasa zipo.Nataja chache japo si kwa uzito wake: "Fisi" waliokuwa wanashambulia Uwajibikaji na nidhamu wameondoshwa."Mbweha" waliokuwa wamegeuza nchi kuwa ya kufoji foji na waliotaka kuigeuza nchi iwe ya ili mradi vyeti tu katika utendaji wameshatafunwa.

Suala la Sukari kweli kalisongesha na limefikia hapo uliposema.Kama ulisikiliza mpango wa maendeleo wa miaka 5 ukiwasilishwa Bungeni Dawa yake iko jikoni.Kuna mfuko wa jamii mmoja utajenga kiwanda na nina imani tatizo la waliokuwa wanaagiza sukari na kuificha wakifanya hivyo tena wakati huo watatumia wao na familia zao.Nami nionavyo pamoja na madhara yaliyojitokeza kufuatia mshike mshike ule ulilenga kwanza kutoa funzo dhidi ya ushenzi tuliokuwa tunafanyiwa.Ni afadhali kwamba bei imepanda na sukari ipo na ya viwango kuliko ilivyokuwa hapo awali kwamba tunaipata kwa bei nafuu lakini ikawa ni ya kudhoofisha uhai wetu siku za usoni.Kumbe kilichokuwa kinafanya tuone unafuu wa bei ni rehani ya maisha yetu.

Kwa hiyo hoja ya kuongezewa muda ni proposition tu na inakolezwa na mambo ya "mbolea" yanayotokea.

Wewe wangalau umejenga hoja inayoingia akilini na sio hiyo mihemko wala ushabiki. Kwa yote uliyoeleza hapo juu nadhani bado wote tunabaki palepale tutoe muda wa kutosha ndio tufanye hilo linalopigiwa chapuo sasa. Serekali zote zilizopita mbali ya nia yake njema zote zilikuwa na mikakati mizuri ila lengo halikufikiwa, na kibaya zaidi hata lengo likaachwa ukaanza huo uliopelekea akina Seth kupigishwa magoti juzi, na makinikia kutolewa nje kwa mikataba ya ndiooooooooo.
 
Mkuu kwanza nikupongeze kwa kukubali ombi langu la kurudi kuona mchango wangu. Ni kweli hata mimi sina shida kwa rais mwenye uwezo kuongezewa muda wa kukaa madarakani kwani mimi sihitaji kuwa rais. Je ni kweli kutoka wananchi 45m na wakati atakapomaliza muda wa 5+5 iwapo atafanikiwa, watu huenda tukawa 55m+, hakuna mwingine anayeweza isipokuwa yeye tu!!

Kingine ambacho mimi ninasimamia, hivi je kwa sasa ni wakati muafaka wa kuanza kuzungumzia kumuongezea muda ama ni uchuro tu? Je ni lipi hasa ambalo limeleta unafuu wa dhahiri kwenye maisha ya wananchi kiasi kwamba tuone kwamba anahitaji miaka zaidi? Je amefanikiwa katika kilimo ambacho kinabeba watu wengi? Jibu ni hapana na hata bajeti yake ya kilimo inadhihirisha hilo. Hizi hatua anazochukua leo ni kama zimechelewa japo ni nzuri. Je tuna uhakika wa kupata lolote la maana pindi atakapomalizana na hao anaowachukulia hatua sasa? Wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba tunaongozwa na hisia kiasi kwamba tunaona ndio uhalisia. Kwanini tusitoe muda, wangalau miaka 8 ili tuone ufanisi wake hapo tuone kama kuna haja ya yeye kuongezewa muda?

Wasiwasi wangu viongozi wetu sisi waafrika tunawajua tabia zao na udhaifu wao. Leo hii mgema anaweza kusifiwa kisha tembo akalitia maji. Atatengeneza sheria mapema kwa hizi hisia zetu, kisha mbele ya safari hata tukiona hafai ikawa ngumu kumtoa. Mifano ni mingi ya hiki ninachokisema, wala hatuenda mbali Mugabe hapo, ana zaidi ya miaka 30 madakani, uchumi umeanguka lakini hataki kutoka madarakani kwa gia la uzalendo. Wote tumeona juzi suala ambalo liko ndani ya ilani yake akilikataa tena hadharani na wala chama chake hakijaweza kumzuia, na kibaya mno waziri Mwigulu anakazia taasisi yoyote itakayoonyesha mtazamo tofauti basi ataifuta!!! Tunaweza kufanya ushabiki lakini tusishangae iko siku tukalia kilio cha mbwa mdomo juu.

Mkuu sio mambo ya uchuro.Ni matashi mema.Ikiwa hatuwezi kuanza mjadala juu ama anafaa au hafai kuongezewa muda basi hatuna tofauti na mtu anayetembea huku akijitazama miguu take badala ya kuangalia mbele.Mkuu Mimi sijasema Magu hana mapungufu ila wengi mzani wetu unaelemea upande mazuri zaidi kuliko mapungufu.

Kumhukumu mtu kwa tabia za mtu mwingine huko kufanya fallacy.Ikiwa ndivyo kwamba anaweza kugeuka na kuishi sawa na Mgabe kwa nini Malkia Elizabethi hajawa sawa na Mgabe? Au kwa nini Putin hajawa sawa na Mseveni (kwa kadri ya uoni wetu)?

Mapungufu yake tunayoyahofia tuyachukue kama fursa.Tuyachukue kama daraja.Tusiogope kuvuka daraja.Mapungufu yasiwe kituo Bali mkato.Tumwambie waziwazi kuwa sisi watanzania tunaweza kuhitaji kukuongezea muda lakini mkataba wetu na sisi ni kwa mambo ya kuumba upya uhai wetu.
 
Humjuwi vzr mwinyi ni msanii, usishangae kasema ivo kwa kinyume chake
Inawesekana sana, upo sahihi. Au anataka asikie watu watasema nini. Kwangu mimi sijaona lolote la pekee hata kufikia kuongezewa muda.

Ni ujinga wa hali ya juu kukiuka katiba yetu wenyewe kwaajili ya mtu mmoja. Unaposema huyu ni mzuri, una uhakika gani kuwa huko nje hakuna wazuri zaidi? Namkumbuka Mwalimu alivyokemea ujinga wa kusema tumwongezee Rais fulani kwa kuwa ni mzuri. Aliuliza kuwa je matarajio yenu ilikuwa mmpate Rais mbaya? Mbaya anatakiwa atolewe hata kabla ya kumaliza kipindi chake cha miaka 5. Aliye mzuri amalize kipindi chake cha miaka 5. Mzuri sana aongezewe mingine 5, halafu akapumzike ili tumpate mzuri mwingine.

Mwalimu alisema kuwa kama Rais anayependwa sana ni sharti abadilishiwe katiba, kule Marekani Reagan angebadilishiwa katiba lakini hawakufanya hivyo.

Kubadilisha katiba kwaajili ya mtu mmoja ni wendawazimu wa hali ya juu. Tuukatae uwendawazimu huo, tuukatae ujinga wa namna hiyo. Tuheshimu katiba. Katiba haistahili kuchezewa na kubadilishwa mara kwa mara.
 
Mkuu sio mambo ya uchuro.Ni matashi mema.Ikiwa hatuwezi kuanza mjadala juu ama anafaa au hafai kuongezewa muda basi hatuna tofauti na mtu anayetembea huku akijitazama miguu take badala ya kuangalia mbele.Mkuu Mimi sijasema Magu hana mapungufu ila wengi mzani wetu unaelemea upande mazuri zaidi kuliko mapungufu.

Kumhukumu mtu kwa tabia za mtu mwingine huko kufanya fallacy.Ikiwa ndivyo kwamba anaweza kugeuka na kuishi sawa na Mgabe kwa nini Malkia Elizabethi hajawa sawa na Mgabe? Au kwa nini Putin hajawa sawa na Mseveni (kwa kadri ya uoni wetu)?

Mapungufu yake tunayoyahofia tuyachukue kama fursa.Tuyachukue kama daraja.Tusiogope kuvuka daraja.Mapungufu yasiwe kituo Bali mkato.Tumwambie waziwazi kuwa sisi watanzania tunaweza kuhitaji kukuongezea muda lakini mkataba wetu na sisi ni kwa mambo ya kuumba upya uhai wetu.

Mkuu sipingi mtazamo au mitazamo yenu kwani hiyo ndio demokrasia tunayoitaka. Mimi nimesema kwa sasa ni mapema sana kwani we have seen nothing perculiar. Ni vyema tukawa na subira tungoje tuone mabadiliko yenye nafuu na sio dalili za mabadiliko.

Mkuu mm nimemtaja Mugabe na kwa msisitizo nikasema viongozi wetu wa kiafrika. Ww unanitajia mfano wa Malkia Elizabrth na Putin. Kwangu hapa naona ni kama umelazimisha niikubali hoja yako. Huko UK malkia haongozi serekali bali waziri mkuu na kila siku tunaona wanabadilisha. Kwa Putin alichofanya alikaa kwa muda wake, kisha akatoka akawa waziri mkuu, halafu akarudi tena. Hapo alitumia udhaifu wa katiba yao kufanya yake. Hata hivyo yeye sio mfano mzuri wa demokrasia. Halafu hao viongozi wa kizungu uliowataja bado hawaongozi nchi kama hizi zetu ambazo bado wakulima wengi wanalima kwa jembe la mkono na kutegemea mvua. Hujasikia hizo nchi zao zinachangishana kununua madawati. Hao wanashindana kupeleka vyombo kwenye anga za juu. Huko watu hawakimbii na mabox ya kura mzee. Wakati sisi bado tunazuia wanafunzi wajawazito wasipate elimu bali wakashone cherehani na asitokee mtu kuhoji hata kama una wazo tofauti!!

Tuwe wakweli tu, kwetu sisi waafrika kufikiria au kutamani kumuongezea rais muda wa kukaa madarakani ni kujitafutia matatizo. Na uzoefu nao unaonyesha hivyo, wengi wa viongozi wanakaa madarakani muda mrefu huishia kuumiza na hata kuwaua wale wote wenye mitazamo tofauti na wao kwa kuamini wao wako sahihi 100%.
 
Kama atafanya hivyo NAMUONA GADDAFI,NAMUONA MAGUFULI
NAIONA ZIMBABWE, NAIONA TANZANIA.
 
ndege wafananao huruka pamoja
tulijua tu toka alipoanza urafiki na PK and Co
Dah... Rwanda Ina mabadiliko makubwa chini ya PK..... Kama ilivyo kwenye vita yoyote ile... Vita ya Kiuchumi nayo Ina wahanga pia.... Kwa faida ya wengi.... Huo ndiyo ukweli mchungu
 
Mziki wa mhe rais hakuna mpinzani yeyote yule anayeweza kuucheza.
upinzani tukubali tu hadharani kua huyu mhe ametuzidi uzito.

Kwa huu mziki wake akitembea nao mpaka 2020, itakua haina haja ya kuingia gharama za uchaguzi wa rais.
Hata mkapa na kikwete mliyasema haya haya nyie kazi yenu ni kusifu tu hata kama sukari kilo 10000 au umesahau yale maisha bora kila mtanzania?
 
Mziki wa mhe rais hakuna mpinzani yeyote yule anayeweza kuucheza.
upinzani tukubali tu hadharani kua huyu mhe ametuzidi uzito.

Kwa huu mziki wake akitembea nao mpaka 2020, itakua haina haja ya kuingia gharama za uchaguzi wa rais.
Hata mkapa na kikwete mliyasema haya haya nyie kazi yenu ni kusifu tu hata kama sukari kilo 10000
 
Back
Top Bottom