Rais Magufuli atakubali kuachia ngazi muda wake madarakani ukiisha?

Nasema haya kwa hasira kali sana juu ya unafiki na ujinga unapendelea nchi hii.

Nasema haya huku nchi ikiwa na mihimili miwili tu ya serikali&bunge na mahakama

Nasema haya huku kukiwa na kundi kubwa linaloendeshwa na mihemko na lisilo na mda wa kutafakari kwa kina,kundi CCM

Nasema haya huku kukiwa na kundi kubwa linaloamini kuwa Magufuli yupo juu ya katiba na lolote analosema ni sawa,hata kama wao hawalikubali.

Nasema haya huku watanzania wengi wakiwa wanaamini anachokifanya Magufuli sio wajibu wake bali ni hiyari au hisani

Nasema haya nchi ikiwa imebakiwa na watu jasiri mfano wa Tundu Lissu, wawili au watatu

Nasema haya huku viongozi watangulizi wakiwa ni watuhumiwa wakubwa wa ufisadi.

Nasema haya baada ya kumsikia rais mstaafu mwenyewe kuheshimiwa sana Ali Hasan Mwinyi akipendekeza Rais Magufuli aongezewe mda ikibidi atawale milele

Ni dhahiri sasa Magufuli atatumia ujinga wetu kujiongezea mda na wala hatahitaji nguvu kubwa,ni hizi hizi kiki za makinikia na Escrow zimeshafanikisha hilo. Kura itapigwa na Magufuli atajiongezea mda kwa mujibu wa katiba

Hongera Magufuli

Tunasema haya tukiwa na tumejazwa na kuona nuru mbele yetu.Kwa miaka 30 hatukuwa na Kiongozi wa nchi anayetambua wajibu wake sawa sawa.

Tunasema haya ya kumuomba Magufuli afikirie na aone umuhimu wa kuendelea kuisaidia nchi baada ya muda wake kumalizika hadi hapo atakapopatikana kiongozi atakayeweza vaa viatu vya Magufuli.

Tunasema mambo haya hadharani bila kificho kuanzia sasa kuwa sisi wengine ni wapinzani wa mambo ya hovyo ya CCM kwa muda mrefu lakini kwa anayoyafanya Magufuli tuko naye na tutamhitaji tena kwa muda mrefu sana ikiwa atakuwa Nazo nguvu za kiakili na kimwili.

Tunasema mambo haya ya kumuongezea Magufuli muda kwa sababu utendaji kazi wake mzuri hauwezi kuwa out-weighed na Katiba.

Tunasema mambo haya mchana kweupe kwamba Katiba ipo ili itusaidie kupata viongozi wema na wenye kujua na kufahamu shibe zetu.
 
yeye kasema atagombea hiyo miaka yenu au nyie ni waathirika wa hofu zenu??

Yeye hajasema kama atagombea, lakini huoni trend ya watu wanaotaka aongezewe muda? Inapofikia mpaka rais mstaafu anatamka hilo hadharani unategemea nini? Juzi pia tumeona waziri mkuu mstaafu Joseph Warioba akiongoza maandamo, na waandamanaji wale wakataka pia muda wa rais kuongezewa muda.

Pia nashukuru kwamba umeona hoja yangu ya unafuu wa maisha, na kwa ustadi fulani umekwepa hata kuongelea hilo la bei ya sukari. Nilitarajia angekataza hiyo hali ya watu kutaka yeye aongezewe muda ili hao wenye viherehere waache. Mbona mengine yanayomkera au asiyokubaliana nayo anapinga hapohapo?
 
Mziki wa mhe rais hakuna mpinzani yeyote yule anayeweza kuucheza.
upinzani tukubali tu hadharani kua huyu mhe ametuzidi uzito.

Kwa huu mziki wake akitembea nao mpaka 2020, itakua haina haja ya kuingia gharama za uchaguzi wa rais.
 
Tunasema haya tukiwa na tumejazwa na kuona nuru mbele yetu.Kwa miaka 30 hatukuwa na Kiongozi wa nchi anayetambua wajibu wake sawa sawa.

Tunasema haya ya kumuomba Magufuli afikirie na aone umuhimu wa kuendelea kuisaidia nchi baada ya muda wake kumalizika hadi hapo atakapopatikana kiongozi atakayeweza vaa viatu vya Magufuli.

Tunasema mambo haya hadharani bila kificho kuanzia sasa kuwa sisi wengine ni wapinzani wa mambo ya hovyo ya CCM kwa muda mrefu lakini kwa anayoyafanya Magufuli tuko naye na tutamhitaji tena kwa muda mrefu sana ikiwa atakuwa Nazo nguvu za kiakili na kimwili.

Tunasema mambo haya ya kumuongezea Magufuli muda kwa sababu utendaji kazi wake mzuri hauwezi kuwa out-weighed na Katiba.

Tunasema mambo haya mchana kweupe kwamba Katiba ipo ili itusaidie kupata viongozi wema na wenye kujua na kufahamu shibe zetu.

Mkuu hii post yako nimeipenda kwani imeshiba nondo haswa. Ukiweza hebu rudi post yangu namba 18 uone sisi wengine tunashauri nini kwenye hiki kiashiria. Kisha tuendelee na mjadala.
 
Mkuu hatukatai hata akitawala miaka 200 sio shida kwani sio wote tunapenda kuwa marais. Ila tunahoji unafuu ni upi katika maisha yetu mpaka tutake atawale zaidi ya miaka 5 na iwapo atafanikiwa basi atawale 5 mingine ya mwisho? Hayo madini mpaka sasa hatujaona mafanikio zaidi ya kulianzisha. Ilibidi tusubiri tuone matokeo chanya ya maisha yetu hapo ndio tufikirie hilo mnalotaka nyie. Nakupa mfano mdogo tu. Kabla ya yeye kuingia madarakani alikuta sukari ni 1,800-2,000@kg. Akalianzisha kama alivyolianzisha sasa kwenye madini, matokea ya vurugu ile sukari sasa imepanda mpaka 3,000@kg na amekaa kimya!! Sasa kama suala hilo dogo tu liko hapo tukimuongezea miaka zaidi ya 10 si ndio tutanunua sukari 50,000@kg. Ile 50m kila kijiji sasa hivi wala haiongelewi tena.

Ni kipi kimekuwa nafuu ambacho tunaweza kweli kutembea kifua mbele kwamba sasa kweli tunajivunia? Ni kweli kuanza kufuatilia hao mafisadi wa mali zetu ni jambo jema. Je hiyo pekee italeta unafuu kwenye maisha yetu au ni yeye atapata sifa binafsi na kwa sasa anataka sifa hiyo pia chama chake kizipate. Ilibidi tusubiri wangalau akiwa amefikisha miaka 8 madarakani hapo tungeweza kuwa kwenye nafasi ya kutaka aongezewe muda.
Binafsi hata akileta neema ya " kufa MTU" aondoke tu.Yeye kama binadamu kama binadamu yeyote( aliyezaliwa,akakua na atakufa) sioni sababu ya kumwendekeza.

Lazima atoke na hakuna ujinga wa kuongezewa!
 
Nasema haya kwa hasira kali sana juu ya unafiki na ujinga unapendelea nchi hii.

Nasema haya huku nchi ikiwa na mihimili miwili tu ya serikali&bunge na mahakama

Nasema haya huku kukiwa na kundi kubwa linaloendeshwa na mihemko na lisilo na mda wa kutafakari kwa kina,kundi CCM

Nasema haya huku kukiwa na kundi kubwa linaloamini kuwa Magufuli yupo juu ya katiba na lolote analosema ni sawa,hata kama wao hawalikubali.

Nasema haya huku watanzania wengi wakiwa wanaamini anachokifanya Magufuli sio wajibu wake bali ni hiyari au hisani

Nasema haya nchi ikiwa imebakiwa na watu jasiri mfano wa Tundu Lissu, wawili au watatu

Nasema haya huku viongozi watangulizi wakiwa ni watuhumiwa wakubwa wa ufisadi.

Nasema haya baada ya kumsikia rais mstaafu mwenyewe kuheshimiwa sana Ali Hasan Mwinyi akipendekeza Rais Magufuli aongezewe mda ikibidi atawale milele

Ni dhahiri sasa Magufuli atatumia ujinga wetu kujiongezea mda na wala hatahitaji nguvu kubwa,ni hizi hizi kiki za makinikia na Escrow zimeshafanikisha hilo. Kura itapigwa na Magufuli atajiongezea mda kwa mujibu wa katiba

Hongera Magufuli
Acha kupiga ramli chonganishi wewe.
Mnajitisha wenyewe halafu mnapata hasira za bure,huku watu wanawacheeeka.
Sasa hivi mmeishiwa hoja mmebaki kujitisha,hata kwa JK mlisema akiongeza sekunde mbili tu kwenye utawala wake atajuta.
 
Binafsi hata akileta neema ya " kufa MTU" aondoke tu.Yeye kama binadamu kama binadamu yeyote( aliyezaliwa,akakua na atakufa) sioni sababu ya kumwendekeza.

Lazima atoke na hakuna ujinga wa kuongezewa!
Hata hyo neema hawezi kuileta na huo uwezo hana, kiongozi mzuri huonekana mapema kwa kufata katiba na kutenda haki madictator wengi huwa hawana maono hasa wa kiafrica zaidi ya ubinafsi wa kujaza tumbo zao
 
Yeye hajasema kama atagombea, lakini huoni trend ya watu wanaotaka aongezewe muda? Inapofikia mpaka rais mstaafu anatamka hilo hadharani unategemea nini? Juzi pia tumeona waziri mkuu mstaafu Joseph Warioba akiongoza maandamo, na waandamanaji wale wakataka pia muda wa rais kuongezewa muda.

Pia nashukuru kwamba umeona hoja yangu ya unafuu wa maisha, na kwa ustadi fulani umekwepa hata kuongelea hilo la bei ya sukari. Nilitarajia angekataza hiyo hali ya watu kutaka yeye aongezewe muda ili hao wenye viherehere waache. Mbona mengine yanayomkera au asiyokubaliana nayo anapinga hapohapo?

Mkuu watu wengi hatupendi mambo ya CCM ya hovyo hovyo.Mambo kama yaDC wa Ubungo ya kuweka watu lock up bila sababu za msingi hatukubaliani nayo.Badala ya kuweka "lockup" fikra za kijinga yeye anahangaika na watu wanaotoa fikra mbadala.

Lakini hili la Magufuli kuongoza zaidi ya muda wake wa Kawaida ni jambo la mjadala wa kiafya sana.Tujengeni hoja vizuri na kwa ustadi kwa wale tusiokubaliana na hoja hiyo.

Jengeni hoja kuonyesha ni kwa namna gani kujaribu jaribu uongozi kuna tija badala ya kuendelea na mtu ambaye tumemjaribu na kweli "amelipuka" kama tulivyotaka.

Jengeni hoja vizuri kuonyesha ni kwa namna gani muda unaweza kututawala sisi hadi tukimbizane nao na kushindwa kuendelea kumtumia mtu wa kufanya mambo mema kwa sababu tu muda wake umeisha.

Jengeni hoja vizuri ni kwa namna gani ukomo wa uongozi wa uraisi hauwezi kutenguliwa ikiwa tunaye mtu aliyeonyesha uwezo wa kulisaidia Taifa.

Jengeni hoja kwa nini sasa tusiwe na Katiba inayosema kuwa kuanzia sasa kusiwe na ukomo katika Uraisi Bali ukomo utokane na performance ya Raisi husika.Kwamba ukiwa madarakani hata miezi mitano na wananchi tukaona na kujiridhisha kuwa raisi fulani aliyeko kwenye "usukani" wa Lori ameshindwa kumudu majukumu yake basi anakomea hapo hapo Mara moja.
 
Nasema haya kwa hasira kali sana juu ya unafiki na ujinga unapendelea nchi hii.

Nasema haya huku nchi ikiwa na mihimili miwili tu ya serikali&bunge na mahakama

Nasema haya huku kukiwa na kundi kubwa linaloendeshwa na mihemko na lisilo na mda wa kutafakari kwa kina,kundi CCM

Nasema haya huku kukiwa na kundi kubwa linaloamini kuwa Magufuli yupo juu ya katiba na lolote analosema ni sawa,hata kama wao hawalikubali.

Nasema haya huku watanzania wengi wakiwa wanaamini anachokifanya Magufuli sio wajibu wake bali ni hiyari au hisani

Nasema haya nchi ikiwa imebakiwa na watu jasiri mfano wa Tundu Lissu, wawili au watatu

Nasema haya huku viongozi watangulizi wakiwa ni watuhumiwa wakubwa wa ufisadi.

Nasema haya baada ya kumsikia rais mstaafu mwenyewe kuheshimiwa sana Ali Hasan Mwinyi akipendekeza Rais Magufuli aongezewe mda ikibidi atawale milele

Ni dhahiri sasa Magufuli atatumia ujinga wetu kujiongezea mda na wala hatahitaji nguvu kubwa,ni hizi hizi kiki za makinikia na Escrow zimeshafanikisha hilo. Kura itapigwa na Magufuli atajiongezea mda kwa mujibu wa katiba

Hongera Magufuli
Duh! Hatari
 
Back
Top Bottom