Rais Magufuli apokea zawadi ya sanamu ya Bikira Maria Ikulu Dar

Kuabudu Sanamu:
Hii pia ni ibada ya msingi katika dini ya Kikristo ambapo sala za waumini wake (Wakristo) huwa hazitimii bila ya kuomba na kuabudu sanamu. Masanamu yanayohusishwa zaidi katika ibada hizo ni pamoja na sanamu la mungu-mtu Yesu wa Kikristo akiwa amebebwa na mama yake (Madona) na kumpa cheo cha umama wa mungu. Yaani Theotokos (“Mother of God”), na kwenye sanamu lingine akiwa amekufa msalabani, sanamu la "Bikira Maria", sanamu la malaika na masanamu mengine mengi ya watakatifu wa Kikristo waliokufa!

Kama maandiko ya Biblia tukufu yafundishavyo, ibada hii (ya sanamu) ifanywayo na Wakristo, kiasili imetokana na watu wa mataifa (wapagani). Uthibitisho wa hilo tunaupata katika maandiko yafuatayo:
"Bali walijichanganya na mataifa, wakajifunza matendo yao.Wakazitumikia sanamu zao, Nazo zikawa mtego kwao".
(Zaburi 106:35-36).

Lakini kwa kuwa Lucifer amewapoteza wakasahau hata haya maonyo halali ya M'Mungu:

Usijifanyie sanamu ya kuchonga, wala mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, wala kilicho chini ya dunia; Usivisujudie; wala kuvitumikia; kwa kuwa Mimi, BWANA, Mungu wako, ni Mungu, mwenye wivu...
Kutoka 20:4 kjv

Kwa uchache, maandiko hayo juu yanathibitisha wazi kuwa waasisi na wahusika wakuu wa ibada hiyo (ya sanamu) ni watu wa mataifa, yaani wapagani.

Sambamba na ukweli huo, Biblia haikuacha pia kubainisha jinsi M'Mungu alivyowakemea wanadamu tangu mapema kujaribu kuchonga (kufanya) na kuabudu sanamu, kama ifuatavyo:

"Usijifanyie sanamu ya kuchonga, mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni, au kilicho chini duniani. Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi BWANA, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu, nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao".
(Kumbukumbu la Torati 5:8-9).
Chanzo: Amua Sasa: Biblia Na Mwenyezi Mungu
Kiukweli niwe muwazi bibi yangu FaizaFoxy umenigusa sana! Japo wewe ni muslim lakini umepewa hekima kubwa sana ya kutambua ni wapi wakristo tunapopingana na neno la Mungu.
Ubarikiwe sana sana sana.
 
Kiukweli niwe muwazi bibi yangu FaizaFoxy umenigusa sana! Japo wewe ni muslim lakini umepewa hekima kubwa sana ya kutambua ni wapi wakristo tunapopingana na neno la Mungu.
Ubarikiwe sana sana sana.
Huyu bibi nnachompendea anasoma biblia kuliko hata wakristo wenyewe
 
[QUOqTE="Mbassa jr, post: 23089640, member: 355366"]Kiukweli niwe muwazi bibi yangu FaizaFoxy umenigusa sana! Japo wewe ni muslim lakini umepewa hekima kubwa sana ya kutambua ni wapi wakristo tunapopingana na neno la Mungu.
Ubarikiwe sana sana sana.[/QUOTE]
Kasomeni juu ya sanamu n images in Christianity, siyo dhambi kutumia sanamu! Tena waislam Ata wasiongee kabsaa maana wanamtupiaga shetani mawe kila mwaka,
 
Tatizo ni kufa? Yesu naye alikufa so? Wewe ndiye unaamini katika kufa sisi tunaamini katika kuishi baada ya kufa. Aaminiye hatakufa na ajapokufa ataishi...Mauti imeshindwa kwa kuwa Yesu alivunja minyoriro yake alipofufuka.Pitia biblia vizuri na usome kwa unyenyekevu.


Tatizo ni kuombea watu? Hii ni ajabu sana wachungaji wengi tu wanaombea watu siku hizi lakini hambezi. Binadamu na hasa sisi wakatoliki tumeaswa kuombeana sisi kwa sisi,na tunafanya hivyo and that is biblical tena tunawaombea hata wasio na imani kama wewe, hata wanaotuudhi (kama baadhi ya wachangiaji humu) na wasiomjua Mungu. Kama binadamu wenye kupungukiwa na utukufu wanaweza kuwaombea binadamu wenzao kwa Mungu kuna tatizo gani mwenye heri na mbarikiwa mno aliyevikwa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji la nyota 12 kama Bikira Maria na watakatifu na wafia dini kuwaombea wanadamu kwa Yesu?
Watakatifu wa Mungu wangalipo duniani na mbinguni.na wote wanashirikiana kupitia kwa Yesu Kristo kutufikisha kwa baba wa mbinguni



Sent using Jamii Forums mobile app

Ndugu yangu, unaweza kunionyesha popote katika Biblia ambapo panataka Bikira maria aheshimiwe kama mnavyo jaribu kuaminishwa??
 
Ndugu yangu, unaweza kunionyesha popote katika Biblia ambapo panataka Bikira maria aheshimiwe kama mnavyo jaribu kuaminishwa??
Luke 1. 48
For he has looked upon his handmaid’s lowliness;

behold, from now on will all ages call me blessed.y
 
Jer.31
[1] At the same time, saith the LORD, will I be the God of all the families of Israel, and they shall be my people.
[2] Thus saith the LORD, The people which were left of the sword found grace in the wilderness; even Israel, when I went to cause him to rest.
[3] The LORD hath appeared of old unto me, saying, Yea, I have loved thee with an everlasting love: therefore with lovingkindness have I drawn thee.
[4] Again I will build thee, and thou shalt be built, O virgin of Israel: thou shalt again be adorned with thy tabrets, and shalt go forth in the dances of them that make merry.
[5] Thou shalt yet plant vines upon the mountains of Samaria: the planters shall plant, and shall eat them as common things.
[6] For there shall be a day, that the watchmen upon the mount Ephraim shall cry, Arise ye, and let us go up to Zion unto the LORD our God.
[7] For thus saith the LORD; Sing with gladness for Jacob, and shout among the chief of the nations: publish ye, praise ye, and say, O LORD, save thy people, the remnant of Israel.
 
Haya mambo ya udini hayakupaswa kunasibishwa na taifa kwa maana ya kutuhabarisha. Kwa kuwa ni mambo ya kiimani yalipaswa kufanywa pembeni ya kamera. Hayo ni mambo binafsi ya Rais na imani yake ya kidini. Sasa tunaonyeshwa ili iweje? Hilo sanamu linatusaidia nini sisi kama taifa?
 
Kiukweli niwe muwazi bibi yangu FaizaFoxy umenigusa sana! Japo wewe ni muslim lakini umepewa hekima kubwa sana ya kutambua ni wapi wakristo tunapopingana na neno la Mungu.
Ubarikiwe sana sana sana.
Ukiacha hayo maneno kumuhusu Yesu mengine yote uliyoandika ni kweli tupu ajabu wale wajiitao wakristo hawajui hayo wanaendeleza ibada ya sanamu
 
Awamu hii msitegemee Kanisa Katoliki litasema kitu kuhusu huyu jamaa.

Bila shaka "waliongea mengi" (Kilichompeleka) ndio wakapeana hiyo zawadi.

Mkuu hao kanisa katoliki wanajulikana kwa unafiki hatuwashangai. Kwa yanayoendelea nchini hivi sasa angekuwa Rais ni Muislam ungeona kukithiri kwa matamko ya kanisa dhidi ya utawala. Huyu wa sasa ni mwenzao wamefyata mikia yao kama hawapo vile.
 
Mkuu mimi shida zangu zote huzitupa kwake na huwa najitupa miguun pake na huwa ananiokoa ile mbaya wengine ni bakhita, inyasi na thadei

Sent using Jamii Forums mobile app

Unaacha kumuomba Mungu wa kweli unaabudia masanamu! Hizi dini nyingine hizi yaani basi tu! Unakuta mtu na PhD yake analiabudu na kulinyenyekea sanamu huku akiamini ndilo linalomtatulia matatizo yake. Hatari sana hii.
 
Mwanamke aliyezaa na kunyonyesha mtoto hadi akakua anaendeleaje kubaki bikra?!! Hizi imani nyingine bhana!
 
Basi watu povu linawatokaaaa..
Kwani mkipita bila kukashifu inawacost nini
Ndio keshapokea sanamu na hilo zinawad yake yy na familia .
KAMA HUTAKI ..KUNYA BOGA...

Kama ni zawadi yake yeye na familia yake humu limefuata nini? Kwa nini watujulishe mambo yao ya kiimani? Usikute hilo sanamu ni la dhahabu na ni rushwa iliyotolewa kwa kiongozi kwa mgongo wa imani ili kushawishi baadhi ya maamuzi.
 
Ukitaka kujua nguvu ya Mama wa Mungu Bikira Maria fanya novena kupitia yeye,alikamyanga shetani(joka)kwa miguu yake,ndio kimbilio letu

hakuna tatizo kabisa kila mtu na imani yake hata angempa rozali ni sawa kabisa humu ndo mkuza mambo,akiwa ndo mama yetu tunayemheshimu hakuna tatizo kabisa.

sitashangaa wakienda dhehebu lingine na kumkabithi Biblia hakuna tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app

Acha uongo Mkuu. Angekuwa na nguvu hizo angemuokoa mwanaye pale msalabani! Mbona alimuacha Warumi wakamsulubu? Uongo mwingine uangalie na pa kuupeleka.
 
Bikira Maria mama wa Mungu utuombee.

Sent using Jamii Forums mobile app

mama maria amekufa na hakuna kumbukumbu ya kuwa anaishi popote. hana uwezo wa kukuombea hivi sasa. ngoja nikupe contact ya unakoweza kupeleka maombi yako hapa chini:

piga simu moja kwa moja kwa Yesu mwana wa Mungu aliye hai anayeweza kusamehe makosa mwenyewe. Piga moja kwa moja usije kutapeliwa. Simu yake iko wazi masaa 24 siku saba kwa wiki. maombi yako yatajibiwa kwa wakati unaofaa.
 
Madanganyo ya ukatoliki kuhusu dhambi ya asili:

Je! Umewahi kuona uso wa mtoto aliyezaliwa, ukagusa ngozi nyembamba ya mashavu yake ya rangi nyororo, na ukahisi hatia yake wakati ukiangalia macho yake mazuri? Kwa kulinganisha kabisa, mafundisho ya Kikatoliki yanasema kwamba "watoto wadogo huzaliwa na dhambi!" Katekisimu ya Kanisa Katoliki inasema hivi:


Yeyote aliyezaliwa na asili ya kibinadamu iliyoanguka na kuharibiwa na dhambi ya awali, huhitaji kuzaliwa upya katika Ubatizo ili kuwekwa huru na nguvu za giza na kufanywa watoto wa Mungu, ambako watu wote wanaitwa (1994)

Kwa upande wake Bibilia ambayo ndio kiongozi wa kweli za Mungu inafundisha kwamba watoto hawarithi dhambi za wazazi wao (Kutoka 32: 32-33, Kumbukumbu la Torati 24:16, 2 Wafalme 14: 6, 2 Mambo ya Nyakati 25: 4, Yeremia 31:30; Ezekieli 18:20). Hata hivyo, Wakatoliki huharakisha kusema kwamba Daudi alisema: "Tazama, nilizaliwa kwa uovu, na mama yangu aliniumba kwa dhambi" (Zaburi 51: 5). Ili kuelewa kifungu hiki, ni lazima tukumbuke kwamba sura ya Zaburi 51 ni dhambi ya Daudi, si dhambi ya awali. Fikiria lugha alizotumia Daudi kuonyesha kwamba dhambi aliyokuwa akizungumzia ni dhambi aliyofanya: "Ondoa makosa yangu" (mstari wa 1); "Nioshe kabisa uovu wangu, na kunitakasa kutoka kwa dhambi yangu" (vs. 2); "Ninakubali makosa yangu, na dhambi yangu daima i mbele yangu" (mstari wa 3); "Kwako Wewe, Wewe pekee, nimefanya dhambi" (mstari wa 4); Hakuna hata uhusiano mdogo kwa aina fulani ya dhambi ya asili katika maombi ya mtunga-zaburi. Kwa kweli, ilikuwa ni kutokana na dhambi yake na makosa ambayo mtunga-zaburi aliyafanya na alitamani kuokolewa kutoka kwayo.

Lakini, kwa nini alielezea wakati ambapo aliumbwa tumboni mwa mama yake? Mtunga Zaburi aliluwa akitumia kauli ya kinyenyekevu zaidi ambayo ukiipima vizuri haikumsisha na dhambi za wazazi wake (tazama Zaburi 58: 3). Kauli hii ilikuwa na lengo la kusisitiza hali ambayo mama yake alimzaa katika ulimwengu uliofunikwa, kukabiliwa, na kuathiriwa na dhambi ingawa yeye mwenyewe hakuzaliwa na dhambi.
 
Back
Top Bottom