Rais Magufuli apiga tena simu Clouds, amsifu Diamond na kusema atashughulikia kero za wasanii

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,189
2,970
Habari wakuu,
Leo msanii wa muziki wa kizazi kipya akiwa kwenye mahojiano kituo cha runinga cha Clouds, alilalamikia kuhusu kazi za wasanii kuibiwa na kumuomba Rais Magufuli afanyie kazi hilo kwa uharaka kama anavyofanya kwenye mambo mengine.

Ghafla Rais Magufuli akapiga simu, akasema amelisikia na atalifanyia kazi, kampongeza Diamond kwa kuwa na watoto, kasema anampenda na kupenda wasanii wote ikiwemo waigizaji, pia ameonyesha kuwakubali Shilawadu.

Pamoja na mambo mengine, Diamond alimshukuru Rais mstaafu, Jakaya Kikwete kwa kuwasaidia kuwawekea stika kwenye kazi zao.

Aongelea madawa ya kulevya na kusema tuhuma zinakosesha dili nyingi na inaharibu na inakosesha kazi tofauti na kampuni hujitenga na watu wanaojihusisha. Ambao namna ya kuwasafisha watu ambao wanabainika hawatumii na imsaidie jinsi ya kurudisha carrier yake.

Alipoulizwa kuhusu Paul Makonda kuchafuka na uhusiano na brand yake kwani ni sehemu ya walezi, amesema kila binadamu ana mazuri yake na mabaya yake na hamna mtu aliekamilika, Amesema pamoja na mapungufu yake ndie mtu aliepata uthubutu wa kwenda kutangaza watu na angeamua angefanya kimya kimya na kuchukua pesa za watu. Amedai pale alipokosea aelekezwe na hamna mtu aliekamilika

 
Kama kawa dawa, mh. Rais amejitokeza tena Cloud kwa kupiga simu mubashara akimpongeza Diamond na rebo yake ya WASAFI.

Kaahidi kukutana na wasanii soon !

Big up mh. Rais.
 
Akizungumza mubashara muda mfupi tu uliopita Mheshimiwa Rais JPM amesema kuwa amefurahushwa kujua kuwa Msanii Diamond ni mwana CCM na kwamba hata yeye anampenda mno na kwamba anakipenda mno Kituo cha Clouds tv hasa Kipindi cha 360 na ni Mdau wa Kutukuka wa Kipindi maarufu cha SHILAWADU.

Mheshimiwa Rais aliamua kupiga Simu Kituoni hapo baada ya Diamond kutoa malalamiko yake kuwa Serikali imewatupa Wasanii na kwamba anaomba msaada ndipo Rais akapiga Simu na kumuahidi Diamond na Wasanii wote nchini Tanzania kuwa atawasaidia.
 
Back
Top Bottom