Rais Magufuli aongea na wananchi akiwa njiani akielekea Singida

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,950
29,532
Rais JPM amelazimika kusimama kwa muda na kuongea na wananchi wa Dakawa baada ya kusimamishwa alipokuwa safarini kuelekea Singida.

Amewataka wananchi kuvuta subira na kutovunja sheria wakati serikali ikiendelea na jitihada za kutatua migogoro inayowakabili.

Chanzo: Mdau kutoka Morogoro

Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiongea na wananchi Msamvu mkoani Morogoro mchana wa leo wakati akiwa njiani kulekea Mkoani Dodoma kwa kwa njia ya Barabara, pamoja na kukagua barabara ya Morogoro-Dodoma eneo la Kibaigwa

Kesho anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Sherehe za Miaka 39 ya Chama cha Mapinduzi (CCM) zitakazoadhimishwa Kitaifa mkoani Singida.
 
Chama ndo uphill task yake; Nasubiria kauli kinzani kuhusu hotuba ya jana & zilizopita kutoka kwa M/kiti na wafuasi wake (wafia chama)! Kweli tumuombee huyu jamaa, ana kazi sana.
 
Wakita wafe kwa pressure mwaenyekiti asihutubie apewe jonh ndio ahutubie watakoma watakayokuwa wameandika yeye atoyasoma atasema ya kwake ya kutumbua majipu
 
Wakita wafe kwa pressure mwaenyekiti asihutubie apewe jonh ndio ahutubie watakoma watakayokuwa wameandika yeye atoyasoma atasema ya kwake ya kutumbua majipu
Jamaa hajapanda ndege??
Ila JK lazima apande ndege ule ugongwa wake alipimwa na dr mzungu nadhani hatakiwi akae kwenye kiti umbali mrefu
 
Ndege ipi mkuu, Moshi alienda na ndege
Rais hajawahi fanya ziara yoyote Mkoa wa kilimanjaro, mpaka sasa Kafanya Dodoma, Zanzibar, na Arusha huko Mosi kaenda lini? Kesho atakua singida kwenye maadhimisho ya miaka 39 ya CCM,
 
Rais hajawahi fanya ziara yoyote Mkoa wa kilimanjaro, mpaka sasa Kafanya Dodoma, Zanzibar, na Arusha huko Mosi kaenda lini? Kesho atakua singida kwenye maadhimisho ya miaka 39 ya CCM,
Uwanja wa KIA upo moshi mkuu, wakati anaenda Arusha alitumia uwanja wa KIA na aliongea na wakazi wa KIA JUNCTION.
 
20160205031049.jpg
 
Back
Top Bottom