Rais Magufuli anawafundisha wapinzani kufanya siasa za Mwalimu Nyerere

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,297
2,000
Mwaka 2016 ulikuwa mgumu kwa vyama vya upinzani. Ugumu uliongezeka zaidi pale vyama vilipokatazwa kufanya mikutano ya hadhara japokuwa ni haki yao ya kimsingi inayotolewa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Rais John Magufuli ndiye alitoa tangazo hilo la kuzuia mikutano ya vyama vya siasa. Tangu wakati huo, imekuwa ikiaminiwa kuwa vyama vya upinzani vitakufa kwa sababu havitaweza kujiuza kwa wananchi.

Hisia hizo kuwa upinzani utakufa ni hofu tu na siyo uhalisia. Vyama vya upinzani vina nafasi nzuri ya kufanya siasa tofauti. Siasa ambazo zina nguvu na kuchochea mabadiliko ya haraka kuliko mikutano ya hadhara.

Mwaka 2017, wapinzani wajielekeze kufanya siasa ambazo zilitumiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere. Siasa za kujenga fikra kwa mtindo wa kunong’onezana.

Katazo la Rais Magufuli la kutofanya mikutano ya hadhara, linafundisha zaidi vyama vya upinzani kuimarisha ofisi zao za mikoani, wilaya, tarafa na kata ili watendaji wake wawafikie wananchi.

Wapinzani wakiamka mwaka 2017, watamshukuru Rais Magufuli kwa uamuzi wake wa kukataza mikutano, maana amewapa akili ya kwenda chini kabisa na kuwagusa watu wengi na kwa ukaribu.

Miaka yote wapinzani wamekuwa wakifanya mikutano ya hadhara ambayo haijawapa matokeo bora. Wakati huu wanatakiwa kuwasiliana na wananchi bila vipaza sauti. Wafanye siasa za elimu na ushawishi kwa hoja za ana kwa ana.

Agizo la Rais Magufuli la kupiga marufuku mikutano ya hadhara, linawapa somo wapinzani kufanya siasa za mlango kwa mlango (Canvassing). Siasa za “ukielewa somo nenda kamwelimisha jirani na rafiki kisha rafiki akaseme na rafiki yake.” Hizo ndizo siasa ambazo kwa sehemu kubwa zililikomboa Bara la Afrika.

Utekelezaji wa siasa hizoSiasa ambazo wapinzani wanatakiwa kufanya wakati huu ni kuachana na mtindo wao wa kutumia fedha nyingi za ruzuku makao makuu, badala yake wazitengenezee mfereji ili ziwe zinaingia na kushushwa chini ili watendaji wa chini watekeleze siasa za wakati.

Watendaji wakawaelekeze wanaume kuzungumza wao kwa wao kwenye mikutano ya kijamii, kama vile baa, vilabu vya pombe, wanapokuwa kwenye mpira na michezo mfano bao, drafti, pool, vilevile vijiwe vya kahawa.

Wanawake wafanye majadiliano wanapokuwa kwenye sehemu za ususi, Vicoba, wanapokutana kuchota maji, wanapokwenda kwenye mashine za kukoboa na kusaga nafaka na maeneo mengine.

Hizo ndizo siasa ambazo zilithibitisha umahiri wa Bibi Titi Mohamed alipokuwa akieneza mawazo ya kudai uhuru kwa watu wa chini kabisa. Siasa ambazo Mwalimu Nyerere alizipenda kwa sababu zina ushawishi mkubwa kuliko mikutano ya hadhara.

Mkutano wa hadhara, unaweza kufanya mikutano 100 na kuhutubia watu 10 milioni, lakini ukaondoka ukiwa huna uhakika wa watu walioelewa hotuba na kufuata mawazo yako.

Mikutano ya ana kwa ana huwa na matokeo ya papo kwa papo, maana unazungumza na mtu unamwelewesha, hapohapo unamsoma kama ameelewa au hajaelewa, kwa hiyo ni rahisi kumuingiza kundini kama kaelewa au kumpangia wakati mwingine, ikiwa hajaelewa.

Katika kitabu cha TANU Women Gender and Culture in Making of Tanganyika Nationalism, 1955-1965 (Wanawake wa TANU, Jinsia na Utamaduni katika Kujenga Utaifa wa Tanganyika, 1955-1965), kilichoandikwa na Profesa wa Historia ya Afrika, Susan Geiger, ndani yake kuna nukuu ya Bibi Titi.

Katika nukuu hiyo, Bibi Titi alisema: “Tuliwafikia watu mpaka kwenye vilabu vya pombe, tuliwachukua na kwenda nao ofisi za Tanu. Wanaume walisikiliza hotuba za Mwalimu Nyerere lakini waliogopa, wanawake walikuwa wepesi kujiunga.

“Watu walipanga mstari ofisi ya Tanu kununua kadi. Wanaume waliwapeleka wake zao kuwanunulia kadi. Wengine waliogopa kuhifadhi kadi za Tanu kwenye nyumba zao, mimi nilizichukua na kuwahifadhia.”

Maneno hayo kwa ufupi wake ni kuonesha kuwa haikuwa rahisi kwa Mwalimu Nyerere na washirika wake kuipatia uhuru Tanganyika, bali walijitoa hasa kuwafikia watu.

Wapinzani pia hawatakiwi kulalamika kunyimwa mikutano ya hadhara, bali sasa wajitanue, ofisi za wilaya mpaka kata ziwe hai. Matawi yatumike vizuri na mengine yafunguliwe. Watendaji wa matawi wawezeshwe kufanya kazi ya uenezi wa chama, hivyo ndivyo wataweza kufikia malengo ya kuiondoa CCM madarakani mwaka 2020 au kupata matokeo bora zaidi.

Siasa za mjini hazifai

Mikutano ya hadhara ni siasa za mjini na mara nyingi huwa na matokeo ya uongo. Utajaza mkutano na utaondoka unajisifia kwamba umefanikiwa na unakubalika, kumbe wengine walihudhuria tu lakini hawaguswi.

Wapo mashabiki hasa wa siasa na kwenye mikutano ya hadhara wanajaa lakini wakati wa kuchagua hawapigi kura. Siasa za ana kwa ana, huwaelimisha wasiopiga kura na kuzaa matokeo muhimu kwa wasio na upande.

Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine za Afrika, vyama vya upinzani vimekuwa vikipata matokeo mazuri mijini lakini vinaanguka vijijini. Sababu ni kuwa vyama hivyo haviwafikii watu vijijini.

Mwaka 2017, wapinzani wanatakiwa kujielekeza kuimarisha ofisi zao za vijijini na kuwawezesha watendaji kufanya kazi ya uenezi kwa mtindo wa nafsi kwa nafsi. Lazima vyama vijipapambanue kwa upana na kujieleza kinagaubaga kwa nini vinataka viaminiwe na kupewa dola?

Huwezi kwa sasa kubaki unasema kuwa wananchi wa vijijini ndiyo wanaokibeba chama tawala, wakati vyama vya upinzani vinashindwa kujisogeza karibu yao. Mpigakura hawezi kukichagua chama ambacho hakijui au anakiona kwa mbali.

Mikutano ya hadhara na kujaza watu kwa wingi ni siasa za marembo na ndiyo huwazubaisha wapinzani kudhani wanakubalika kwa kiasi cha kushinda dola lakini matokeo huonesha tofauti. Vyama vijielekeze kwenye siasa za kujenga ukaribu na wananchi wa chini kabisa kisha vitaona matokeo makubwa mwaka 2019 katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Uchaguzi Mkuu 2020.

Siasa za mageuzi ya fikra

Mwalimu Nyerere alipotaka kujenga fikra za Watanzania kupitia siasa za Ujamaa na Kujitegemea alijikita katika kuchapisha vitabu na machapisho mbalimbali yenye kutoa elimu mahsusi.

Hapa nchini, hakuna vyama ambavyo vinatumia njia hiyo. Ofisi za vyama kuanzia taifa mpaka kata, inatakiwa kuwe na vitabu na machapisho ambayo mtu akisoma anaelewa misingi ya chama na madhumuni yake ya kuijenga nchi kama kitapewa dhamana ya dola.

Vyama vimenyimwa kufanya mikutano ya hadhara, basi fedha ambazo zingekuwa zikitumika kuandaa mikutano hiyo, zielekezwe kwenye kuandika na kuchapa machapisho na vipeperushi ambavyo wananchi watagawiwa kwenye maeneo yao.

Mfano; Mgombea Urais wa Chadema mwaka jana, Edward Lowassa, hivi karibuni alikosoa ununuzi wa ndege mpya unaofanywa na Serikali kwa sasa kwa sababu siyo kipaumbele.

Inawezekana hoja ya Lowassa ikawa nzuri lakini wangapi wataisikia na kuielewa? Kama chama chake kingeandaa hoja hiyo kwenye chapisho dogo au vipeperushi, kisha kusambazwa, ujumbe ungefika chini zaidi kwa watu wa vijijini.

Hoja ya Lowassa ni kuwa badala ya ndege, Serikali ingejikita kuwapa watu wake maji safi na salama. Hoja hiyo imesikika zaidi mijini ambako shida ya maji siyo kubwa. Ingepelekwa vijijini na watu kueleweshwa namna ambavyo ndege siyo muhimu kuliko maji ni rahisi kupata uungwaji mkono.

Vyama vya upinzani kwa wakati huu ambao vimekatazwa kufanya mikutano ya hadhara, vijikite katika kufanya siasa za ujenzi wa fikra za watu. Mtu mmoja akielewa na kushiba misingi ambayo chama inasimamia, atakuwa mwalimu mzuri kwa wengine.

Hivi sasa vyama vya upinzani na hata CCM, ukiacha viongozi, hakuna watu ambao wanaweza kushawishi kwa hoja. Wengi wao kelele nyingi na kushambuliana kwenye mitandao ya kijamii. Hawatakiwi watu wa kushambulia, bali wenye kuelimisha.

Anayeshambulia huchukia, ila anayeelimishwa huelimika. Vyama vinahitaji watu wengi watoa elimu kwa wakati huu, ili wavifikishe mbali kwa haraka na uhakika.

Eneo hilo la kujenga fikra litumike vizuri kwenye mitandao ya kijamii. Vyama vinatakiwa viwe na watu ambao wanatumia vizuri jukwaa la mitandao ya kijamii. Kuyatazama mambo kwa jicho pana na kuelimisha.

Vyama viwe na utaratibu kuanzia makao makuu kuwa vinaandaa masomo ya kila mwezi kisha watu wanayachukua na kuyasambaza mitandaoni na watendaji wa vyama kuyafikisha kwa wananchi wa kawaida mpaka vijijini.

Chanzo: Maandishi Genius
 
Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
24,802

Mcubic sijamaliza kusoma article yote, lakini hii sentensi (......, Mwalimu Julius Nyerere. Siasa za kujenga fikra kwa mtindo wa kunong’onezana.) Kwa Nyerere was simple by this technique, kwa sababu the enemy was common to all- adui wetu alikuwa mmoja- mkoloni, we were not divided. Sasa tuko highly divided! Bado andiko lako lina mantiki kubwa
 
McFerson

JF-Expert Member
Jan 8, 2015
1,823

Kwahiyo ndio ukaamua kunukuu Uzi mzima,
 
mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,297
2,000
Mcubic sijamaliza kusoma article yote, lakini hii sentensi (......, Mwalimu Julius Nyerere. Siasa za kujenga fikra kwa mtindo wa kunong’onezana.) Kwa Nyerere was simple by this technique, kwa sababu the enemy was common to all- adui wetu alikuwa mmoja- mkoloni, we were not divided. Sasa tuko highly divided! Bado andiko lako lina mantiki kubwa
Upo sahihi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom