Rais Magufuli Anaposema Niombeeni Ana Maanisha Anakazi Nzito "Kila Upande Ni UOZO

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,804
34,193
Pesa ya wafisadi.jpg


Rais Magufuli Anaposema Niombeeni Ana Maanisha Anakazi Nzito "Kila Upande Ni UOZO Mtupu"


PESA ZILIZOPIGWA NA WAJANJA NSSF NI MARA 3 YA PESA ZILIPIGWA NA WAJANJA WA ESCROW...

HEKARI MOJA ILINUNULIWA KWA SH MILLION 800 BADALA YA MILLION 4 .5.

Katika miradi yote inayosimamiwa na NSSF ya Arumeru na Kigamboni serikali imeingia hasara ya Tshs Trillioni 1.3
Mradi wa Kigamboni wasimama, kuna ufisadi wa zaidi ya Tshs Billioni 179Mikataba yasainiwa kimagumashi bila kufuata sheria, wajenzi ni Waturuki.Ardhiya kigamboni ilinunuliwa kwa Tshs millioni 800 kwa hekari wakati ilitakiwa inunuliwe kwa Tshs Millioni 4.5 kwa hekari.Arumeru ardhi ilinunuliwa kwa Tshs Billioni 1.8 kwa hekari wakati thamani ya hekari moja ni Tshs laki 5 mpaka Millioni 1.
Taratibu za ununzi wa ardhi zilifanyika kimya kimya bila kumshirikisha mwanasheria wa serikali.=============================================


Mradi mkubwa wa ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni jijini Dar es Salaam uitwao Dege Eco Village, ulioanzishwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) umesimama huku ikiripotiwa kuwapo kwa ufisadi wa zaidi ya Sh179 bilioni katika mradi huo.
Mchoro wa mradi huo ulioanzishwa mwaka 2014 kwa gharama ya Dola za Marekani 653 milioni (Sh1.3 trilioni) unaonyesha utakapokamilika utachangia kubadili sura ya jiji la Dar es Salaam kwani kutakuwa na nyumba za kifahari, majengo ya hoteli, maduka makubwa, eneo la wazi la mapumziko, baa, shule, hospitali, kumbi za mikutano, nyumba za ibada na migahawa.

Hata hivyo, mradi huo unaosimamiwa na kampuni ya Hifadhi Builders Limited iliyoanzishwa na Bodi ya NSSF kwa ushirikiano na kampuni ya Azimio Housing Estate Limited (Ahel), huku wajenzi wakiwa kampuni ya M/s Mutluhan Construction Industry Company Limited kutoka Uturuki, huenda usikamilike kwa muda uliopangwa kwani umesimama tangu Januari, ingawa unadaiwa utaanza tena mwezi huu.

Ofisa mmoja mwandamizi wa Serikali ameliambia gazeti la Mwananchi kwamba ujenzi wa nyumba za Dege Eco Village ni miongoni mwa miradi ya kisasa ambayo NSSF imekaguliwa na kubainika kufisadi fedha baada ya kuingia mikataba bila kufuata taratibu, kanuni wala sheria za nchi.
Kwa mujibu wa ofisa huyo, ripoti ya ukaguzi iliyoishia Juni 2015, uliofanywa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akishirikiana na taasisi ya kimataifa ya ukaguzi ya Ernst and Young imeanika ufisadi mkubwa unaotishia usalama wa fedha za wanachama wa shirika hilo.

Mtoa habari huyo amesema mradi wa nyumba za kisasa wa Kigamboni unaojengwa katika ekari 300, unakabiliwa na kashfa baada ya kubainika kuwa NSSF imenunua ekari hizo kutoka kwa mbia mwenzake Azimio Housing Estate Limited kwa zaidi ya Sh800 milioni kwa ekari, wakati shirika hilo linamiliki viwanja vingine maeneo hayo vyenye thamani ya Sh4.5 milioni kwa ekari.

“Ukipata ripoti hiyo ya ukaguzi utaweza kuona ilivyochambua miradi mbalimbali ya ujenzi jijini Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Pwani na Mtwara. Kwa mfano mradi wa Arumeru mkoani Arusha, NSSF imenunua viwanja kutoka Azimio kwa Sh1.8 bilioni kwa kila ekari,” alieleza ofisa huyo.

Uchunguzi unaonyesha kwamba Bodi ya NSSF na Azimio walitiliana saini Novemba 15, 2013, kuhusu uendeshaji wa miradi mbalimbali. Azimio walijieleza kuwa wanamiliki ardhi yenye ukubwa wa ekari 20,000 Kigamboni, ekari 655.3 Arumeru, ekari 7,832.7 Pwani, ekari 200 Mwanza, ekari 5,723.6 Mtwara, na kwamba maeneo hayo yanafaa kwa ujenzi wa miji ya kisasa.
Taratibu ziliitaka NSSF kujiridhisha kuhusu uwepo wa ardhi hiyo, uhalali wa kisheria wa Azimio kumiliki eneo hilo pamoja na thamani halisi ya ardhi hiyo kutoka mamlaka zinazohusika. NSSF hawakufanya hivyo na wala hawakumshirikisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

“Napenda kukuthibitishia kwamba NSSF waliridhia bila ya kujiridhisha kuhusu uwapo wa ardhi hiyo bali walitiliana saini miradi ya pamoja kujenga nyumba Kigamboni na Arumeru bila kujiridhisha,” alisema ofisa huyo.

Mradi wa Kigamboni una thamani ya Dola za Marekani 653,436,675 (Sh1.3 trilioni), na mradi wa Arumeru thamani yake ni Dola 3,340,589,543 hadi utakapokamilika.
Tatizo jingine kubwa ni kuhusu umiliki wa mradi. Uchunguzi unaonyesha mkataba wa mradi huo uliitaka Azimio kuchangia asilimia 55 zikiwamo ekari 300 ambazo ni sawa na asilimia 20 ya mradi, huku NSSF ikichangia asilimia 45. Uchambuzi unaonyesha Azimio imetoa ekari 300 za Kigamboni kwa Dola 108,906,113, na ekari 655.3 za Arumeru kwa Dola 556,764,924.

Kwa hiyo kwa miradi miwili hiyo, NSSF ‘imenunua’ ardhi yenye thamani ya Dola 665,671,037 (Sh1.33 trilioni) kutoka Azimio.

Uchunguzi unaonyesha kuwa Serikali imekasirishwa na hatua ya taasisi hiyo ya umma ‘kununua’ ekari moja ya ardhi kwa zaidi ya Sh800 milioni huko Kigamboni, wakati bei halisi ya ardhi iliyotangazwa na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke mwaka 2012 wakati ikiuza viwanja vyake ilikuwa Sh8, 000 kwa mita za mraba, kwa hiyo ekari moja ilikuwa Sh39 milioni.

Vilevile, NSSF yenyewe ilikuwa inamiliki ekari 267 Kigamboni ilizonunua kutoka kampuni ya Georgia Homes (T) Ltd kila moja kwa Sh4.5 milioni, hivyo hatua ya shirika hilo ‘kununua’ ekari moja kwa Sh800 milioni kutoka Azimio haikubaliki.

Hata mradi wa Arumeru, NSSF pia imebainika kufuja fedha kutokana na kukubali kununua ekari moja kwa Sh1.8 bilioni, kinyume na thamani halisi ya viwanja kwenye eneo ambalo lipo kilometa 30 kutoka Jiji la Arusha. Uchunguzi umebaini wenyeji wa eneo hilo wanauza ekari moja kwa bei kati ya Sh500, 000 na Sh1 milioni.

Hatua ya NSSF ‘kununua’ ekari 300 Kigamboni kila moja kwa Sh800 milioni imesababisha hasara ya Sh179 bilioni na ekari 655.3 Arumeru kununuliwa kila moja kwa Sh1.8 bilioni imeingiza hasara ya Sh1.165 trilioni. Kwa hiyo, miradi miwili hiyo imeingiza hasara ya Sh1.3 trilioni.

“Tusubiri, lakini nina uhakika watu ambao kwa uzembe, walilishauri shirika kuingia kwenye matatizo haya na kuhatarisha fedha za wanachama lazima watawajibishwa ili kuepusha matatizo mengine yajayo kwa fedha za wanachama wa mfuko,” alisema ofisa huyo.

Ofisa huyo alisema kwamba hadi ukaguzi ulipofanyika shughuli zote hata manunuzi ya vitu muhimu kwa ajili ya mkandarasi zilikuwa zinafanywa na NSSF pamoja na mawasiliano na wasambazaji wa huduma. Hadi wakati wa ukaguzi, NSSF ilikuwa imeingiza kwenye mradi Sh205.141 bilioni na hazikuwapo nyaraka zilizoonyesha mchango wa Azimio mbali ya ardhi.

chanzo.‎Fouard SomiMagazeti ya Tanzania - www.magazetini.com
 
Nchi hii imehujumiwa sana....nampongeza Rais kwa nia yake njema. Atende haki na kila mtu avune alichopanda
 
Kaguzi zimekua zikianika maovu sana ishu nobody cared back then
 
JULIUS MTATIRO.jpg



Mtatiro leo ameamka na hili juu ya ufisadi wa NSSF

EKARI MOJA YA ARDHI, BILIONI MOJA- WIZI WA KIWANGO CHA PhD!

Mtatiro J


Napitia hii ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) juu ya NSSF. Kwamba shirika hilo la umma lilitumia TZS 250,787,041,800 (Shilingi Bilioni Mia Mbili Hamsini na Milioni Mia Saba) kununua ekari Mia tatu za ardhi katika mji wa Kigamboni. Kwa hiyo kila ekari moja ilinunuliwa kwa TZS 835,956,806 (Shilingi Milioni mia nane thelathini na tano).

Kama kuna watu wamesomea wizi kwa kiwango cha PhD basi hapa Tanzania tunaongoza. Yaani ardhi ya Kigamboni inauzwa ekari moja kwa takribani shilingi milioni elfu moja (bilioni 1)! Pesa za wanachama wa NSSF! Pesa za umma! Kama ni kwenye mpira wa leo (soka) basi aliyetufundisha ni Lionel Messi!

Na Jana nimemsikia JPM anasema meli zaidi ya 60 zilizoingia kwenye Pwani ya Tanzania (Bandarini) zilipotea katika mazingira ya kiutatanishi. Nikajisemea kimoyomoyo,"huwenda ziliwekewa matairi na sasa ni daladala". Yani hata meli inapotea! (Yaani meli nzima hailipi kodi na haijulikani iliko tena). Huwenda ziliposhusha mizigo zilizama!
 
Khaaa.... MUNGU amuongoze wajulikane walio husika na washitakiwe na kufungwa vifungo vya maisha wote...
 
Back
Top Bottom