chiefnyumbanitu
JF-Expert Member
- Nov 28, 2015
- 906
- 426
Leo imetimia mwaka mmoja, miezi mitano na siku nne tangu Rais John Magufuli alipokabidhiwa nchi.
Ni kipindi ambacho anapaswa kuanza kufanya mapitio kuelekea kwenye tathmini ya nusu muhula wa Serikali, yaani Government Midterm Review.
Mwaka ujao, kipindi kama hiki kama Mungu atatuweka hai, Rais Magufuli atakuwa anatimiza nusu ya muhula katika uongozi wake wa miaka mitano.
Hivyo basi, wakati huu ni mwafaka Rais Magufuli akawa anaufanyia tathmini uongozi wake, kuelekea kwenye tathmini nzima ya nusu muhula.
MOSI: Aliwakuta wananchi wana hali gani na sasa wapoje? Kama anaona amewafikisha pazuri, hiyo ni heri. Ikiwa amewafikisha penye afadhali kuliko alipowakuta basi azidi kuchapa kazi. Kama aliwakuta wana nafuu na sasa hali ni mbaya basi arekebishe kuelekea nusu muhula.
PILI: Amani, utulivu na usalama. Je, aliwakuta wananchi wakiishi kwa wasiwasi? Wakihofia usalama wao? Watu wakipotea bila taarifa. Watu wakitekwa? Kama alikuta hali ilikuwa mbaya na sasa kapunguza tatizo, basi adumishe ulinzi kwa raia.
Ikiwa hayo mambo hayakuwepo na yameibuka wakati wake, basi atazame upya mfumo wa ulinzi wa raia ambao alikula kiapo cha kuwalinda kupitia Katiba.
TATU: Rais gani kabla yake, alishuhudia msaidizi wake akivamia kituo cha runinga au chombo chochote na habari akiwa na bunduki kisha kulazimisha kurusha kipindi alichotaka huku akitoa vitisho, kisha Rais mwenyewe akamtetea huyo msaidizi wake?
Kama yupo Rais aliyefanya hivyo kabla yake, basi huo ni mfano mbaya ambao hapaswi kuuiga. Ikiwa hayupo Rais aliyefanya hivyo, basi atambue kuwa ametambulisha mfano mbaya kwa kumtetea Makonda aliyevamia Clouds TV.
NNE: Kabla yake, kuna waziri aliwahi kufukuzwa kazi kisha akatishiwa bastola hadharani na mtu anayedaiwa ni ofisa usalama, kitengo cha ulinzi wa viongozi? Kama iliwahi kutokea basi ni kosa ambalo hapaswi kuliiga. Kama hakukuwahi kutokea kitu hicho, basi tukio la Nape kutishiwa bastola linapaswa kushughulikiwa kwa nguvu kubwa ili kusafisha taswira ya uongozi wake.
Haya mambo ya kutoa silaha bila mpango ndiyo yalisababisha Mwangosi auawe na FFU.
TANO: Rais gani kabla yake alipata kuwaambia wamiliki wa vyombo vya habari kuwa hawana Uhuru huo ambao wanadhani wanao? Kama yupo basi ajiepushe na maneno yake. Kama hayupo, basi ajisahihishe kwa sababu vyombo vya habari siyo tu vinatakiwa kuwa huru, bali pia vionekane vipo huru.
Hayo ni kwa uchache. Mengi tu ajitathmini kwayo. Uhusiano wake na wafanyabiashara unaisaidia nchi au unaiangamiza? Utu wa Mtanzania na vitisho vingi vilivyopo. Je, viongozi wanawaheshimu na kunyenyekea wananchi au wanawapeleka kibabe?
Ndimi Luqman MALOTO