Rais Magufuli amteua Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria(OUT)

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI​

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 25 Mei, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mheshimiwa Pinda unaanza mara moja.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano,IKULU Dar es salaam
25 Mei, 2016


index-jpeg.350895
 
Habari wanaJF,

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Joseph Magufuli amemteua Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda waziri mkuu mstaafu wa Tanzania kuwa mkuu wa chuo kikuu huria (Open University Of Tanzania)

Uteuzi huu unafuatia baada ya aliyekuwa mkuu wa chuo hicho Bi. Asha-Rose Mtengeti Migiro kuteuliwa kuwa balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

index.jpeg
 
Hongera sana mkulima Pinda, kifanye chuo kiheshimike maana wahitimu wa OUT wanadharauliwa sana mtaani kana kwamba hawajasoma.
 
Kwanini hakumchagua Mtu toka upande wa pili kama vile Mzee Mtei au Mzee Lowasa au Mzee Mrema na kama hao?
 
Sijawahi kuona umuhimu wa vyeo hivi maana ni ceremonial tu hawana mamlaka yoyote
 
Waziri mkuu mstaafu alishaamua kurudia kazi yake ya ukulima kwanini mh Rais hakumuacha ajilimie zake mapapai yake.
 
Labda ni ile picha ya kwenye MPESA imefanya wamkumbuke.Hongera kwa maamuzi hayo mzee huyu ametumikia nchi kwa uadilifu ndivyo anavyotakiwa kuheshimiwa hivyo.
 
Angemuacha Mzee wa watu na kilimo chake...mimi sioni sababu ya kumrudisha mtu aliyestaafu na anafanya shughuli zake vizuri kama Mzee PINDA kwenye hivi vyeo.

Inachotakikana sasa ni yeye kutupa ushauri elekezi ktk kilimo ili tuwe kama yeye.
 
Back
Top Bottom