Rais Magufuli amteua Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), achukua nafasi ya Dr. Modestus Kipilimba

Status
Not open for further replies.
Rais Magufuli amemteua Kamishna Diwani Athumani Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa(TISS). Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TISS, Dr. Modestus Kipilimba atapangiwa kazi nyingine.


Tokea 2015, Kamishna Diwani Msuya ameshika nyadhifa mbalimbali kwa kasi sana

2015:
Kaimu Kamishna wa Kamisheni ya Intelijensia ya Jinai

Mei 2015: Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)

Novemba 2016: Katibu Tawala Kagera

Septemba 2018: Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU

Septemba 2019: Mkurugenzi Mkuu TISS

----------
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua na kumuapisha Karnishna Diwani Athumani Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Uteuzi wa Kamishna Diwani Athuman Msuya umeanza leo tarehe 12 Septemba, 2019 na ameapishwa leo Ikulu Jijini Dar Es Salaam.

kabla ya uteuzi huo, Kamishna Diwani Athumani Msuya alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Akizunguniza baada ya kumuapisha, Rais Magufuli amerntaka Kamishna Diwani Athuman Msuya kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kwa kuweka nibele masilahi va Taifa.

Kamishna Diwani Athuman Msuya anachukua nafasi va Dkt. Modestus Kipilimba ambaye atapangiwa kazi nyingine

View attachment 1205370

View attachment 1205386

View attachment 1205394
Mkurugenzi Mkuu TISS, Diwani Athuman akiapishwa



DIWANI ATHUMAN MSUYA NI NANI?


Diwani Athuman Msuya katika utumishi wake kwenye Jeshi la Polisi ameshika vyeo na nyadhifa mbalimbali, ikiwemo kuwa msaidizi binafsi (Aide-De-Camp) wa IGP Omary Mahita. (Aide-de-camp ama kwa kifupi ADC au 'bodyguarg' kama wengi mlivyozoea kuwaita).

Mwaka 2008 alipandishwa cheo kutoka Mrakibu wa Polisi (SP) kuwa Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) na baadae kuteuliwa kuwa Mkuu wa upelelezi mkoa wa Mbeya (RCO).

April 28 Mwaka 2010 alipandishwa cheo kutoka Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) kuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kubaki na majukumu yake yaleyale ya Mkuu wa upelelezi mkoa wa Mbeya.

Novemba mwaka 2010 IGP Said Mwema alimpangia majukumu mapya ya kuwa Kamanda wa polisi (RPC) mkoa wa Shinyanga kuchukua nafasi ya ACP Daudi Siasi.

Mei 2012 alihamishwa kutoka Shinyanga kurudi Mbeya kuendelea na majukumu yake kama Kamanda wa polisi (RPC) wa mkoa wa Mbeya.

Novemba 21 mwaka 2013 Rais Jakaya Kikwete alimpandisha cheo kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP).

Alidumu katika cheo hicho kwa wiki mbili tu, na Disemba 06 mwaka huohuo (2013) Rais Kikwete alimpandisha tena kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) na kumteua kuwa Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (Deputy DCI).

Mwaka 2014 alibadilishiwa majukumu kutoka Deputy DCI, kuwa Kaimu Kamishna wa kamisheni ya Intelijensia ya Jinai.

Tarehe 20 Machi 2015, Rais Kikwete aliwapandisha vyeo maafisa watatu (3) wa Jeshi la Polisi kutoka Naibu Kamishina (DCP) kuwa Makamishina kamili (CP). Maafisa hao ni Kenneth Kasseke, Elice Mapunda na Diwani Athuman.

Mei 12 mwaka 2015 Rais Kikwete alimteua Kamishna Diwani Athuman kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuchukua nafasi ya Isaya Mungulu ambaye alistaafu.

Novemba 18 mwaka 2016 Rais Magufuli alitengua uteuzi wake katika nafasi ya DCI na kumteua kuwa Katibu Tawala (RAS) mkoa wa Kagera.

Miaka miwili baadae yani mwaka 2018, Rais Magufuli alimtoa kuwa RAS Kagera na kumteua kuwa Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU kuchukua nafasi ya Valentino Mlowola ambaye aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba.

Septemba 12 mwaka 2018 Diwani Athumani Msuya aliapishwa kuwa Mkurugenzi mkuu TAKUKURU. Na Septemba 12 mwaka 2019 ameapishwa tena kuwa Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), kuchukua nafasi ya Mchungaji Dkt. Modestus Kipilimba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Diwani ana shahada ya uzamili ya Sheria (LLM).

View attachment 1206133

Kipilimba yu wapi kwa sasa?
 
Huu ushauri mkuu atakuwa anapewa na mtu wa"nje"! Sidhani kama watu ndani ya TISS wameshindwa kupendekeza mkurugenzi kutoka ndani ya watu walioko ndani wanaotekeleza majukumu ya kitengo kila siku badala ya kumpa ukurugenzi mtu aliekuwa mtoa taarifa za umbeya tu
Anaweza akawa mtu mrefu wa pale pembeni ya Kigoma
 
Kipilimba yu wapi kwa sasa?
Ni Mchungaji feki, yupo Mbezi anatoa watu mapepo wakati na yeye damu za watu zinamlilia. Kanisa la T.A.G linakumbatia wachungaji wauaji.

Pia hata Bashite huwa anajifanya mlokole.

Maswali ni mengi kuliko majibu!
 
Ni Mchungaji feki, yupo Mbezi anatoa watu mapepo wakati na yeye damu za watu zinamlilia. Kanisa la T.A.G linakumbatia wachungaji wauaji.

Pia hata Bashite huwa anajifanya mlokole.

Maswali ni mengi kuliko majibu!

Mkuu ni vema kuwa na uhakika na unachoandika. Si kweli kabisa hiki ulichoandika hapa kuhusu Kipilimba. Kama unakumbuka Mhe. Rais alimteua kuwa balozi wa Tz nchini Namibia. Na alishaapishwa na kwenda huko. Hiyo Mbezi alipo ni ipi? Halafu kutaja kanisa fulani linakumbatia wauaji, kwani makanisa mengine pia hamna watu wanaofanya kazi nyeti kama aliyokuwa nayo? Ni maoni yangu. Asante.
 
Ni Mchungaji feki, yupo Mbezi anatoa watu mapepo wakati na yeye damu za watu zinamlilia. Kanisa la T.A.G linakumbatia wachungaji wauaji.

Pia hata Bashite huwa anajifanya mlokole.

Maswali ni mengi kuliko majibu!
Tubu dhambi ya kumutia KIPILIMBA ki-dharau na kashfa, damu gani inamlilia wakati usalama wa Taifa ni idara kubwa na yenye vitngo vingi?

Kuna ushahidi kwamba hao wanao uwawa ni usalama wa Taifa wamefanya hivyo?
Na unaposema mchungaji feki, mbona kuna mashehe Wanafanya ugaidi, kubaka na kuzini kinyume na sehemu Mungu aliyoiweka kwa ajili hiyo?

Mbona kuna mapadre huko vatican wamebaka, tena watoto wadogo kwa mamia? Na wamekiri wazi wazi?
Hao nao ni mapadre feki na mashehe feki?
 
Tubu dhambi ya kumutia KIPILIMBA ki-dharau na kashfa, damu gani inamlilia wakati usalama wa Taifa ni idara kubwa na yenye vitngo vingi?
Kuna ushahidi kwamba hao wanao uwawa ni usalama wa Taifa wamefanya hivyo?
Na unaposema mchungaji feki, mbona kuna mashehe Wanafanya ugaidi, kubaka na kuzini kinyume na sehemu Mungu aliyoiweka kwa ajili hiyo?
Mbona kuna mapadre huko vatican wamebaka, tena watoto wadogo kwa mamia? na wamekiri wazi wazi?
Hao nao ni maoadre feki na mashehe feki?
Nani atubu???!! Mimi au muuaji?

Kwa hiyo ni halali mtu aue kwa kuwa na Vatican wanatenda dhambi?

Hivi unajua nafasi ya DG katika kumshauri Rais? Hivyo vitengo vyote vipo chini ya DG mmoja.

Utekaji na uuaji
Ununuzi wa wabunge na madiwani wa upinzani hiyo yote ilikuwa kazi ya vitengo vyake.

Unajua ni wafanyabiashara wangapi wamenyang'anywa pesa na akaunti za kuzuiliwa?


Kama una akili timamu sidhani kama utafurahia haya.
 
Meko haridhishwi na utendaji wa diwani!atampiga chini na kuteua yule wa cyber security tpdf kuwa mkurugenzi mpya!!!Haya nimewafungulia codes njooni mchangie uzi!!
Sidhani, ounce tetesi zikisha sambaa kuna kanuni ya kupotezea, kwa maana watatafuta muda mwingine na watu wengine,ila sijui protocols za utawala wa Magufuli .
Pili Huyo Boss wa TISS mbona ni kama ana Mosad signature?Hivi hivi wamteme?Mbona kama ni full masinondo? Au fitina?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom