Rais Magufuli amteua Kamishna Diwani Athuman Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), achukua nafasi ya Dr. Modestus Kipilimba

Status
Not open for further replies.

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,074
4,098
Rais Magufuli amemteua Kamishna Diwani Athumani Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa(TISS). Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TISS, Dr. Modestus Kipilimba atapangiwa kazi nyingine.

Diwani.PNG

Tokea 2015, Kamishna Diwani Msuya ameshika nyadhifa mbalimbali kwa kasi sana

2015:
Kaimu Kamishna wa Kamisheni ya Intelijensia ya Jinai

Mei 2015: Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)

Novemba 2016: Katibu Tawala Kagera

Septemba 2018: Mkurugenzi Mkuu TAKUKURU

Septemba 2019: Mkurugenzi Mkuu TISS

----------
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua na kumuapisha Karnishna Diwani Athumani Msuya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Uteuzi wa Kamishna Diwani Athuman Msuya umeanza leo tarehe 12 Septemba, 2019 na ameapishwa leo Ikulu Jijini Dar Es Salaam.

kabla ya uteuzi huo, Kamishna Diwani Athumani Msuya alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Akizunguniza baada ya kumuapisha, Rais Magufuli amerntaka Kamishna Diwani Athuman Msuya kuchapa kazi kwa juhudi na maarifa na kwa kuweka nibele masilahi va Taifa.

Kamishna Diwani Athuman Msuya anachukua nafasi va Dkt. Modestus Kipilimba ambaye atapangiwa kazi nyingine

TISS.PNG


JF.PNG


EEQiiJ-XkAAsmXc.jpg

Mkurugenzi Mkuu TISS, Diwani Athuman akiapishwa



DIWANI ATHUMAN MSUYA NI NANI?


Diwani Athuman Msuya katika utumishi wake kwenye Jeshi la Polisi ameshika vyeo na nyadhifa mbalimbali, ikiwemo kuwa msaidizi binafsi (Aide-De-Camp) wa IGP Omary Mahita. (Aide-de-camp ama kwa kifupi ADC au 'bodyguarg' kama wengi mlivyozoea kuwaita).

Mwaka 2008 alipandishwa cheo kutoka Mrakibu wa Polisi (SP) kuwa Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) na baadae kuteuliwa kuwa Mkuu wa upelelezi mkoa wa Mbeya (RCO).

April 28 Mwaka 2010 alipandishwa cheo kutoka Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) kuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kubaki na majukumu yake yaleyale ya Mkuu wa upelelezi mkoa wa Mbeya.

Novemba mwaka 2010 IGP Said Mwema alimpangia majukumu mapya ya kuwa Kamanda wa polisi (RPC) mkoa wa Shinyanga kuchukua nafasi ya ACP Daudi Siasi.

Mei 2012 alihamishwa kutoka Shinyanga kurudi Mbeya kuendelea na majukumu yake kama Kamanda wa polisi (RPC) wa mkoa wa Mbeya.

Novemba 21 mwaka 2013 Rais Jakaya Kikwete alimpandisha cheo kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) kutoka Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP).

Alidumu katika cheo hicho kwa wiki mbili tu, na Disemba 06 mwaka huohuo (2013) Rais Kikwete alimpandisha tena kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) na kumteua kuwa Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (Deputy DCI).

Mwaka 2014 alibadilishiwa majukumu kutoka Deputy DCI, kuwa Kaimu Kamishna wa kamisheni ya Intelijensia ya Jinai.

Tarehe 20 Machi 2015, Rais Kikwete aliwapandisha vyeo maafisa watatu (3) wa Jeshi la Polisi kutoka Naibu Kamishina (DCP) kuwa Makamishina kamili (CP). Maafisa hao ni Kenneth Kasseke, Elice Mapunda na Diwani Athuman.

Mei 12 mwaka 2015 Rais Kikwete alimteua Kamishna Diwani Athuman kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) kuchukua nafasi ya Isaya Mungulu ambaye alistaafu.

Novemba 18 mwaka 2016 Rais Magufuli alitengua uteuzi wake katika nafasi ya DCI na kumteua kuwa Katibu Tawala (RAS) mkoa wa Kagera.

Miaka miwili baadae yani mwaka 2018, Rais Magufuli alimtoa kuwa RAS Kagera na kumteua kuwa Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU kuchukua nafasi ya Valentino Mlowola ambaye aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba.

Septemba 12 mwaka 2018 Diwani Athumani Msuya aliapishwa kuwa Mkurugenzi mkuu TAKUKURU. Na Septemba 12 mwaka 2019 ameapishwa tena kuwa Mkurugenzi mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), kuchukua nafasi ya Mchungaji Dkt. Modestus Kipilimba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Diwani ana shahada ya uzamili ya Sheria (LLM).

93E954A1-821A-4C77-9130-F206F1F1B73E.jpeg
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom