Rais Magufuli amteua Dr. Kyaruzi kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi TANESCO

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzanoa Dr. John Pombe Joseph Magufuli leo tarehe 31.05.2016 amemteuwa Dr Alex L. Kyaruzi kuwa mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la umeme Tanzania (TANESCO).

Kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Nishati Prof Sospeter Muhongo amewateua wafuatao kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuanzia tarehe 31.05.2016 hadi tarehe 30.05.2019

1. Dkt. Samwel Nyantahe
2. Dkt. Lugano Wilson
3. David Elias Alal
4. Mhandisi Stephen Peter Mabada
5. Mhandisi Leonard R. Masanja

Aidha, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amekamilisha uteuzi wa Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Madini la Taifa (STAMICO). Kuanzia tarehe 31.05.2016 hadi tarehe 29.05.2019

Abdalah H. Musa
Dkt. Coretha Komba
Felix M. Maagi
Dkt. Lightness Mnzava
John B. Seka

Aidha imeelezwa kuwa uzinduzi wa bodi hizi utafanyika makao makuu ya mashirika haya tarehe 02.06.2016 siku ya Alhamis saa 4:00 asubui kwa STAMICO na Saa 8:00 Mchana kwa Tanesco.

9ce70598-be14-45c4-8877-de2cedfce439.jpg
 
Teuzi hazijakwisha tu muanze kuwatumikia wananchi??


Ooh ghashh!!
 
Magufuli is an equal opportunity employer. Atakuwa anaangalia uzoefu wa mtendaji na sio imani yake, japo in some cases
'gender balance' ni muhimu pia'
 
Ashiakamoo Dk kilala kheri nimependa zile bodizilizopita zimejazana mashemeji mananii hizi za vichwatupu
 
Dr kyaruzi hatimae ameingia tanesco kama mwenyekiti wa bodi, Walimbania ukurugenzi kipindi ngereja ni waziri
 
Back
Top Bottom