Rais Magufuli amteua Bi. Salma Kikwete kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

JamiiForums

JF Official Account
Nov 9, 2006
6,227
5,270
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ikulu, Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 01 Machi, 2017 amemteua Mhe. Salma Kikwete kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Mhe. Salma Kikwete ni Mke wa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Mhe. Salma Kikwete ataapishwa kwa mujibu wa sheria na taratibu zitakazotangazwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,IKULU
01 Machi, 2017

Dar es Salaam

IMG_3758.JPG


Masahihisho toka Ikulu:

Mama Salma Kikwete ameteuliwa kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na SIO Mbunge wa Viti Maalum kama ilivyoandikwa awali.
 
Bunge limeiva...

Mama na mwana ndani ya nyumba...

Huyu naye atakuwa anaandaliwa wizara ... naota tu.

CCM ni ile ile... wamejipanga!!!

Kama lengo ni kusimamisha mjadala wa fojari za Bashite basi nawavulia kofia. Taifa sasa litahamia kujadili uteuzi wa mke wa mstaafu na kusahau mjadala wa kufoji vyeti uliofanywa na [HASHTAG]#munguwadar[/HASHTAG] mwenye asili ya Koromije.

Ila kutoka kwenye umama wa kwanza ulioandamana na ulinzi uliotukuka na escort ya heshima, hadi kuwa mbunge wa kawaida kuja kutukanana na kina Sugu, sidhani kama ni inalipa. Mama hakuwa na cha kupoteza... angeendelea kukaa karibu na mzee wetu ahakikishe anapata anachohitaji baada ya kazi ngumu ya urais kwa miaka 10.
 
Back
Top Bottom