Rais Magufuli amsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya RAHCO

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,720
55,852
Rais Dkt.Magufuli amsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa Kampuni miliki ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Mhandisi Benhadard Tito na kuvunja bodi hiyo.
attachment.php

Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli(RAHCO), Mhandisi Benhadard Tito akifafanua Jambo.

=============================
==

Rais wa Jamhuri ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO) Mhandisi Benhadard Tito ili kupisha uchunguzi wa kina kufuatia ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi uliobainika katika mchakato wa utoaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati.

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema, Rais Magufuli amefikia uamuzi huo baada ya kuitisha kikao cha wataalamu kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za serikali ambazo zinahusika katika utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani "Standard Gauge"

Amesema pamoja na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO, Rais Magufuli ameivunja bodi ya RAHCO baada ya kujiridhisha kuwa haikutekeleza ipasavyo wajibu wake katika kusimamia mchakato wa zabuni hiyo na badala yake imeonekana kutetea kilichofanyika

Aidha Rais Magufuli amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO Mhandisi Benhadard Tito kutoa ushirikiano kwa vyombo vya serikali vitakavyofanya uchunguzi zaidi kuhusu mchakato wa Zabuni hiyo.

Pia ameiagiza Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya kampuni za ukandarasi zilizopewa zabuni ya ujenzi huo endapo itathibitika kuwa zimeshiriki katika ukiukwaji wa sheria.

Katika hatua nyingine Balozi Sefue amesema, Rais Magufuli amevunja bodi ya Mamlaka ya Reli Tanzania (TRL) kutokana na kutoridhishwa na jinsi bodi hiyo ilivyoshughulikia ripoti ya uchunguzi wa mchakato wa ununuzi wa mabehewa ya treni.

Gerson Msigwa

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU

22 Desemba, 2015
 

Attachments

  • DSC_0792.JPG
    DSC_0792.JPG
    21.3 KB · Views: 21,166
Kwa kirefu jamni!

Hata maelezo ya ziada kuhusu mtu huyo, kashifa yake na particulars za kampuni husika
 
Majipu yapo mengi sana ngoja tumpe muda rais wetu wa kuweka mambo sawa
 
Mkuu mbona post zako huwa zinakuwa zimeshiba Leo umekuwaje?, umekuwa kama junior member
 
Jpm kazi anayo kwani kila anapogusa majipu tupu inavyoelekea haya majipu yameshamaliza mwili mzima.
 
Nimepokea message hii

#Habari:Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi mkurugenzi mkuu wa kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania RAHCO Mhandisi Benhadard Tito #(Pichani) kufuatia ukiukwaji mkubwa wa taratibu za utoaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati sambamba na na kuivunja bodi ya RAHCO.
 
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telegrams : "CABINET"DAR ES SALAAM
Telephone : 2116898, 2116900/6
E-mail : chief@ikulu.go.tz
E-mail : ikulu@ikulu.go.tz
Fax : 2113425/2116914/2117272


PRESIDENT?S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD
11400 DAR ES SALAAM.


Rais wa Jamhuri ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO) Mhandisi Benhadard Tito ili kupisha uchunguzi wa kina kufuatia ukiukwaji mkubwa wa taratibu za manunuzi uliobainika katika mchakato wa utoaji wa zabuni ya ujenzi wa reli ya kati.Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesema, Rais Magufuli amefikia uamuzi huo baada ya kuitisha kikao cha wataalamu kutoka Wizara na Taasisi mbalimbali za serikali ambazo zinahusika katika utekelezaji wa Mradi wa Ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani "Standard Gauge"Amesema pamoja na kumsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO, Rais Magufuli ameivunja bodi ya RAHCO baada ya kujiridhisha kuwa haikutekeleza ipasavyo wajibu wake katika kusimamia mchakato wa zabuni hiyo na badala yake imeonekana kutetea kilichofanyikaAidha Rais Magufuli amemtaka Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO Mhandisi Benhadard Tito kutoa ushirikiano kwa vyombo vya serikali vitakavyofanya uchunguzi zaidi kuhusu mchakato wa Zabuni hiyo.Pia ameiagiza Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya kampuni za ukandarasi zilizopewa zabuni ya ujenzi huo endapo itathibitika kuwa zimeshiriki katika ukiukwaji wa sheria.Katika hatua nyingine Balozi Sefue amesema, Rais Magufuli amevunja bodi ya Mamlaka ya Reli Tanzania (TRL) kutokana na kutoridhishwa na jinsi bodi hiyo ilivyoshughulikia ripoti ya uchunguzi wa mchakato wa ununuzi wa mabehewa ya treni.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
22 Desemba, 2015
 
Mimi naomba kufahimishwa majukumu ya hiyo taasisi/kampuni/shirika/mradi inayoitwa RAHCO ktk reli za Tanzania.
 
Back
Top Bottom