AUGUSTINO CHIWINGA
JF-Expert Member
- Apr 23, 2017
- 222
- 695
Na.
Augustino Chiwinga.
Siku moja mwanafalsafa Socrates aliwasha taa mchana kweupe na akaenda nayo kwenye soko la Athens, kule Ugiriki. Pale sokoni wananchi wengi walimshangaa sana Socrates wakamuuliza; kwa nini amewasha taa sokoni wakati ni mchana na mwanga wa taa yake wala hauonekani kutokana na mwanga wa jua uliopo.
Socrates aliwajibu hivi, ‘’Pamoja na nuru hii ya jua lakini akili za watu wengi ziko kwenye giza nene’’.
Mfano huu naufananisha na jinsi ambavyo mamilioni ya watanzania tulikua gizani kifikra. Tulikua huru lakini sio huru kifikra.
Nchi za ulaya na Marekani ambazo tunaziita nchi zilizoendelea(Developed countries) zilipata maendeleo mara baada baada ya kupata viongozi waliowaletea uhuru wa ukombozi wa fikra wananchi wao.
Pamoja na mageuzi makubwa waliyoyafanya kama vile ya kiuchumi kijamii na kisiasa na kadhalika , lakini pia walifanya mageuzi makubwa ya kifikra kwa wananchi wao.
Mageuzi hayo ya makubwa ya kifikra walijitahidi kuyasema na kuyasisitiza kila siku mpaka wananchi wakaelewa wakayageuza kuwa ni mila desturi na tabia zao za kila siku.
Tangu serikali ya awamu ya 5 iingie madarakani nayo imefanya mageuzi mengi makubwa ya kifkra kwa watanzania.
Mageuzi ya fikra juu ya uwajibikaji, uadilifu , uchapakazi,uaminifu na uzalendo.
Fikra hasi ambazo jamii ya kitanzania tulikua nazo kwa miaka mingi sasa tumeachana nazo.
Rais Magufuli ametupa uwanda wa fikra mpya kwamba ili mtu apate pesa basi ni lazima afanye kazi halali.
Njia za kupata pesa kijanja kwa dili haramu zote zimedhibitiwa madhubuti na wake waliosambazwa sehemu mbalimbali.
Hivyo basi kila raia anao wajibu wa kufanya kazi kwa bidii mahali alipo na asitegemee kupata pesa bila ya kufanya kazi.
Rais Magufuli pia ametufunza kufikiri tofauti kwamba Tanzania bila mdudu rushwa inawezekana . Kwa miaka mingi tatizo la rushwa lilikua limeota mizizi hapa Tanzania , wananchi walikua wanauziwa haki zao kama njugu.Lakini siku hizi wananchi wanafikiri tofauti wanauelewa mpana na wameacha kununua haki zao na tumeshuhudia wananchi wengi wakiripoti TAKUKURU kwa wingi kabisa tofauti na kipindi cha nyuma.
Zamani tulikua tuna fikra kwamba ili mtu afanikiwe kimaisha basi ni lazima afanye dili haramu lakini sasa hivi tunafikra za tofauti nazo ni kwamba ili mtu afanikiwe kimaisha basi ni lazima afanye kazi halali na apate kipato halali .Kinyume na hapo atakachokutana nacho ataenda kukisimulia katika kuta za jela ya Ukonga.
Tunahitaji viongozi aina ya Magufuli ambao wanabadilisha "mindset " zetu katika zama hizi za utandawazi na changamoto za kidunia.
Hakuna ukombozi mkubwa duniani kama ukombozi wa fikra.
Watanzania tulihitaji ukombozi wa kifikra tulikwama katika mengi, tulidumaa katika mengi.
George Benard Shaw alipata kuandika haya; “Maendeleo hayawezekani bila mabadiliko ya fikra na wale ambao hawawezi kubadilika namna wanavyofikiri hawawezi kubadili chochote”. Falsafa itatusaidia kuwa na maarifa yatakayotusaidia kufanya uamuzi sahihi kwa kufahamu lipi lifanyike na kwa namna gani, na kwa wakati gani, na lipi tuliache, na kwa nini tuliache.
Mh.Rais Magufuli anataka kujenga kizazi chenye uwezo wa kufikiri kwa upana “Reasoning generation”. Anataka kujenga kizazi cha kuwajibika na si kizazi cha kulalamika. Anataka kujenga kizazi chenye uwezo wa kuwakosoa viongozi wavivu, wala rushwa wazembe ,viongozi wabadhirifu ,viongozi wasio na maono kwa Taifa letu, viongozi wasio na uzalendo na Taifa lao.
Mwanasayansi Albert Einstein alipata kushauri hivi, “Ukifikiri mwaka mmoja ujao panda mbegu. Ukifikiri miaka 10 ijayo panda mti. Ukifikiri miaka 100 ijayo elimisha watu”.
Mwanasayansi huyu alikuwa na maana hii, kwa kupanda mbegu utavuna mara moja. Kwa kupanda mti utavuna mara kumi. Kwa kuelimisha watu utajenga kizazi kinachojitambua.
Watanzania kwa pamoja tufanye kazi ya kulijenga Taifa letu. Tanzania itajengwa na Watanzania. Tanzania yenye heri na neema itajengwa na Watanzania. Tanzania yenye amani, umoja na undugu itajengwa na Watanzania.
Ni kweli bado mbele yake Rais Magufulu ana kazi tena ngumu ya kulijenga Taifa letu. Huu ni wakati wa kuyatafsiri maisha kama kipindi cha mpito cha kufanya kazi, kujituma na kusonga mbele. Tusiogope. Tusonge mbele. Sisi ni Tanzania mpya sisi no kizazi cha matokeo chanya.
Wasalaam,
Augustino Chiwinga.
Nyangao-Lindi
0756 810804