Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,160
Serikali yoyote duniani inaweza kuitwa ina utawala bora, iwapo tu itazingatia utawala wa sheria, kama unavyoitwa kwa kiingereza "power seperation" ambao unaheshimu mgawanyo wa madaraka kati ya mihimili 3 mikuu, ambayo ni serikali, Bunge na Mahakama, katika kile kinachoitwa "check and balance"
Hapa nchini kwetu, kama ambavyo aliwahi nukuliwa mkuu wetu wa nchi, akitamba kuwa mhimili wa serikali ndiyo "superior" kwa wenyewe kujichimbia chini zaidi na hivyo kuwa juu ya mihimili hiyo mingine!
Hilo limethibitika baada ya Rais Magufuli kumteua kada na CCM, Dr Wilson Mahera, kuwa ndiyo Mkurugenzi mpya wa uchaguzi hapa nchini, kitendo ambacho ni uvunjaji wa waziwazi wa Katiba yetu ya nchi, kwani analazimika kuteua mkurugenzi wa uchaguzi ambaye siyo kada wa chama chake
Hivi kitendo hicho cha Rais tunaweza kukielezaje, kama siyo kuudharau mhimili wa mahakama??
Sote tunakumbuka uamuzi wa hivi karibuni wa mahakama kuu, wa kusema kuwa wakurugenzi wa wilaya hawawezi tena kuwa wasimamizi wa uchaguzi zinazohusisha uchaguzi za vyama vingi hapa nchini baada ya mahakama hiyo kujiridhisha kuwa wapo wakurugenzi ambao pia ni makada wa CCM zaidi ya 74 hapa nchini ambao wamepewa madaraka hayo ya kusimamia chaguzi hizo
Ingawa tunajua kuwa serikali imekata rufaa kupinga uamuzi huo, kwa kuwa rufaa hiyo haijaanza kusikilizwa , kwa hiyo kwa sasa inafahamika wazi kuwa maDED, HAWAPASWI kusimamia chaguzi za aina yoyote hapa nchini
Hivi kitendo cha Rais wetu kumteua kada huyo wa CCM, siyo kitendo cha kuidharau mhimili huo wa mahakama kwa maamuzi iliyoyafanya??
Hivi kitendo hicho kina tofauti gani na mathalani mechi ya mpira wa miguu ya watani wa jadi ya Yanga na Simba, kubaini kuwa mwanachama wa kindakindaki wa moja ya klabu hiyo ndiye aiyeteuliwa kuwa "refa" wa mechi hiyo??
Ni dhahiri kuwa timu pinzani itagomea kucheza mechi hiyo kwa kuamini kuwa "refa" aliyeteuliwa kusimamia mechi hiyo, hatotenda haki kwa upande wao
Uthibitosho mwingine wa Rais wetu kuingilia mihimili mwingine ni hivi karibuni kunukuliwa akimweleza Spika wa Bunge letu kuwa amefanya vyema kumtimua aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, ambaye dunia nzima inajua kuwa yupo nje ya nchi kwa matibabu, kutokana na "watu wasiojulikana" kumminia risasi nyingi kwa lengo la kumuua, lakini kwa kudra ya Mwenyezi Mungu, alimnusuru kimiujiza na akanusurika kuuawa na hadi hivi sasa anaendelea kupata matibabu nje ya nchi
Hivi Rais Magufuli anawezaje kumwita Tundu Lissu kuwa amelitelekeza jimbo hilo wakati dunia nzima inafahamu kuwa Tundu Lissu yupo nje ya nchi akijitibu??
Hayo ni matukio mawili kati ya mengi sana, ambayo nchi yetu chini ya utawala huu wa serikali ya awamu ya tano unavyojaribu kwa kila njia ili kuua upinzani,ambao umedumu hapa nchini kwa zaidi ya miaka 25 hivi sasa
Kama nchi ni lazima tuheshimu kwa nguvu zote misingi ya kulinda demokrasia yetu na tufahamu pia kitendo cha kuvuruga zoezi la uchaguzi, ni kitendo kitakachohatarisha amani ya nchi yetu, ambayo ndiyo lulu pekee ambayo nchi yetu inajivunia nayo