VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Ni kuhusu kuweka wigo wa kusema, kutenda na kuwajibika kwa viongozi wao. Rais Magufuli amefika pale pale pa Rais Mstaafu Kikwete pa kuweka cha kusemwa, kutendwa na kuwajibika nacho. Kikwete aliweka wigo huo wakati wa Bunge la Katiba. Kikwete, akiwa Rais wa Tanzania, aliuweka Urais pembeni na kuuvaa vilivyo uenyekiti wa chama-CCM.
Kwenye hotuba yake ya kufungua Bunge la Katiba, Kikwete aliweka wazi na imara msimamo wa CCM juu ya Rasimu ya pili ya Tume ya Jaji Warioba. Hapo ndipo mambo yalipoanza kuharibika. Kila mjumbe wa Bunge la Katiba aliyehusiana na CCM, alikuwa akirudia tu yaliyosemwa na Kikwete. Msimamo wa chama. Wigo.
Baada ya kuchaguliwa na kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania, Rais Magufuli alionesha 'demo' ya atakavyo kwenye utawala wake. Akaonesha mifano ya kuteua, kutengua, kufukuza, ziara za kushtukiza na kutobadilisha maamuzi yake. Wigo. Kwasasa, yanashuhudiwa yale yale ayatakayo Rais Magufuli.
Kiongozi wa kuteuliwa, hasa Mawaziri,Manaibu Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na wengineo, wameshaona kuwa kufanya ziara za kushtukiza, kutengua, kufukuza na kutobadili maamuzi ni utendaji utakiwao na Rais Magufuli. Wigo. Wanajitahidi, kadiri wawezavyo, 'kuperform' kwenye mtazamo huo. Wigo.
Ama kweli viatu vya Rais Mstaafu Kikwete vimemtosha Rais Magufuli!
Mzee Tupatupa wa Lumumba, Dar es Salaam