Rais Magufuli alipaswa awe Addis Ababa, Ethiopia leo!

''..Baadhi ya Maraisi wa nchi za Kiafrika wanakutana mjini Addia ababa nchini Ethiopia..''

Sijui kwa nini ulianza hivi, hii inafanya kusiwe na hoja ya kujadili kutokuhudhuria kwa JPM....

''..Baadhi ya Maraisi wa nchi za Kiafrika HAWATAKUWEPO mjini Addia ababa nchini EthiopIa..''
 
Baadhi ya Maraisi wa nchi za Kiafrika wanakutana mjini Addia ababa nchini Ethiopia kwenye Mkutano mkuu wa Umoja wa nchi za Afrika, mpaka leo hii Magufuli wetu hajaingia Ethiopia na wala hakuna dalili kama atatia timu!

HAPA KAZI TU!

Aende wapi na jipu lake limewiva na linatoa harufu mbaya ! Kumbe humtakii mema Magufuli unataka hilo jipu likampasukie huko huko limtie aibu mbele za marais wa Africa!
 
Lazima kuna tatizo mahala flani...ni kweli Mkwere alizidisha kwenda nje, lakini zipo safari za msingi ambazo Rais anapaswa kwenda...wala sio sifa kujifungia magogoni tu na kuifungia TBC kuonesha bunge ...live,

anyway, ngoja tuwasubiri Mafisi wa Lumumba, huenda wakaja na sababu zilizosababisha Mapadlock asiende. Ethiopia...
 
WAKUU wa Nchi za Afrika wanatarajiwa kukutana katika mkutano wa kawaida wa kila mwaka mwishoni mwa mwezi huu jijini Addis Ababa, Ethiopia. Mkutano huu ni sehemu muhimu ya uwepo wa Umoja wa Afrika (AU). Wakati viongozi wa awali wa bara hili walipofikiria namna ya kuileta Afrika pamoja, mojawapo ya mambo ilikuwa ni kuwa na chombo kitakachowakutanisha viongozi wa nchi zote ili kujadili mambo ya msingi yanayohusu bara hili.

Tanzania ilikuwa ni mojawapo ya nchi waasisi wa AU wakati ilipoanzishwa kama Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) mnamo mwaka 1963.
Tanzania ni mojawapo ya nchi muhimu kwenye AU. Imewahi kuwa Mwenyekiti wa OAU na AU. Imewahi kuwa Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi ya Nchi za Kusini mwa Afrika. Mwanadiplomasia wa Tanzania, Dk. Salim Ahmed Salim, ndiye mtu aliyewahi kuwa Katibu Mkuu (Mtendaji Mkuu) wa OAU kwa muda mrefu kuliko mtu (raia) mwingine wa nchi yoyote barani Afrika ! Hii haikuwa bahati mbaya. Ilitokana na mchango wetu mkubwa kwenye uanzishwaji wa AU na pia namna wenzetu wanavyotuheshimu na kutuona wa maana.

Ni imani yangu kuwa Rais John Pombe Magufuli atafanya ziara yake ya kwanza ughaibuni wakati wa Mkutano huo wa Addis. Hii ni kwa sababu, nchi yetu inahitaji aende huko. Kuna dhana inajengeka sasa kwamba kusafiri nje ya nchi kwa viongozi wetu ni dhambi. Nakubali kwamba kuna matatizo kwenye utaratibu wa safari za viongozi ambao unatakiwa kuangaliwa upya lakini sikubali kwamba safari za nje ni mbaya.

Kuna suala la umuhimu wa mikutano husika, idadi ya wanaotakiwa kwenda, kiwango cha malipo kinacholipwa na suala zima la gharama nyingine. Haya ni mambo ya kuangaliwa lakini si kusema kwamba safari ni mbaya. Mkutano wa Viongozi wa AU ni muhimu kutokana na historia yetu kwenye umoja huo. Kama Magufuli atakwenda Addis, hiyo itakuwa ni fursa kwake ya kukutana na wenzake na kufahamiana nao.
Hii ni fursa ambayo Magufuli anaihitaji. Kwa sababu ya historia yake ya nyuma na ukweli kwamba hana mizizi kwenye dunia ya kidiplomasia, mikutano ya namna hii inampa fursa adhimu ya kujiongeza hapa na pale.

Inafahamika kwamba kwenye mkutano kama huu wa mwezi Januari, viongozi wa AU hutumia nafasi hiyo kumtambulisha kiongozi mpya na kwa kawaida hupewa nafasi ya walau kuwahutubia wenzake. Hii ni nafasi ambayo Magufuli anaihitaji. Kwenye mkutano kama huo wa Addis, Magufuli anaweza kukaa kwa siku mbili tu. Na wala hahitaji kwenda na msafara mkubwa. Ipo ndege ya Rais ambayo ilinunuliwa na serikali kwa sababu ya majukumu ya namna hii.

Ni kweli kwamba Magufuli anahitajika zaidi hapa kwetu. Lakini, sisi ni Tanzania. Sisi si mojawapo ya nchi ndogo barani Afrika ambazo hazina historia yoyote kwenye ukombozi wa bara letu. Mwenyekiti wa AU, Robert Mugabe, ataangalia ilipo Tanzania na kutazama kama Magufuli amekuja. Jacob Zuma wa Afrika Kusini atafanya hivyo pia. Wawakilishi kutoka Sahara Magharibi, Comorro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Msumbiji nao watatazama.

Magufuli kuhudhuria mkutano wa AU, hakutaongeza mishahara kwa wafanyakazi wa Tanzania, hakutaboresha elimu yetu, hakutaondoa maradhi na hakutaongeza ajira kwa vijana. Lakini, bado ni mkutano muhimu kwetu kuhudhuria. Ni muhimu kwa Rais wetu kujitambulisha kwa wenzake wote kwa wakati mmoja. Kuzungumza nao na kutoa mwelekeo wa wapi Tanzania inataka kwenda na inatarajia nini kutoka kwa wenzake barani Afrika.

Kuna mambo au maamuzi ambayo nchi inatakiwa kusimamia hata kama hayaonekani kuwa na faida yoyote. Uhusiano wetu na Israel kwa mfano, tungetaka, tungeendelea nao lakini tukabaki na Wapalestina kwa sababu ya msimamo wetu. Tanzania inasimamia misingi ya Umajumui wa Afrika. AU ndicho chombo pekee kikubwa ambacho walau kinasimamia ndoto hiyo hata kama kwa mapungufu mengi. Pasipo AU, ndoto ya siku moja kuwa na Afrika iliyoungana itakuwa imekufa kabisa.

Taifa au mwanadamu asiye na ndoto ni sawa na kitu mfu. Utaifa ni ndoto. Kwamba watu hawa wa nchi moja wameamua kuwa pamoja ili kutimiza malengo fulanifulani. Kwetu sisi Watanzania, ndoto ya kuwa na Afrika moja imara na yenye maendeleo ni ya kudumu.
Ndiyo maana, naamini kuwa, Rais Magufuli atahudhuria mkutano huu wa Addis. Atahudhuria kwa sababu Watanzania walimchagua ili kusimamia kile ambacho sisi kama taifa tumeamua kusimamia.

Nafahamu mazingira ambayo serikali ya Magufuli na nchi yetu inapita kwa sasa. Wakati mwingine ni mazingira ambayo si rafiki sana kwa mambo yanayohitaji kufanywa kwa kuzingatia tafakuri na lojiki. Lakini, itakuwa siku mbaya katika historia ya nchi yetu endapo Rais John Pombe Magufuli atakacha kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika mwishoni mwa mwezi huu.

Source: Raia Mwema
 
Lazima kuna tatizo mahala flani...ni kweli Mkwere alizidisha kwenda nje, lakini zipo safari za msingi ambazo Rais anapaswa kwenda...wala sio sifa kujifungia magogoni tu na kuifungia TBC kuonesha bunge ...live,

anyway, ngoja tuwasubiri Mafisi wa Lumumba, huenda wakaja na sababu zilizosababisha Mapadlock asiende. Ethiopia...
Nimeambiwa rais wetu hana passport....
 
Mkuu kuwa na heshima na raisi wetu tabia ya kumwita ma padlock uache leo

Sawa kabisa...tusimdhalilishe Rais kiasi hicho...Rais ni alama ya taifa letu...ndiyo kichwa...nyie mbunge wenu wa UKAWA akiitwa Hole mtafurahi??? Tusifike huko, tuwe na heshima kwa Rais na hata viongozi wengine...
 
mnataka aende wapi wakati anatumbua majipu. fisadis hawapumui wala hawaepi kisu cha kutumbuliwa.
 
Itakuwa bado anasubiri kibali cha Ombeni Sefue. Akiruhusiwa atasafiri tu ..
 
Back
Top Bottom