Rais Magufuli akutana na viongozi wote wakuu wa CCM

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
Pamoja na mambo mengine Rais Magufuli amesema anasikia sikia kuna watu wanalalamika lalamika eti tunawanyanyasa wakati tunawatumbua. Wengine wanasema eti haki za binadamu hazifuatwi wakati wa kuwatumbua utadhani wakati wao wakati wanawaibia wananchi masikini hawakufahamu kama kuna haki za binadamu zinazowazuia kuwaibia wananchi.

Rais Magufuli amesema, wakati tunawateua walifurahi kutajwa hadharani lakini tukiwatumbua hadharani wanalalamika kutajwa hadharani.

''Kwa hiyo haki za binadamu tu kwa hawa waliowaibia wananchi lakini hakuna haki za binadamu kwa wananchi masikini walioibiwa?'' Alisema

''Waliwaibia Watanzania hadharani, lazima tuwatangaze hadharani'' alisema.

Aliendelea kusema, ''mateso waliyoyapata Watanzania wengi masikini kwa sababu ya kuibiwa na wachache lazima na hawa wachache wayapate mateso waliyoyasababisha kwa wananchi''.

''Eti wanasema apewe muda wa kujieleze, kwani yeye aliwapa wananchi muda wa kujieleza wakati hajawaibia?'' Rais alisema

''Kwa hiyo unaweza kuona hata hawa wanaowatetea wezi na wabadhilifu wa mali za umma ni majipu na tutaanza kuwafuatilia ili pia tuwatumbue'' alisema.

VIDEO:



51.JPG

Rais Magufuli na Mkewe wakiwa meza kuu pamoja na viongozi wakuu wa CCM Taifa.
50.JPG

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia Wenyeviti, Makatibu wa Chama cha Mapinduzi wa mikoa na Wilaya za Tanzania bara na Visiwani Ikulu jijini Dar es Salaam



Baadhi ya Wenyeviti wa CCM wa Mikoa mbalimbali wakipiga makofi kumshangilia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati akitoa hotuba yake Ikulu jijini Dar es Salaam.
29.JPG

Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akitoa maneno mawili matatu
35.JPG

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisikiliza kwa makini taarifa zilizokuwa zikitolewa na baadhi ya Wenyeviti na Makatibu wa CCM kutoka mikoa mbalimbali nchini. Kulia kwake ni makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti CCM Taifa Philip Mangula na Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli.
46.JPG

Baadhi ya Viongozi wa CCM wakinyoosha vidole kutaka kutoa maoni yao kwa Rais Magufuli.
55.JPG

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Mohamed Sinani Ikulu jijini Dar es Salaam
59.JPG

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM kutoka mikoa mbalimbali nchini mara baada ya kumaliza kuzungumza nao Ikulu jijini Dar es Salaam
================================================
 
Jamani sukari imepanda bei kilo moja tsh 2600 tumekimbia beer tuwe walevi wa chai nako shidaaa duu namba hiyooooo tunaisoma..
 
Wale ambao alisema wakati wa kampeni kwamba mchana wapo CCM, usiku UKAWA, kwanini wengine walikuwepo kwenye ukumbi? Au kile kiungulia chake (Wasaliti) alichosema kimemkaba pale Lumumba baada ya kutoka Uwanja wa Taifa kuapishwa - kimeshapata tiba ya asili?
 
Back
Top Bottom