Rais Magufuli akutana na Viongozi wa TUCTA!

Rais Dkt. John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) na kuwahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Tano itaendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano kati yake na wafanyakazi




4.JPG

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Trade Union Congress of Tanzania -TUCTA) Ikulu jijini Dar es Salaam.

Katika Mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, Mheshimiwa Rais Magufuli amesema pamoja na kuimarisha ushirikiano huo, Serikali ipo tayari kupokea maoni na ushauri wowote utakaotolewa na vyama vya wafanyakazi wenye lengo la kuboresha maslahi ya wafanyakazi na kuongeza tija kazini.

Mhe. Rais Magufuli amesema Serikali inatambua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi na itaendelea kuchukua hatua za kukabiliana nazo kama ambavyo imeanza kufanya hivyo.

“Nataka kuwahakikishia nyinyi viongozi wa TUCTA na wafanyakazi wote kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inawapenda wafanyakazi na ipo tayari kuwapigania, jambo la msingi tutangulize maslahi ya Taifa, kawaambieni wafanyakazi wachape kazi na Serikali itawalinda” amesema Mhe. Rais Magufuli.

6_6.JPG


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa TUCTA Tumaini Nyamhokya mara baada ya kumaliza kikao na kupiga picha ya pamoja Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wao Viongozi wa TUCTA wakiongozwa na Rais wa Shirikisho hilo Bw. Tumaini Nyamhokya wamempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa juhudi kubwa zinazochukuliwa na Serikali yake kujenga uchumi imara, kuimarisha utendaji kazi wa watumishi wa Serikali, kupambana na rushwa, kuondoa watumishi hewa na kulipa madeni ya watumishi.

Viongozi hao wameahidi kushirikiana na Serikali katika kusimamia haki na wajibu wa wafanyakazi na wameomba Serikali iendelee kufanyia kazi masuala mbalimbali ya wafanyakazi ikiwemo kuwalipa stahili zao na kuboresha mazingira ya kazi.

5_18.JPG


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na baadhi ya viongozi wa TUCTA mara baada ya Kikao chao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mei mosi naona ipo kwenye maandalizi ya kuwahadaa wafanyakazi.Yaani awamu hii wafanyakazi watammsi jk manake hotuba zake na ahadi zake za mei mosi kuaga anazitimiza kwa 99.99999% sio huyu anaye fikiri bado waziri wa ujenzi.
 
Viongozi wa tucta niwachumia tumbo kama wachumia wengine..hawajali wengine niwabinafsi wanajipenda wenyewe
 
Uwezi kufanya kazi kama masilah sio lazima wataboronga 2 hizo kazi kama walimu wanateseka san madeni kibao huko mitaani yan kam sio mtumishi wa serikali mpk wanafkia kukumbka kipindi cha nyuma.
 
Kirefu cha TUCTA ni kama alivyo fafanua mtoa mada? Na TUICO kirefu chake nini?
 
Tucta haaahaaa mei mosi hainihusi mie ni mkulima ..ila nafurah wafanyakaz coz walikuwa wanaringa sana ooooh mie afisa huku kalewa siku hizi uafisa wa wap?
Mafanikio hayaji kwa kumchukia aliye fanikiwa.
 
Kama Bunge tu halisikilizwi ndio hao watasikilizwa kweli?

Mei Mosi ndio imewafanya wakutane na maana Bajeti teyari imeshapangwa bado tu kupitishwa.
Bunge na Tucta vitu viwili tofauti.. Tucta ni wataalamu.. Bunge limekusanya watu mbalimbali.. Wanao jielewa na wasiojielewa.. Sababu tu kapigiwa kura basi yupo bungeni.. Jaribu kuangalia lugha ya bungeni, baadhi ya Wabunge hawana lugha za kiongozi
 
Simuoni raisi wa Dar es salaam katika picha! Tukirudi kwenye mada, TUCTA wameenda kuosha sura tu hakuna kitu wanaweza kubadilisha, pale ni kisiki cha mpingo..
 
Raisi wetu akifanya Mkutano na Viongozi wa Shirikisho wa Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), Ikulu Jijini Dar!
1.jpg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika kikao na Viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (Trade Union Congress of Tanzania -TUCTA) Ikulu jijini Dar es Salaam April 20, 2017
2.jpg
Nawashauri mwajiriwa yeyote alie member wa tucta ajitoe tu,wanapokea contribution kila mwezi ila hawana kazi wanayofanya. Tucta na cwt kazi bure
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom