MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha pamoja na kuzungumza na Balozi wa Marekani hapa nchini Mark Childress Ikulu jijini Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia hapa nchini anayemaliza muda wake Luigi Scotto Ikulu jijini Dar es Salaam
=========================================================
Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe. Mark Childress aliyekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema kutolewa kwa fedha hizo ni uthibitisho kuwa kutotolewa kwa fedha za awamu ya pili ya mradi wa changamoto za milenia (MCC-2) hakujaondoa uhusiano na ushirikiano wa Tanzania na Marekani ikiwemo utoaji wa misaada ya maendeleo.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia hapa nchini anayemaliza muda wake Luigi Scotto Ikulu jijini Dar es Salaam
=========================================================
"Tumezungumza mambo kadhaa, na wiki hii Tanzania na Marekani kupitia shirika letu la misaada la USAID tunatarajia kutiliana saini mkataba wa zaidi ya dola milioni 400 kwa ajili ya mwaka ujao, pia tumezungumza kuwa kutakuwa na dola milioni 800 zitakazotolewa na Marekani kwa ajili ya miradi mbalimbali na hii haihusiani na MCC.
"Ukweli ni kwamba tunayo mengi ya kufanya pamoja katika sekta mbalimbali zikiwemo afya, elimu na kilimo na tutafanya kila juhudi kuhakikisha haya yanafanikiwa" Amesema Balozi Mark Childress muda mfupi baada ya kumaliza mazungumzo na Rais Magufuli.
Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amesema serikali yake ya awamu ya tano itaendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano na ushirikiano na Marekani na kwamba fedha za msaada kutoka Marekani ni muhimu kwa maendeleo ya Tanzania.
Katika hatua nyingine Rais Magufuli ameagana na Balozi wa Italia hapa nchini Mheshimiwa Luigi Scotto ambaye amemaliza muda wake wa miaka mitatu.
Balozi Luigi Scotto amesema katika kipindi chake amewezesha kuongezeka kwa biashara kati ya Italy na Tanzania kwa asilimia 35 na ameielezea Tanzania kuwa ni nchi nzuri aliyoipenda na kwamba ataendelea kutangaza fursa zilizopo Tanzania huko Italia na kwingineko.