Rais Magufuli akutana CAG Prof Musa Juma Assad, DPP Biswalo Eutropius Mganga na Mufti Sheikh Zuber

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli leo amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wanne Ikulu, Dar es salaam.

Taarifa kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Gerson Msigwa alisema Rais Magufuli alikuwa na na mazungumzo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Juma Assad kuhusukupunguza gharama za matumizi ya kuendesha serikali na kuongeza ukusanyaji wa mapato ya Serikali.
CAG.jpg

Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Prof. Mussa Juma Assad akizungumza na Rais Magufuli.

Rais Magufuli pia amekutana na Mkurugenzi wa Mashitaka Tanzania, (DPP) Biswalo Eutropius Mganga ambaye amesema mazungumzo yao yalihusiana na mikakati ya namna ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka inavyopaswa kufanya kazi ili kuendana na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano isemayo “Hapa Kazi Tu”
DPP.jpg


Rais Magufuli akisalimiana na Mkurugenzi wa mashtaka Bw. Biswalo Eutropius Mganga

Kiongozi Mwingine aliyekutana na Rais Magufuli ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zuber Ally ambaye amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri
SHEH2.jpg

Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuber Ally akizungumza na Rais leo Ikulu
 
Its Obvious, kwani hatuyajuhi huku uswazi yapo hayo, hivi magufuli anajisikiaje kukaa ofosini na fenicha za kichina?

Kwa hiyo ulitaka ayatupe hayo halafu anunue mengine kwa watanzania kwa gharama nyingine kindly refer ' what would Magufuli do"
 
Back
Top Bottom