MTV MBONGO
JF-Expert Member
- Feb 18, 2016
- 1,261
- 1,222
enzi za JK kilio kikubwa kwa wananchi ni RUSHWA na MAFISADI. japo matatizo ni mengi. Dk. Magu tangu aingie madarakani anavuma katika anga hizo hizo. ametumbua watu zaidi ya 150 kitu ambacho hakijawahi kutokea ktk historia ya Bongo. mipango yake ya kudhibiti watumishi hewa waliomshinda JK, mipango ya flyovers na mengineyo inawavutia wengi. hata ktk ishu ya sukari watu wengi wameelewa nia nzuri ya prezidaa. iwapo atakuwa mwaminifu wa kweli mpaka mwisho, tutafika mbali sana na tutafunika EAST & CENTRAL AFRICA. sidhani kama baada ya yeye kuna mpinzani atakayeweza kusimama dhidi ya mgombea wa chama tawala baada ya Dk. Magu. ila kinyume chake, akiharibu yeye huku watu wakikumbuka ya JK, nadhani chama tawala kitaanguka kwa kishindo cha ajabu