Rais Magufuli akitaka kufanikiwa aruhusu immigrants na Dual Citizenship

MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,143
3,222
Rais magufuli akitaka kufanikiwa awamu hii fanya hivi

Ruhusu immigrants waje wafanye kazi Tanzania bila working permit, kwa sababu.
  • Wahamiaji huwa ni creative
  • Wahamiaji huwa ni cheap labour
  • Wahamiaji huwa wanatengeneza ajira kutokana na uzoefu wao waliotokana nao huko
  • Wahamiaji unawatumia utalaam wao, na ulitumia zero cost kuwasomesha. Nchi zao ziliwasomesha tokea chekechea mpaka chuo kikuu, harafu wewe ukawatumia kama cheap labour.
  • Wahamiaji hawatokuja kujichanganya kazi na siasa.
  • Wahamiaji hatatumiwa kwa hujuma za kisiasa.
  • Wahamiaji hawatakuja kuandamana hata siku moja kwa sababu zozote zile.
Ruhusu DUO Citizenship:
Hii ni haki ya binadamu na ya msingi, dunia ni kijiji sahivi huwezi jifungia tu, pia utapata watanzania wazawa na wenye asili watalaam kwelikweli. Hata CHINA, walituma watoto wao ulaya na marekani kuiba utaalamu.

Hiyo elimu tunayofundishwa hapo Tz hatutakuja kugundua kitu chochote wala kuitumia kwa lolote zaidi ya kuitumia kama application tu. Kuna kitu wazungu wametuficha ktk elimu na ili ukipate lazima u dispatch watoto wawe na uraia wa huko ulaya na waje watuletee hiyo elimu. Huwezi mtuma mtu eti kusoma bachela akapata hiyo elimu. Kwa elimu ya Tanzania tutawalaum bure ma prof.
---------------------------------------------------------------------------
Na

Wanasiasa wengi wa Tanzania wamenunua nyumba nje ya Tanzania. Hii ukiwa na nyumba nje ya Tanzania tayari ni implicitly huyu mwanasiasa ana Dual citizenship. Harafu huyu mwanasiasa akitoka hapo anaenda ku brainwash wananchi wa kawaida kwamba hataki dual wakati wenyewe tayari wanazo.
---------------------------------------------------------------------
Mimi naamini kuna kitu wazungu wamekificha ktk elimu. Mfano
Impact of Immigration on UK Economy
Impact of Immigration on UK Economy | Economics Help

Na
Changes to immigration rules boost businesses and students - News stories - GOV.UK
International students and businesses are set to benefit from a series of changes to the Immigration Rules being announced today.

The changes are part of the government’s continuing work to ensure the best and brightest talent can come to the UK to work, study and invest in business.
---------------------------------------------------
Na
Harafu wenye raia moja ya Tanzania ndo wanaficha Hela Dubai, Jersey, Switzland. Yani anaiibia Tanzania huyu mwenye raia moja ya Tanzania anazificha hizo pesa UK, na UK wanamzurumu hizo pesa wanawapa watu raia wa UK kama job seeker allowances.
Maana hizi hela za mafisadi wanazozificha zurich huwa wanazurumiwa tu at the end. Wananyimwa visa ama kupewa ban yakukanyaga EU ama US.

On the other hand, huyu anaenyimwa Dual citizenship mtanzania safi anayefanya kazi UK anatuma pesa Tanzania harafu wanaziita diaspora remittances, eti hizi diaspora remittances ni mhimu kwa uchumi wa Tanzania. By the way, it's mad.
----------------------------------------------------------
Na
Kuna maziwa mengi na mito mingi wenda kuliko nchi yoyote duniani. Tuna ardhi yenye rutuba na iliyo wazi wenda kuliko nchi nyingi. Na bado, Rais unapewa warnings na wananchi kwamba watapatwa na njaa sababu mvua inasuasua. Na utatakiwa kuwapatia chakula wananchi hawa pindi njaa itakapo chachamaa, yote unayotegemea kufanya yanakuwa reversed na kubaki kupiga hatua palepale. The thing is reverse biased, you should get it forward biased. Kivipi

Ruhusu Dual citizenship na immigrants, they would close this gap once and for all.
 
Hilo la kuwaruhusu waje kufanya kazi bila working permit nalikataa. La dual citizenship bado sijaekewa kwa nini tunang'ang'ania kuwa na uraia wa nchi moja. Ngoja wataalamu waje kukufafanulia vizuri hili.

Unakumbuka Botswana wakati inapata uhuru? ilichukua wataalaam around africa, bila wao kuingia gharama ya kuwasomesha wala kuwapa mkopo wala nini imewachukua wameshaiva tayari. Kawaangalie leo Botswana ulinganishe na wengine.

Pili nchi kama UK wakitoa immigrants ina collapse.

Tatu na mwisho unafikiri kwanini US hua wanatoa green cards? immigrants ni mhimu sana ktk kujenga uchumi.
 
Ni kweli immigrants ni muhimu lakini bado nasisitiza wawe na working permit. Bado naamini tuna wataalamu kwenye nyanja nyingi tu na wengi hawana kazi. Tukiruhusu watu wa nnje waje kufanya kazi kwetu tunatakiwa tujiridhishe pasipo shaka kuwa hatuna hao wataalamu. Ulaya kazi ni ngumu pia,na wanachofanya ulaya wanaanzisha projects Africa na mahala pengine ili watu wao wapate kazi. Sasa tukiwapa hii loop hole watajazana hapa kwetu na kuwanyima nafasi wazawa wenye sifa.
 
Uko na wazo zuri niliwai kufika ngara na ujiji kuna waburundi wengi sana ni cheap labour wanapiga Kazi sana na niwaaminifu"

Pia moja ya siri ya CHINA ilituma watoto wakajichanganya huko ulaya na marekani wakasoma siri ya elimu yenyewe ya mafanikio wakasoma teknolojia ya ukweli ukweli na wakairudisha huko kwao. Na ndiyo wakawa na uwezo wa ku reverse engineering.

Iran, nuclear kuipata hiyo elimu, waliwachanganya watoto wake ktk shule za ujerumani wakawa kama wajerumani, walivyoiva kama scientists ndo wkarudi Iran. Huwezi pata hii elimu kama huna uraia wa nchi husika, itaishia shule za kata za ulaya. Huwezi ingia military school za ulaya zinazogundua ma vitu kama huna uraia mzazi wa mtoto.
 
Immigrants sio tatizo , ila tatizo letu mifumo yetu ina loopholes zina zo wezesha. Watu kukwepa kodi.
Wenzetu waliondelea mifumo Yao inaku sababisha ufanye kazi Maana Huna mjomba wa ku mtegemea na pili una lipa kodi na kununua bidhaa zao iwe chakula Nguo etc na hata Kama uta tuma hela nyumbani au kwenu lakini kwa ujumla wake wanakuwa wame faidika na uwepo wako na kuwepo kwako pia unaongea ajira na kukuza service industry Kama bank , air transport , masuka ya vyakula na Nguo etc
 
Unakumbuka Botswana wakati inapata uhuru? ilichukua wataalaam around africa, bila wao kuingia gharama ya kuwasomesha wala kuwapa mkopo wala nini imewachukua wameshaiva tayari. Kawaangalie leo Botswana ulinganishe na wengine.

Pili nchi kama UK wakitoa immigrants ina collapse.

Tatu na mwisho unafikiri kwanini US hua wanatoa green cards? immigrants ni mhimu sana ktk kujenga uchumi.
ni kwa kuwa walioenda kufanya kazi Botswana walikuwa cheap au ni kwa sababu Botswana hawakuwa na wataalamu wa kutosha na pesa walikuwa nayo ya ku import wataalamu? which is which? Je Dkt mtanzania alikuwa analipwa less than dkt wa Botswana?!
 
Ni kweli immigrants ni muhimu lakini bado nasisitiza wawe na working permit. Bado naamini tuna wataalamu kwenye nyanja nyingi tu na wengi hawana kazi. Tukiruhusu watu wa nnje waje kufanya kazi kwetu tunatakiwa tujiridhishe pasipo shaka kuwa hatuna hao wataalamu. Ulaya kazi ni ngumu pia,na wanachofanya ulaya wanaanzisha projects Africa na mahala pengine ili watu wao wapate kazi. Sasa tukiwapa hii loop hole watajazana hapa kwetu na kuwanyima nafasi wazawa wenye sifa.

Mkuu nakubaliana na hoja zako, lakini unafikiri tunawatalaamu sehemu yoyote ile? I bet you hatuna. Mfumo wa elimu yetu hatuna wataalamu, hii elimu ni kuwa mtumiaji, siyo utaalamu huo. Na ndio maana tunawalamu ma prof kila siku. Swala la wataalamu serikali iangalie namna ya DUO citizenship.
 
Unakumbuka Botswana wakati inapata uhuru? ilichukua wataalaam around africa, bila wao kuingia gharama ya kuwasomesha wala kuwapa mkopo wala nini imewachukua wameshaiva tayari. Kawaangalie leo Botswana ulinganishe na wengine.

Pili nchi kama UK wakitoa immigrants ina collapse.

Tatu na mwisho unafikiri kwanini US hua wanatoa green cards? immigrants ni mhimu sana ktk kujenga uchumi.

Unaongea vitu tofauti, Watswana walikuwa hawataki shule na kulikuwa hawana wasomi ndio kisa cha kutafuta wafanyakazi kutoka nje
Tanzania tulishapita kwenye hiyo stage, baada ya uhuru kulikuwa na Wanigeria wengi walikuja kufanya kazi, pia Wamalawi, Wanyarwanda, Waganda, Wakenya, wazambia pia walikuwepo, kwa sasa Tanzania haina shortage ya skilled people
 
Ningekuunga mkono ungesema serikali isibane kuajiri wasomi wa ngazi ya PhD toka nchi kama Uganda ili vyuo vyetu viwe na walimu wa kutosha wenye sifa...maana najua Uganda kuna PhDs za kutosha lakini ajira hawana...sasa hivi vyuo vya privae vingeruhusiwa bila masharti kuajiri toka nchi jirani (hata vya serikali) ili waje watufundishie wanetu...ila walipwe local rates
 
Hilo la kuwaruhusu waje kufanya kazi bila working permit nalikataa. La dual citizenship bado sijaekewa kwa nini tunang'ang'ania kuwa na uraia wa nchi moja. Ngoja wataalamu waje kukufafanulia vizuri hili.
Mkuu nikiangalia sana WEWE SI mtanzania. Hata hivyo nitakusaidia. WAHAMIAJI hawatoi CHEAP labour bali WAZAWA. CREATIVITY haiko based on WAHAMIAJI. Kuna watanzania WENGI walio CREATIVE. Hivyo hiyo NAIKATAAA!
Nakubaliana nawe kuwa DUAL CITIZENSHIP ni sawa. Kwa mtazamo wangu mtu anaweza KUGOMBEA nafasi YEYOTE KISIASA lakini SI URAIS!!!

Maana watanzania HAWAWAJUI ni kwa nini WALIUKANA URAIA wa Tanzania.

Kuhusu KURUHUSU immigrants bila REGULATED process ITAUA AJIRA ya WAZAWA. Ila tu mahali TZ HAWANA wataalamu!
 
Unaongea vitu tofauti, Watswana walikuwa hawataki shule na kulikuwa hawana wasomi ndio kisa cha kutafuta wafanyakazi kutoka nje
Tanzania tulishapita kwenye hiyo stage, baada ya uhuru kulikuwa na Wanigeria wengi walikuja kufanya kazi, pia Wamalawi, Wanyarwanda, Waganda, Wakenya, wazambia pia walikuwepo, kwa sasa Tanzania haina shortage ya skilled people

Tanzania ,Ina shortage nenda kwenye mambo ya ICT utakuta watu kutoka nje ya nchi wakenya nk. Hata hivyo , unafikiri sisi tunaelimu sana kuzidi UK, US-green cards na Germany?
 
Mie nadhani kusiwekwe work permit,tutapata massive number ya watu watakaotaka kuja Tanzania,hapa sasa ndio tuchuje nani abaki nani aende,Tuangalie wapi tuna short ya skills,kama ni engineers,madaktari,nurses ama wafanya biashara,hawa ndio wapewe residency permit hapa Tanzania.
 
Mkuu nikiangalia sana WEWE SI mtanzania. Hata hivyo nitakusaidia. WAHAMIAJI hawatoi CHEAP labour bali WAZAWA. CREATIVITY haiko based on WAHAMIAJI. Kuna watanzania WENGI walio CREATIVE. Hivyo hiyo NAIKATAAA!
Nakubaliana nawe kuwa DUAL CITIZENSHIP ni sawa. Kwa mtazamo wangu mtu anaweza KUGOMBEA nafasi YEYOTE KISIASA lakini SI URAIS!!!

Maana watanzania HAWAWAJUI ni kwa nini WALIUKANA URAIA wa Tanzania.

Kuhusu KURUHUSU immigrants bila REGULATED process ITAUA AJIRA ya WAZAWA. Ila tu mahali TZ HAWANA wataalamu!

Regulated process ipi? wewe ukiwa na kampuni unaitisha interview anayeweza ndo unamchukua.
Wahamiaji ni creative kutokana na ukweli kuwa anakuwa hayupo nyumbani na anatumia uwezo wa ziada ili ku survive, hapo ndo creativity inapokuja.
 
Back
Top Bottom