Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,252
- 113,645
Labda ndio maana tumekumbushwa kutokunukuu tofauti/kinyume?Umesoma ulichokiandika? Umezingatia misingi ya uandishi kutenga paragraph za kauli za Magufuli na paragraph ya kile unachokiamini wewe?
Umesema kweli. Maalim akiandika kitabu na akawa na uhuru wa kuelezea yale mambo yaliyo nyuma ya pazia basi kitakuwa kitabu kizuri sana. Na nia hasa ya kuandika vitabu kama hivi ni kusimulia yale mambo ambayo hayajulikani au hayajawekwa hadharani.
JK hana cha kuandika, sana sana ataandika jinsi timu yake ya Totteringham jinsi inavofungwa baada ya kuwapiga chenga Watanzania waliokuwawa na hamu ya kufahamu nini kilichokuwa kinajiri nyumbani Tanzania. Lingine analoweza kuandika ni lile la kuvinjari kama kapagawa kwa pesa za walipa kodi.
Kilizinduliwa kimya kimya hicho, JK hachoki kwa vituko, Mwenyezi Mungu amjalie Maisha mema na starehe zake, hakuwajali kabisa Watanzania masikini...Nadhani Kikwete ameandika kitabu hivi karibuni.
..I thought alikuwa ughaibuni hivi karibuni ku-introduce kitabu chake.
Mimi ningefurahi sana kusoma vitabu vya hawa:
1) Freeman Mbowe
2) Tundu Lissu
3) Mawazo, Ben Saanane, Mwangosi na Filikunjombe. Hawa nimewaweka pamoja kwa sababu ni marehemu, wengine wanaweza kufanya tafiti na kuandika juu yao.
..Kikwete naye ameandika.
..ila sijakiona amazon.
Cha Ndugai siwezi kukisoma kabisa. Ila hivi vitabu wanaandika tu yale wanayotaka tuyajue. Mengine wanaficha.Katika uzinduzi wa kitabu cha Rais mstaafu Benjamin Mkapa uliofanyika mapema leo, Rais John Magufuli amewahimiza viongozi wastaafu kuandika vitabu vya maisha yao.
Hususan, Rais Magufuli amesema atafurahi kusoma kitabu cha Maalim Seif Sharif Hamad.
Kwa kweli hata mimi nitafurahi sana, mno, kukisoma kitabu cha Maalim Seif.
Harakati zake za kupigania demokrasia zimeanzia mbali sana.
Na kilele chake nadhani kilikuwa ni ule uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi wa mwaka 1995!
Naamini Maalim alishinda urais wa Zanzibar.
Ila kwa inda na figisu ambazo inadaiwa ziliongozwa na Rais mstaafu Nyerere, ushindi wa kupikwa akapewa ‘Komandoo’ Salmin Amour! Hivi yuko wapi huyu mtu siku hizi??
Lakini, kweli Maalim anaweza kuandika kitabu chake na kutiririka kwa uhuru bila ya serikali kutaka kumfanyia cencorship?
JK hana cha kuandika, sana sana ataandika jinsi timu yake ya Totteringham jinsi inavofungwa baada ya kuwapiga chenga Watanzania waliokuwawa na hamu ya kufahamu nini kilichokuwa kinajiri nyumbani Tanzania. Lingine analoweza kuandika ni lile la kuvinjari kama kapagawa kwa pesa za walipa kodi.