Rais Magufuli ahamasishe muswada wa mahakama ya mafisadi

ng'adi lawi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
2,956
1,114
Bunge letu limejaa mafisadi na watetezi wa mafisadi na wanafiki kwa hiyo namna ya kuwatambua na kuwang'oa ni kuupeleka huo muswada huo haraka. Wale watakaopinga watajidhirisha na kwa kuwa ni wengi muswada utakataliwa. Ikifikia hapo rais avunje bunge ili tumchagulie wabunge safi. Bila kufanya hivyo rais wetu kipenzi atahujumiwa na hili bunge na atafanya kazi katika mazingIra magumu.
 
Mahakama tayari ipo na kama ingekuwa inafanya kazi inavyotakiwa aliyesimamia uuzwaji wa nyumba za serikali, ununuzi wa MV Dar es Salaam kutoka India, utafunaji wa hela za barabara n.k naye angekuwa tayari kizimbani.
 
Hiyo mahakama ni hatari.Nchi itayumba.Hakuna haja ya hiyo mahakama tuendelee hivi hivi huku sisi wa chini tukikiona cha mtema kuni kimaisha.
 
Kibaraka wa kwanza wa mafisadi huyu hapa
 
Hivi karibuni nikiwa Nairobi nilibahatika kuzungumza na rafiki mmoja ambaye ni jaji wa Mahakama Kuu ya Kenya. Tuligusia hilo la mahakama ya mafisadi akazungumza ukweli fulani kwa njia ya utani. Alisema, "Nani aliwaambia kuwa sisi majaji hatutaki pesa? Kama raisi wangu angeamua kuanzisha mahakama hiyo hapa, ningefurahi sana akiniteua kuwa jaji wa mahakama hiyo. Ningesahau umasikini milele." Nikamuuliza, "Unamaanisha nini?" Akaniambia, " Mabilionea wangapi ambao wamefungwa ama kufilisiwa? Labda ambao hawajui kucheza karata zao vizuri." Nilimuelewa vizuri.
 
Mahakama tayari ipo na kama ingekuwa inafanya kazi inavyotakiwa aliyesimamia uuzwaji wa nyumba za serikali, ununuzi wa MV Dar es Salaam kutoka India, utafunaji wa hela za barabara n.k naye angekuwa tayari kizimbani.
Huko hawagusi maana wakigusa huenda Magufuli akaifuta hiyo mahakama, hairuhusiwi kuendesha kesi za Mwakyembe juu ya mabehewa mabovu ambayo sasa kawasukumia mpira wa chini wanaoteseka yeye anapeta bungeni na wizarani,ccm wanambeba kwa sababu aliwasaidia kumrubuni Dr Slaa hadi akawasariti Ukawa.
 
Hiyo mahakama ni hatari.Nchi itayumba.Hakuna haja ya hiyo mahakama tuendelee hivi hivi huku sisi wa chini tukikiona cha mtema kuni kimaisha.
Wakitaka watu waiamini hiyo Mahakama waanze na kesi ya Uuzaji nyumba za Serikali, ununuzi wa kivuko kibovu cha Mwaka 1978 kwa billion 8 wakati kivuko kipya cha Azam tena kikubwa kimenunuliwa kwa billion 5 tu,kesi za escrow, Buzwagi, mikataba ya madini, Gesi, uagizaji sukari nje ya Nchi, pesa za ccm kupigwa na wajanja ikibidi Mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali apitie ccm makao makuu ajionee kisha kazi ianze, hiyo Mahakama kwa kuanzia ianze na hapo tu angalau italeta maana, kinyume na hapo hiyo Mahakama isianzishwe kabsa maana itakosa mashiko.
 
Mahakama ya Mafisadi kama haitakuwa na kesi za Escrow, uuzaji mshirika ya umma na nyumba za Serikali pamoja na Ununuzi wa kivuko feki, mabehewa chakavu, tenda za Ununuzi Magari ya Serikali, ndege ya Rais, ulaji chenji ya rada na chenji ya bunge la Katiba na Ufujaji mwingineo mwingi isianzishwe kabsaaa maana bila hizo kesi hiyo itakuwa Mahakama ya wajanja wachache.
 
Back
Top Bottom