Rais Magufuli afichua ufisadi miradi hewa ya maji

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1069670

RAIS John Magufuli amechua miradi hewa ya maji, yenye thamani ya Sh bilioni 102, iliyotakiwa kutekelezwa katika kipindi cha mwaka 2013/2018. Alibainisha hayo jana katika Mji Mdogo wa Makambako mkoani Njombe, wakati akiifungua Barabara ya Manga-Nyigo-Igawa yenye urefu wa kilomita 138.7.

Barabara hiyo imejengwa kwa gharama ya Sh bilioni 232.6, ambazo ni mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia. Rais Magufuli aliishukuru Benki ya Dunia kwa kuikopesha Tanzania fedha hizo, zilizofanikisha ujenzi wa barabara hiyo. Kuhusu tatizo la miradi ya maji nchini, Rais Magufuli alisema ulifanyika uhakiki wa miradi ya maji kuanzia mwaka 2013/2018 na wataalamu kutoka Wizara ya Fedha.

Miradi ya maji iliyohakikiwa na wataalamu hao, ilikuwa na thamani ya Sh bilioni 119, lakini uhakiki ulibaini miradi ya kweli ilikuwa na thamani ya Sh bilioni 17 tu. Alisema miradi mingine yote ambayo thamani yake inakuwa ya Sh bilioni 102, ilikuwa miradi hewa na fedha hizo hazikulipwa. Kutokana na hilo, alimtaka Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa kufanya mabadiliko katika wizara hiyo, kwa kuwabana watendaji wake ili miradi ya maji iwe halisi na ikamilike kwa wakati na wananchi wapate maji.

Rais Magufuli pia alimtaka Mbarawa kuhakikisha Sh bilioni 45 zilizotengwa kwa ajili ya miradi ya maji katika mji wa Makambako, zinatumika kama ilivyokusudiwa na ahakikishe miradi hiyo inakamilika. Awali, Profesa Mbarawa alimweleza Rais kuwa upatikanaji wa maji Makambako unakia asilimia 61.2 na mkandarasi atakayetekeleza mradi wa maji wa Makambako wa Sh bilioni 45, ataanza kazi ikapo Septemba, mwaka huu.

Wakati akisisitiza kuhusu kupatikana kwa maji Makambako, mwananchi mmoja aliyejulikana kwa jina la Albert akiwa na bango lake, aliitwa na Rais Magufuli ili kueleza shida yake. Albert alimweleza Rais kuwa katika eneo la Manga, maji hutoka wanapokuja viongozi wa kitaifa tu na baada ya hapo maji hutoweka na tatizo hilo limekuwepo tangu mwaka 2009.

Kauli hiyo ya Albert ilimfanya Rais Magufuli kumwita Mkurugenzi Mtendaji wa Makambako na Mhandisi wa Maji, kujieleza kwa nini kuna tatizo hilo. Katika maelezo yao, walimweleza Rais kuwa baadhi ya vifaa yakiwemo mabomba na viunganishio, havikuwa na ubora uliotakiwa na yalikuwa yakipasuka kila mara, jambo lililomfanya Rais asiridhike na maelezo hayo na kumtaka Waziri Mbarawa kufuatilia.

Barabara Kwa upande wa miradi ya barabara, Rais Magufuli aliiagiza Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Wakala wa Barabara (Tanroads), kuhakikisha gharama za kutengeneza kilomita moja ya barabara kwa gharama ya Sh bilioni 2 inashuka mara moja, la sivyo wasimwite tena kufungua barabara itakayojengwa kwa gharama hiyo.

Akisisitiza kuhusu kupanda kwa gharama za kujenga barabara kwa kilomita kuka Sh bilioni 2, Rais Magufuli alisema pamoja na kazi nzuri inayofanywa na Wizara na Tanroads, lakini makadirio yao ya ujenzi kwa kilomita yameanza kuwa juu. “Tangu nilipoanza ziara yangu mkoani Mtwara mpaka Njombe, nimekuwa nikishuhudia hilo, kwa mfano barabara niliyoweka jiwe la msingi ya Njombe- Makete yenye urefu wa kilomita 107, inagharimu Sh bilioni 224, maana yake kwa kila kilomita moja inagharimu Sh bilioni 2, hivyo hivyo kwa barabara ya Mbinga-Mbamba Bay yenye urefu wa kilomita 67, inajengwa kwa Sh bilioni 134, hilo ni tatizo,”alieleza Rais Magufuli.

Alisema Tanroads wameanza kubadilika kwa kuweka makadirio ya juu kwenye zabuni zao, hali inayowafanya wazabuni nao kuja na makadirio ya juu. Alisema yeye alikuwa Waziri wa Ujenzi kwa miaka 18, hivyo anajua michezo inayochezwa na wahandisi na kumtaka Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe kulifanyia kazi suala hilo. “Msinipeleke tena kwenye miradi mingine ambayo itajengwa kwa Shilingi bilioni 2 kwa kilomita, mtafungua wenyewe,” alisisitiza Rais Magufuli.

Aidha, Rais Magufuli pia alitoa mwito kwa Benki ya Dunia kupitia Mwakilishi wake, Denis Biseko aliyekuwepo kwenye ufunguzi huo akimwakilisha Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo nchini, Bella Bird, kuwa benki hiyo iiondolee Tanzania kikwazo cha kukopesheka kwa kuwa inachelewesha miradi ya maendeleo ya wananchi. Alisema hakuna nchi duniani, iwe tajiri au maskini, isiyokopa, kitu cha msingi ni uwezo wa nchi wa kulipa madeni hayo.

Alisema Tanzania kama inakopesheka maana yake ina uwezo wa kulipa, hivyo hakuna haja ya kuichelewesha miradi ambayo imepangwa kutekelezwa kwa fedha za mkopo kutoka benki hiyo. Kwa mujibu wa Rais Magufuli, kwenye miaka ya 1990, Benki ya Dunia ilikuwa inachelewesha kutoa cheti hicho (no objection), na matokeo yake Tanzania ilianza kutengeneza barabara kwa fedha zake yenyewe. Alisema Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa, iliamua kutenga Sh bilioni 1.4 kila mwezi katika bajeti yake kwa ajili ya kujenga barabara nchini.

Kwa kuwa fedha zinazokopwa, hazitumiki kwa ajili ya kulipa mishahara au chai ya rais au rais kusari nje ya nchi, ila ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo inayogusa maisha ya wananchi, Rais Magufuli alimtaka Biseko kukisha ombi lake kwa Mkurugenzi Mkazi wa benki hiyo, Bella ili kikwazo hicho kiondolewe. Kutokana na wananchi wa Makambako kudai dia ya maeneo yao kuchukuliwa kwa ajili ya kujengwa Kituo cha Kutolea Huduma cha Pamoja (One Stop Centre), Rais Magufuli alimwagiza Waziri Kamwelwe kubaki Makambako mpaka atakapomaliza kutatua tatizo hilo.

Kwa mujibu wa Rais Magufuli, Wizara na Tanroads walichukua eneo kubwa kuliko inayohitajika, lenye urefu wa kilomita mbili na upana wa mita 400. Alisema eneo hilo ni kubwa na ndiyo maana wanashindwa kuwalipa wananchi dia wanayoidai. Alimtaka Waziri Kamwelwe kubaki ili kusimamia eneo hilo kupimwa upya na kuchukua mita 500 tu, badala ya ukubwa wa awali.

Alisema lengo la kituo hicho ni kuyafanya malori yanayotoka Dar es Salaam kwenda mikoa ya Kusini na nchi jirani, kufanyiwa ukaguzi na baadhi ya idara za serikali ikiwemo Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) na Polisi. Rais Magufuli alikuwa katika ziara ya siku tatu mkoani humo tangu Jumanne wiki hii akitokea mkoani Ruvuma.
 
View attachment 1069670

1.5T ambazo hazijulikani ziliko ni nyingi sana ukilinganisha na hizo 102B, it is only 0.07% ya hiyo 1.5T iliyoterezea kusikojulikana

Kweli nyani haoni kaliole….. Ahahahahahahaaa
 
Back
Top Bottom