Rais Magufuli afanya uteuzi na kutumbua. Dr. Bana, Kipilimba waula. RC Kebwe wa Morogoro achinjiwa baharini

Kila siku teuzi tu tumeshachoka!!

Yaani uteuzi unatangazwa live, alafu Bunge liko gizani na wajinga wanaamini huu ndio uongozi unaotufaa!!
Alishasema,ukizembea atakutumbua.Uzembee halafu uachwe au uhamishwe,no way.That is history.Huwezi kazi uliyoteuliwa kuifanye kajitafutie shuhuli nyingine.Hapa kinachoangaliwa ni kazi,huna output kule!Kwa hiyo unataka uteuzi ufanywe kimya kimya,anaogopwa nani.Akili zingine bwana,dah.
 
Mabalozi wapya 12 walioteuliwa na Rais Dkt Magufuli leo, ambao watapangiwa vituo vya kazi hapo baadae:

1. Mohamed Mtonga
2. Dkt. Jilly Maleko
3. Dkt Benson Bana
4. Meja Jenerali Mstaafu, Anselimu Bahati
5. Prof. Emmanuel Mbennah
6. Maimuna Tarishi
7. Meja Jenerali Mstaafu, Gaudence Milanzi
8. Ali Jabir Mwadini
9. Dkt Modestus Kipilimba
10. Jestas Nyamanga
11. Prof. Dr. Kennedy GASTORN
12. Mhandisi Aisha Amour

Vituo vitakavyojazwa na Mabalozi wapya ni:

1. Falme za Kiarabu (Abu Dhabi)
2. Bujumbura (Burundi)
3. Brussels (Ubelgiji)
4. Cairo (Misri)
5. Harare (Zimbabwe)
6. Kuwait City (Kuwait)
7. Pretoria (Afrika Kusini)
8. Riyal (Saudi Arabia)
9. Tokyo (Japan)
10. Umoja wa Mataifa (Switzerland)
11. Umoja wa Mataifa (New York)
12. Abuja (Nigeria)

NB: Mlingano wa namba haumaanishi kuwa ndio kituo cha kazi cha balozi husika.
Kahendaguza wa Umoja wa Mataifa (Switzerland), amefanya kosa gani hadi kurudishwa nyumbani?
 
Matangazo ya moja kwa moja kutoka Ikulu Jijini Dar es Salaam kuhusu uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli yatawajia kuanzia saa 9:20 alasiri leo tarehe 20 Septemba, 2019.

View attachment 1212456

========================

Rais Magufuli amefanya mabadiliko ambapo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Charles Kabeho, amehamishiwa wilaya ya Chato na Mkuu wa Wilaya ya Chato Msafiri Mtemi amehamishiwa Wilaya ya Tarime.

Rais John Magufuli memteua Lowata Sanare kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, pia amemteua Musa Masele kuwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro.

Rais Dkt Magufuli ameteua Mabalozi 12 ambao wataiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali. Uteuzi huo unatokana na vituo hivyo ama kuwa wazi, Mabalozi kumaliza muda wao, kustaafu au kurejeshwa nyumbani ambapo watapangiwa kazi nyingine.

Modestus Kipilimba, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), ameteuliwa kuwa Balozi. Kituo chake cha kazi kitatangazwa baadae.

Majina kamili ya Mabalozi walioteuliwa ni
1. Mohamed Mtonga
2. Dkt. Jilly Maleko
3. Dkt. Benson Bana
4. Meja Jen. (Mst), Anselimu Bahati
5. Prof. Emmanuel Mbennah
6. Maimuna Tarishi
7. Meja Jen. (Mst) Gaudence Milanzi
8. Ali Jabir Mwadini
9. Dkt Modestus Kipilimba
10. Jestas Nyamanga
11. Prof. Dr. Kennedy Gaston
12. Mhandisi Aisha Amour
Mbona wengine wakitumbuliwa hawaandikwi?
 
Da jamaa jina langu sijui walipeleka au ndio ilikua ahadi hewa mheshimiwa akiniteua naahidi sitamuangusha mi ntakua nalala site yani nikipata uteuzi tu napitia mlimani city nanunua tent langu naweka kwenye v8 kazi inaanza
wewe ndo unawaza km mimi kabisaaa! sijui kwa nini hanioni? ntapiga kazi wewe
 
Back
Top Bottom