Rais Magufuli afanya uteuzi na kutumbua. Dr. Bana, Kipilimba waula. RC Kebwe wa Morogoro achinjiwa baharini

Papaa Mobimba

JF-Expert Member
Jan 27, 2018
753
3,096
Matangazo ya moja kwa moja kutoka Ikulu Jijini Dar es Salaam kuhusu uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli yatawajia kuanzia saa 9:20 alasiri leo tarehe 20 Septemba, 2019.

A2F1481F-C548-43FC-A84F-96D8D06C7081.jpeg


========================

Rais Magufuli amefanya mabadiliko ambapo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Charles Kabeho, amehamishiwa wilaya ya Chato na Mkuu wa Wilaya ya Chato Msafiri Mtemi amehamishiwa Wilaya ya Tarime.

Rais John Magufuli memteua Lowata Sanare kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, pia amemteua Musa Masele kuwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro.

Rais Dkt Magufuli ameteua Mabalozi 12 ambao wataiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali. Uteuzi huo unatokana na vituo hivyo ama kuwa wazi, Mabalozi kumaliza muda wao, kustaafu au kurejeshwa nyumbani ambapo watapangiwa kazi nyingine.

Modestus Kipilimba, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), ameteuliwa kuwa Balozi. Kituo chake cha kazi kitatangazwa baadae.

Majina kamili ya Mabalozi walioteuliwa ni
1. Mohamed Mtonga
2. Dkt. Jilly Maleko
3. Dkt. Benson Bana
4. Meja Jen. (Mst), Anselimu Bahati
5. Prof. Emmanuel Mbennah
6. Maimuna Tarishi
7. Meja Jen. (Mst) Gaudence Milanzi
8. Ali Jabir Mwadini
9. Dkt Modestus Kipilimba
10. Jestas Nyamanga
11. Prof. Dr. Kennedy Gaston
12. Mhandisi Aisha Amour
 
Tunasubili kwa hamu kuwafahamu wateule kama habari hizi ni za kweli
 
Back
Top Bottom