Rais Magufuli afanya uteuzi na kutumbua. Dr. Bana, Kipilimba waula. RC Kebwe wa Morogoro achinjiwa baharini

Hivi ni KWA nini miaka yote marais huwa wanawateua Watu wazee, vibibi NA vibabu kwenda kuwa Mabalozi huko nje ya nchi???

Ina maana hakuna vijana wenye sifa ya kuweza kuteuliwa kuwa mabalozi??
Hivi vizee vinavyoteuliwa kuja kuwa mabalozi huko nje ya nchi vingi vina roho mbaya sana, vinatusumbua sana sisi Watanzania tunaoishi nje ya Tz wakati tunapokwenda kwenye Balozi za nchi yetu kufuata huduma.

Yaani unapofika ktk ofisi za Ubalozi wa Tz kufuata huduma unakiona kibabu au kibibi kimekunja sura KWA roho mbaya utadhani mbogo. Vizee hivi vingi bado vina mawazo ya UJIMA, wakimuona Mtanzania yoyote huko nje ya nchi wao wanamuhesabia kuwa ni Mzurulaji.

Tunaomba Rais awe anawateua vijana kuwa Mabalozi ambao wana mawazo mapya ya kisasa, yanayokwenda NA wakati, aache kuwateua vizee vilivyochoka mwili NA AKILI.
 
Matangazo ya moja kwa moja kutoka Ikulu Jijini Dar es Salaam kuhusu uteuzi uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli yatawajia kuanzia saa 9:20 alasiri leo tarehe 20 Septemba, 2019.

View attachment 1212456

========================

Rais Magufuli amefanya mabadiliko ambapo, Mkuu wa Wilaya ya Tarime Charles Kabeho, amehamishiwa wilaya ya Chato na Mkuu wa Wilaya ya Chato Msafiri Mtemi amehamishiwa Wilaya ya Tarime.

Rais John Magufuli memteua Lowata Sanare kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, pia amemteua Musa Masele kuwa Mkuu wa Wilaya ya Malinyi mkoani Morogoro.

Rais Dkt Magufuli ameteua Mabalozi 12 ambao wataiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali. Uteuzi huo unatokana na vituo hivyo ama kuwa wazi, Mabalozi kumaliza muda wao, kustaafu au kurejeshwa nyumbani ambapo watapangiwa kazi nyingine.

Modestus Kipilimba, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), ameteuliwa kuwa Balozi. Kituo chake cha kazi kitatangazwa baadae.

Majina kamili ya Mabalozi walioteuliwa ni
1. Mohamed Mtonga
2. Dkt. Jilly Maleko
3. Dkt. Benson Bana
4. Meja Jen. (Mst), Anselimu Bahati
5. Prof. Emmanuel Mbennah
6. Maimuna Tarishi
7. Meja Jen. (Mst) Gaudence Milanzi
8. Ali Jabir Mwadini
9. Dkt Modestus Kipilimba
10. Jestas Nyamanga
11. Prof. Dr. Kennedy Gaston
12. Mhandisi Aisha Amour
HAKYA MUNGUUUU BENSON BANA KAULAAAAA!A HAHAHAAHHHAHAHHAHHA MVUMILIVU HULA MBIVUUU HAHAHAH NO KUSHIKA CHAKI TENAAAAA NA KUSAHIISHAAAAA MITIANI
 
Watanzania wananampenda sana Rais wao Go on Magufuli wanasema Mwalimu alikuaga bora zaidi yako ila naona mpaka awamu inaisha utakua umeandika historia.
Haitakiwi na haifai kumlinganisha Nyerere na mpuuzi yoyote yule hapa Tanzania
 
Usiwe Mtumwa wa Kigogo. Ni kigogo huyohuyo alisema KP yuko chini ya ulinzi. Kingine inatakiwa ujue swala la kiongoz kutumbuliwa na kupewa cheo kingine ni kawaida
huyohuyo kigogo baadaye akasema wazee wameshauri apewe ubalozi.

mkuu kama una beef na huyo kigogo usinihamishie mimi.
 
Huyu alipewa kazi maalum akashindwa. Ila kikubwa ni kuwa Wabelgiji wameisusa Tz kutokana na issue ya Lissu. Hapa Jiwe kamuonea balozi wake!
Hivi ikitokea Kapilimba kapelekwa Ubelijiji...unaweza ukafikiria nini hapo..au kumpa Mh Lissu ushauri gani.
 
Hivi ikitokea Kapilimba kapelekwa Ubelijiji...unaweza ukafikiria nini hapo..au kumpa Mh Lissu ushauri gani.

1.Atatakiwa awe mwangalifu sana ktk maisha yake yote ya kila siku, awe NA body guards NA madaktari WA kupima vyakula vyake kabla hajala.
2.Asiyende ktk Ofisi za Ubalozi WA Tz au WA nchi nyingine yoyote ile bila ulinzi mkali ili yasije yakamkuta yaliyomkuta Mwandishi WA Habari Jamal Kashoghy.

Ikiwa haya yote yatashindikana, then:-
3.Atume maombi maalumu na kuushawishi Umoja WA Ulaya (European Union, EU) ili ukatae Kumpokea huyo Balozi aliyeteuliwa kuiwakilisha Tz huko barani Ulaya. Balozi asikubakiwe kuingia wala asipewe Viza ya kuingia wala kuishi ktk nchi yoyote ile barani Ulaya.
 
Hivi ikitokea Kapilimba kapelekwa Ubelijiji...unaweza ukafikiria nini hapo..au kumpa Mh Lissu ushauri gani.
Wapo walio wakali zaidi ya huyu wako tayari eneo la tukio---------------------usiwatishe watu
 
Kila siku teuzi tu tumeshachoka!!

Yaani uteuzi unatangazwa live, alafu Bunge liko gizani na wajinga wanaamini huu ndio uongozi unaotufaa!!
Mbunge ulishiriki kumteua na ka hatimizi wajibu wake msubiri jimboni umkabe na maswali na mwisho wa siku wapiga kura wenzio watakuelewa na kumtumbua kwa kura.

Rais acha atimize wajibu wake kama nahodha na chombo chake kisiende mrama
 
Back
Top Bottom