MsemajiUkweli
JF-Expert Member
- Jul 5, 2012
- 13,171
- 23,991
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Misri, Abdel Fattah El Sisi kabla ya kuanza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao .
Rais John Pombe Magufuli na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi wakitoka kwenye chumba cha mazungumzo baada ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za AU mjini Addis Ababa Ethiopia.
Rais John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao rasmi katika moja ya Ofisi za AU mjini Addis Ababa Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kuwasili kwa ajili ya mazungumzo katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma mara baada ya kumaliza mazungumzo yao
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn wakati akitoka kwenye mkutano wa AU mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.