johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 94,035
- 164,307
Rais John Magufuli alitoa mpya wakati akimueleza Mama Salma Kikwete ambaye ni mke wa Rais mstaafu , Jakaya Kikwete kwa kusema kuwa siyo tu ni mchapakazi hodari bali pia ni mzuri wa muonekano.
Magufuli aliyasema hayo katika namna iliyoashiria utani wakati akihutubia umati wa wananchi waliojitokeza kumsikiliza kwenye uwanja wa Ilulu mjini Lindi, ikiwa ni katika sehemu ya ziara yake ya siku nne kwenye mikoa ya Lindi na Mtwara.
"Mama Salma Kikwete si uchapakazi tu bali pia ni mzuri jamani....kwani uongo?" Rais Magufuli alihoji wananchi na kuibua shangwe kabla ya kuongeza: "Najua nayasema haya kwa kuwa mzee JK hayupo, vinginevyo hata ngumi ningerushiwa..." alisema na kuibua kicheko zaidi ikiwamo kutoka kwa Mama Salma aliyekuwapo uwanjani hapo.
Chanzo: Nipashe