Dunia nzima inajua kuwa Tanzania mikononi mwako haina Demokrasia ,umefanya kila unaloweza kuua Demokrasia na Uhuru wa Habari.
Mimi hapa nakuandikia nikiwa natumia ID fake ili kulinda usalama wangu.
Lakini jukwaa hili la Jamiiforums nalotumia linaandamwa na serikali ili litoe siri au majina halisi ya wakosoaji wa serikali humu, na hadi sasa Kesi ipo mahakamani.
Wewe ni mkuu wa nchi, mfalme wa taifa la Tanzania, kutamka kwako hadharani kwamba eti Tanzania ina Demokrasia kubwa, ni kuwadhihaki watu wako uliowanyima haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka.
Nikueleze wazi kwamba tangu umeingia madarakani umesahau kabisa kuwa maisha yana kesho, leo hii wewe ni Rais ila siku zijazo hutakuwa Rais tena, na hawa wanaokupa sifa kila siku hata ambako hustahili watakugeuka wote na kuanza kumsifia Rais atakayekuwa madarakani.
Mh Rais, hofu yako iko wapi hasa? mbona kuna sehemu unafanya vizuri kiasi cha kukubalika na watu automatically? Kwanini umekubali kuchoreshwa kiasi hicho?
Yaani wewe ni Binadamu, una mapungufu mengi tu sasa iweje ukubali kusifiwa kiasi hicho na wanaokukosoa waonekane wabaya?
Mwl Nyerere aliulizwa swali na mwandishi wa BBC enzi za uhai wake akiwa Rais mwaka 1983.
"Why are you getting ready to retire? "
Mwl Nyerere alijibu.
"Because I need to create a fresh legacy of mine and my country as well ".
Leo hii watanzania tunajivunia Mwl Nyerere, hata mabeberu walimpenda na kumwogopa Mwl.
Nyerere aliwahi kumshauri Kaunda na kumwambia.
"Mzee mwenzangu, achia madaraka kabla watu hawajakuchoka ".
Kaunda alikuwa Kiburi, hakuwa na hekima, hakusikiliza ushauri wa Mwl, matokeo yake alikuja kuondoka madarakani kwa aibu kubwa mno.
Wazambia hawana Rais wa kujivunia Kama sisi watanzania tunavyojivunia kwa Nyerere.
Ni kwa sababu Kaunda hakuacha Legacy nzuri.
Kikwete ameondoka madarakani na kuacha Legacy ya kuheshimu mfumo wa vyama vingi na Demokrasia.
Miaka ya nyuma Kati ya 1980 au 1984 Tanzania ilikumbwa na balaa la njaa, Nyerere hakuwaambia watanza nia kwamba ni wavivu na hawalimi watakufa njaa...
Alikimbilia Marekani kuomba msaada wa Chakula kwa ajili ya watu wake, msaada ulikuja haraka na malori yakaanza kusambaza Chakula nchi nzima, kila kaya iligawiwa Chakula cha kutosha, Mahindi ya njano, Burga (American meal) Maziwa ya unga pamoja na mafuta ya kupikia.
Wananchi walikula na kusaza hadi balaa la njaa lilipoisha .
Je wewe utaacha Legacy gani kwa taifa lako?
Rejea ya Tetemeko la Bukoba, MV Nyerere, Wafanyakazi, Demokrasia na Uhuru wa Habari, Uchumi wa nchi na anguko kuu la Mihimili ya Serikali.
=====
Maoni ya Wadau