Rais Magufuli acha dhihaka

nikipitia nyuzi za jf enzi za mh. Kikwete na za sasa napata wakati mgumu. sijui wale wachangiaji wa enzi zile walihama jukwaa au ni hawa hawa waliobadili id!!!!!

hivi watanzania tunataka nini?
 
Kushauri tushauri kila mmoja kwa mtazamo wake na kwa mapenzi mema ya nchi yetu. Lakini Mimi binafsi naamini kwa dhati kwambà utawala wa awamu ya tano ni mpango wa Mungu kwa nchi yetu. Awamu hii imetufundisha mambo. Kinyume na wengi walivyoamini viongozi aina ya nyerere ni nadra sana kupatikana. Walio wengi ni watu wa kawaida sana na wakati mwingine hata ni below average or even worse. Awamu hii imetudhihirishia kuwa kumbe kwa katiba tuliyonayo sisi raia tukishachagua viongozi tunageuka kuwa watwana (subjects) wa kuwatumikia wao na hatuna njia yoyote ya kuwasahihisha wanapopotoka mbali na kusubiri uchaguzi mwingine ambao hata hivyo wanaweza kushinda bila kupata kura zetu. Taasisi zetu za utawala bora hazina nguvu kwa sababu zimedhibitiwa na hao hao wanasiasa. Utawala huu umewafanya hata baadhi ya viongozi wastaafu wa nchi hii kuanza kuonyesha waziwazi kuwa hawana amani tena na jinsi tunavyoenenda kisiasa kama nchi.
 
Unaongelea Mwl Nyerere yupi? Mbona mlimwita haambiliki leo hii nyie tena ndio mmekuwa mstari wa mbele kujitamba kwamba mlikuwa mnamkubali. Bado hatujasahau jinsi mlivyokuwa mnamkebehi leo hii baada ya kufa ndio mnamwona alikuwa mzuri? Hata JPM akiondoka baada ya muda wake mtakuja na kusema bora JPM angekuwepo, ni binadamu ambao hamna shukrani mmejaa usaliti mioyoni mwenu. Hata muda haujapita kila uchwao mlimsimanga JK ohhh anatembea kama Vasco da Gama etc leo mnamlilia kwa sababu alikuwa hana uwezo wa kuongoza na mlifanya Tanzania dangulo la wauza unga na wezi wa meno ya Tembo nk.

Watanzania wengi hawana shukrani tu pamoja na wewe. Kwanza hufahamu maana ya Demokrasi kwa sababu 1. Demokrasi sio kwa sababu wewe binafsi na kikundi chako cha vikaragosi mna chuki binafsi then mnakuja na ngonjera kusema kwamba hakuna demokrasi. Kwa faida yako na makasuku wenzako tafsri ya Demokrasi hapa chini:

''Democracy is a form of government in which the people have the authority to choose their governing legislation. Who people are and how authority is shared among them are core issues for democratic development and constitution. Some cornerstones of these issues are freedom of assembly and speech, inclusiveness and equality, membership, consent, voting, right to life and minority rights.''

Kama lugha imekupiga chenga shauri yako. Sasa kama wewe umekwazika sema ni lipi hapo ambalo unasema limekukwaza kwa ushahidi sio kuleta viroja kwenye hoja muhimu. Majungu peleka kwa makasuku wenzako.
Hiyo hiyo definition ya democracy ndio imeshakiukwa ktk nchi hii kwa siku nyingi.

Hiyo freedom of speech, freedom of assembly ziko wapi. Haki hiyo ya kupiga kura iko wapi au hiyo the right to life iko wapi wakati kuna wengine hadi leo hawajulikani waliko.

Kama huwezi kuyaona hayo basi wewe ndio kasuku wa ukweli yule atakuwa feki.
 
Ole,
Ole huwa unanichekesha vibaya, naona huwa unataka ushahidi, huwa sikuelewi unataka ushahidi gani kuwa demokrasia yetu inabakwa hivi sasa. Mtu akipitia hoja zako anaweza kudhani una hoja za msingi, lakini ukiangalia ni mtu uliyeshiba propaganda za kizee, kwa maneno marahisi uko ndani ya box.
 
"Mzee mwenzangu, achia madaraka kabla watu hawajakuchoka "

Hii kuachia madaraka bado mwaka 1 tusubiri sanduku la kura ikiashindikana basi hiyo 2025 ataondoka kwa mujibu kwa katiba...ipawapo atatumia njia nyingine kubaki madarakani ndo tutazungumzia mfano ya hao akina Mugabe , Gadafi na wengineo huyu hajamaliza muda tusubiri muda ufike
 
Nyinyi mashabiki wake Rais, munamupenda sana sana na pia kumuongelea na kumuandika.. mbona hamuja ongelea kiongozi wetu wa nchini.. kiongozi wa upinzani Bungeni!! Hivi yupo pouwa?
anakanyaga katiba yao huyo KUB? usichanganye minara
 
Ni Nchi zile zile na watu wale Mara zote wasema Tz hakuna democrasia, sasa hiyo ambayo imeondolewa ilitangazwa mwaka Au lini kuwepo nchin
 
Back
Top Bottom