Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Katika hafla ya kuwaapisha Mawaziri wawili na Mabalozi watatu aliowateuwa hivi karibuni Ikulu Dar es Salaam, Rais Dr. John Pombe Magufuli ameanika sababu ya kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani.
Rais Magufuli ameonyesha na kukiri kuumizwa na 'ubovu' wa mkataba uliosainiwa ambao ulitanguliwa na usiri mkubwa pamoja na kila dalili za rushwa na kuhongwa kwa wahusika. Wahusika walikuwa wakipokea fedha za kimarekani wakati wa vikao vyao n hata kulipiwa malazi yao.
Rais Magufuli amesikitishwa na kutokuwa na taarifa ya mkataba huo tangu mwanzo hadi alipoombwa kuidhinisha jambo ambalo hakuwa akilifahamu na ambalo halikuwahi kuwasilishwa kwenye kikao chochote cha Baraza la Mawaziri. Mkataba husika una thamani ya zaidi ya shilingi trilioni moja.
Katika kuweka sawa jambo hilo la kimkataba, Rais Magufuli amemkabidhi nyaraka maalum Waziri wa Mambo ya Ndani George Simbachawene ili aweze kuanzia kufanya kazi huku Rais Magufuli akiukataa mkataba uliosainiwa na utekelezaji wake. Waziri ameagizwa kuona namba ya kuondokana na mkataba huo.
Rais Magufuli amesema kuwa Naibu Waziri hakuwa anajua kwa undani kuhusu jambo hilo ingawa alikuwa akipata madokezo na alitakiwa kutoa taarifa juu ya kilichomo kwenye madokezo hayo mapema. Rais akasema kuwa Naibu Karibu Mkuu wa Mambo ya Ndani najua jambo hilo kuanzia mwanzo hadi mwisho wake.
Kimsingi, nipo pamoja na Rais wangu Magufuli kwenye vita dhidi ya rushwa na ufisadi. Mambo haya yamelitesa kwa muda mrefu sana taifa letu hasa kwenye kuzalisha kesi za hovyohovyo na zenye kuligharimu pakubwa taifa letu ndani na nje ta nchi yetu. Viva Magufuli!