ng'ombo
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 418
- 619
UTHUBUTU wa kusema tunaibiwa, tumekuwa nao miaka nenda rudi.
Jakaya Mrisho Kikwete, alieleza hilo miaka 10 iliyopita. Ameendelea kulisema hadi anaondoka madarakani.
Lakini hakuna hatua zilizochukuliwa. Aliishia kuunda tume na kamati - Kamati ya Bomani na Lau Masha.
Hata huyu aliyepo sasa ataishia na uundaji wa Kamati. Hawezi kuchukua hatua.
Sababu ni mbili:
1. Mikataba hii imefungwa kupitia sheria za madini zilizopo. Ni sheria halali.
Zimepitishwa na Bunge baada ya kuletwa bungeni na serikali kwa idhini ya rais na baraza lake la mawaziri.
Anyelalamikia sheria hizi leo -John Pombe Magufuli - alikuwamo bungeni na alikuwa waziri.
Ni kupitia sheria hizi, makampuni ya madini yamepewa mamlaka ya kuvuna kila kitu na kupeleka kwao na kutuachia mrahaba wa asilimia tatu.
Hivyo ukiliangalia jambo hili kiundani unaweza kugundua kuwa hakuna wizi.
Kinachobebwa kupelekwa nje, kinatolewa kihalali kabisa kwa mujibu wa sheria. Labda tunaweza kusema, kuna unyonyaji.
Kwamba tunachopewa hakilingani na kinavunwa. Na huu ni wimbo wetu wa miaka mingi.
Rejea makala za kadhaa kwenye magazeti.
Kwa mfano, Manyerere Jacton aliandika kwenye RAI - "Balozi Mpungwe, mwananchi au muuza nchi?"
Alikuwa anajadili ujambazi kwenye mugodi ya Milerani.
MwanaHALISI liliripoti, "Mkapa na ujambazi wa Kiwira."
2. Mikataba yote ya madini ilisainiwa baada ya baraza la mawaziri kuidhinisha. Hakuna aliyesaini bila kutumwa.
Ukiamua kwenda mahakamani kushitaki waliosaini, watajitetea na kusema walitumwa na rais.
Rejea kesi ya Prof. Mahalu ambapo magazeti yaliandika kwa mapana kuwa "Mahalu ni fisadi." Lakini mahakama imemsafisha.
Aidha, huwezi kubadilisha sheria katikati ya mkataba na ukataka makampuni ya madini yalipe kupitia sheria mpya ulioleta.
Sheria tutakazotunga zitawahusu wawekezaji wapya; na au wale waliopo wakati wa kuongeza mikataba yao, baada ya mikataba ya awali kumalizika.
Kwa muktadha huo, tukatae utapeli wa kuambiwa Magufuli amethubutu. Hakuna alichothubutu. Hakipo na hakitakuwapo.
Source: Saed Kubeba - Dodoma