Rais Mafuli, Kajitoa Sadaka Kwa Ajili ya Maskini/Wanyonge

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,168
1,071
Aina za Sadaka
Mtoa Sadaka
Mpokea sadaka
Mfaidika na sadaka

Nimekuwa nikifuatilia sana kauli nzito zenye maudhui lukuki ya uhalisia na dira ya utendaji za Mh. Rais JPM katika vita ya kuwakomboa wanyonge,maskini,wanyonywaji,wakandamizwaji,wenye njaa ya haki,wenye kiu ya elimu,walio magerezani kiufahamu na walio uchi kimatumaini.Inahitaji sikio la nne kumeng'enyua maono yake yasioyumba kisiasa/kiuchumi na kijamii.

Amethubutu kufanya maamuzi magumu sana ndani ya kipindi kifupi cha uongozi wake huku akitoa kauli ya kujitoa sadaka kwa ajili ya maskini/wanyonge wa Taifa Tanzania..waongeaji wenye kusikika hawawezi kuongea kwenye mazuri sababu ya fikra pinzani kiitikadi na makundi maslahi kisiasa/kiuchumi na kijamii...Kwa miaka mingi tulilalama juu ya upole,ukimya,udhaifu ktk utamkaji/utendaji/uroho/upofu wa uthubutu/ufanyaji maamuzi magumu kwa mustakabari wa nchi/taifa ama kwa faida ya wengi na vizazi vijavyo...

La utumbuaji /Sukari na mengineo yanayokuja ni viashiria tosha vya msigano wa maslahi kati ya wanaoguswa ama kuathiriwa na maamuzi ya serikali dhidi ya watendaji wa serikali..Wafaidika wa mfumo mbovu wa kulindana na waliokuwa wakiwalinda si tu yamkini wanahaha kujizuia na tsunami la kuguswa na maamuzi magumu lakini pia yamkini wanapanga mikakati ya kujinusuru/kujitetea/kufunika uozo/kupambana na mfumo mpya unaotishia uhai wa michakato ya udhalimu/wizi/ufisadi na umalaya wa rasilimali.

Mtikisiko ni mkubwa kila kona,hofu ya nidhamu imelejea kila kona iliojaa udhalimu na kujisahau..ulaji wa kuzingatia urefu wa kamba unatoweka kila kukicha,wazee wa 10% na cha juu wanavikimbia vivuri vyao na vimemo vya walioitwa wakubwa vimetoweka kwenye madokezo...Hakuna mpinzani anaeweza kupongeza zuri la mpinzani ila mpinzani wa kukosoa baya hakosekani...ndo siasa..

JPM Amejitoa sadaka..yupo tayari kufa/kulaumiwa/kuumizwa/kuteswa/kutolala/kubatizwa majina yote ...kwa faida ya maendeleo/Ustawi ya maskini wa mijini na vijijini..maskini wa leo na wa kesho..
 
Back
Top Bottom