Rais kuingilia taasisi zingine ni kukosa leadership skills?!!

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,820
117,375
Wakuu mtusaidie hasa wale waliosoma Management and Leadership,na wote wenye uzoefu katika uongozi mtupe miongozo

Nchi hii ina taasisi nyingi katika mihimili mikuu mitatu!Vilevile muhimili wa Executive unaundwa na taasisi nyingi sana,ambapo zingine zipo kikatiba,kisheria,kikanuni na hata kimuundo!Taasisi hizi zimepewa mamlaka na majukumu katika kutekeleza adhma ya kuundwa kwake!

Moja kati ya sifa za nchi imara na madhubuti ni uimara wa taasisi zake katika maamuzi na utendaji. Tazama mfano mzuri Marekani,Rais Trump is not everything!Huko chini kuna taasisi imara sana,kidampa kama mimi tu anaweza kuzuia Trump kutekeleza ahadi yake ya kihuni-huni aliyoitoa huko kwenye kampeni!

Sasa hapa kwetu naona hali ni tofauti kabisa!Katika muhimili wa serikali ni taasisi chache sana huru mfano CAG na ofisi yake,at least naona uhuru fulani hivi! Zilizobaki ni majanga!

Mifano ni mingi sana,lakini hoja hapa ni kwamba ili kuleta maendeleo ya kweli ni lazima taasisi ziwe huru katika maamuzi!Sheria zimeweka utaratibu mzuri wa kupitisha maamuzi kuanzia chini kwenda juu ana juu kwenda chini!Kama rais anayo nafasi katika mchakato wa kupitisha maamuzi basi ashiriki huko na sio kuvamia tu na kuleta mkanganyiko na ugumu katika kutekeleza

Vilevile masuala ambayo rais anadhani ni muhimu ajadiliane kwanza na taasisi husika na wataalamu wake na kupanga mipango mizuri ya kutekeleza kabla ya kutoa tamko

Hii staili ya uongozi awamu hii naona haitakuwa na msaada sana.Naona kama mgonjwa anapigwa sana "ndulele" bila kujali anaumwa nini!

Rais Magufuli ukiimarisha na kuzipa uhuru taasisi ndio utakuwa umeweka msingi imara sana wa Tanzania ya leo na kesho hata usipokuwepo! Zimamoto zinaziendelea zina maisha mafupi sana,siku ukizima ghafla na zenyewe zimeishia hapo.Utakuwa kama vile hakukuwahi kuwa na rais anaitwa Magufuli

Haiwezekani wewe ndio rais, wewe ndiye IGP, wewe ndiye BASATA, wewe huyo huyo ni Waziri wa Afya, Miundombinu na Ulinzi, wewe ndiye CAG, TRA na TAKUKURU ni wewe

Miaka michache kabla Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama aliitembelea Afrika, Tanzania ikiwemo. Nakumbuka alisema Afrika haina tatizo la kukosa watu shupavu (Strong people) bali ina tatizo la kukosa taasisi imara (Lack of strong institutions). Akasema viongozi wengi wa Kiafrika wanakazana kujijengea umaarufu wao binafsi na hawajishughulishi kujenga taasisi imara. Tatizo hili limepelekea kila anayeingia madarakani anaanza upya. Hakuna mwendelezo wa agenda za kujenga nchi kitaasisi. Hili ndilo tatizo tunalokumbana nalo sasa Tanzania. Hebu fikiri jambo la ajira ya madaktari kwenye utumishi wa umma kwenye sekta ya afya. Waziri wa afya hajui hata ni kwa nini Rais kaagiza kuajiriwa nchini kwa madaktari waliokuwa waende Kenya. Anasema
anachokijua yeye ni kwamba wizara haina fedha za kuajiri lakini Rais kaagiza waajiriwe. Waziri anakiri wazi kwamba ni Rais pekee ndiye anayejua hao madaktari watalipwaje. Ina maana hapo hakuna utendaji wa kitaasisi bali wa mtu mmoja. Tunajua bunge hupitisha bajeti ya ofisi ya Rais na bajeti ya wizara ya afya ambayo pamoja na mambo mengine hutumika kuwalipa madaktari na watumishi wengine wa wizara mishahara na malipo mengine wanayostahili. Kwa hiyo waziri atakuwa anawaongoza na kuwasimamia madaktari ambao wanawajibika kwa Rais anayewalipa mshahara. Hapa hatujengi taasisi imara bali tunamjenga mtu mmoja. Huyu akimaliza muda wake anayekuja anakuta taasisi zipo hoi, na anaanza upya. Naye, kwa tabia za viongozi wa kiafrika ataanza kujijenga yeye. Ndiyo maana nchi zetu hizi za dunia ya tatu zinaendelea kuwa kichekesho kila kukicha. Ndiyo maana Bashite kila akisimama kuongea lazima aanze kumsifia 'mzee' wake. Maana ndicho mzee anachokipenda.

Kiutumishi na kiutendaji waziri ndiye msimamizi mkuu wa raslimali vitu na watu, sera na mipango mbalimbali ya wizara husika. Ndiye anayewajibika kuisemea na kujibia wizara, ikiwemo namna watumishi wake wanavyoajiriwa na stahili zao za kiutumishi. Lakini watanzania tujiulize, kwanini huyu ndugu yetu anataka awe yeye tu kwa kila kitu? Hata baada ya kuamuru hao madaktari waajiriwe kuna tatizo gani kumwambia wazi waziri wake namna hawa madaktari watakavyolipwa? Kwanini amfiche waziri wake?
 
Madudu kama ya NIDA mnataka rais asiingilie kati kweli? Hiyo mikataba ya hovyo ya mlimani city tena iliyoratibiwa na vipanga nayo atizame tu, hapana.

Kaingilia TBA tumeona 10b zimetosha kujenga magorofa 20, bado mnasema tu, hapana akusanye cheki zote azifungie kabatini awe anatoa anapojiridhisha kuwa hela inaenda kwa walengwa.
hata yeye ni jipu tu huko wizara ya ujenzi alipokua ameacha miradi kibao ya kifisadi
 
Madudu kama ya NIDA mnataka rais asiingilie kati kweli? Hiyo mikataba ya hovyo ya mlimani city tena iliyoratibiwa na vipanga nayo atizame tu, hapana.

Kaingilia TBA tumeona 10b zimetosha kujenga magorofa 20, bado mnasema tu, hapana akusanye cheki zote azifungie kabatini awe anatoa anapojiridhisha kuwa hela inaenda kwa walengwa.
Rais haishi milele,assume Mungu kampenda zaidi within a year,tutaanza upya?
 
Kaingilia TBA tumeona 10b zimetosha kujenga magorofa 20, bado mnasema tu, hapana akusanye cheki zote azifungie kabatini awe anatoa anapojiridhisha kuwa hela inaenda kwa walengwa.
Hebu nenda uwaulize hao TBA gharama halisi kama watakwambia kwamba wamejenga kweli kwa 10 billion! moto unaowawakia hawana hamu!!
 
Shida anataka aonekane yeye tu kwenye MEDIA "FENT FONT"

Raisi ndo anayeamua na kutoa vibali vya ajira, Wizara ya utumishi ipo na wafanyakazi zaidi ya 1000 plus waziri, bunge linalopanga bajeti na matumizi ya serikali lipo, lakini mwenye jukumu la kuamua kuajiri ni Raisi. This is one man show
 
Rais siyo muamuzi wa nani aajiriwe wala idara gani iajiri watu wangapi,ni IDARA au TAASISI husika kulingana na uhitaji.Kwa sasa RAIS anataka kuuza sura zaidi.Hakuna utendaji wa kitaaluma zaidi ya kutafuta kiki.

Hivi tunaingia mwaka wa Tatu hakuna ajira za madaktari wakati tunajua hali za hospitali zetu,madaktari wapo nyumbani wagonjwa wanakosa service.uko tayari kupeleka Madaktari kwa jirani wakati nyumbani kwako ni shida,naona tuna shida ya uongozi,hatuna kiongozi tuna kitu kingine kabisa hapo
 
Wakuu mtusaidie hasa wale waliosoma Management and Leadership,na wote wenye uzoefu katika uongozi mtupe miongozo

Nchi hii ina taasisi nyingi katika mihimili mikuu mitatu!Vilevile muhimili wa Executive unaundwa na taasisi nyingi sana,ambapo zingine zipo kikatiba,kisheria,kikanuni na hata kimuundo!Taasisi hizi zimepewa mamlaka na majukumu katika kutekeleza adhma ya kuundwa kwake!

Moja kati ya sifa za nchi imara na madhubuti ni uimara wa taasisi zake katika maamuzi na utendaji. Tazama mfano mzuri Marekani,Rais Trump is not everything!Huko chini kuna taasisi imara sana,kidampa kama mimi tu anaweza kuzuia Trump kutekeleza ahadi yake ya kihuni-huni aliyoitoa huko kwenye kampeni!

Sasa hapa kwetu naona hali ni tofauti kabisa!Katika muhimili wa serikali ni taasisi chache sana huru mfano CAG na ofisi yake,at least naona uhuru fulani hivi! Zilizobaki ni majanga!

Mifano ni mingi sana,lakini hoja hapa ni kwamba ili kuleta maendeleo ya kweli ni lazima taasisi ziwe huru katika maamuzi!Sheria zimeweka utaratibu mzuri wa kupitisha maamuzi kuanzia chini kwenda juu ana juu kwenda chini!Kama rais anayo nafasi katika mchakato wa kupitisha maamuzi basi ashiriki huko na sio kuvamia tu na kuleta mkanganyiko na ugumu katika kutekeleza

Vilevile masuala ambayo rais anadhani ni muhimu ajadiliane kwanza na taasisi husika na wataalamu wake na kupanga mipango mizuri ya kutekeleza kabla ya kutoa tamko

Hii staili ya uongozi awamu hii naona haitakuwa na msaada sana.Naona kama mgonjwa anapigwa sana "ndulele" bila kujali anaumwa nini!

Rais Magufuli ukiimarisha na kuzipa uhuru taasisi ndio utakuwa umeweka msingi imara sana wa Tanzania ya leo na kesho hata usipokuwepo! Zimamoto zinaziendelea zina maisha mafupi sana,siku ukizima ghafla na zenyewe zimeishia hapo.Utakuwa kama vile hakukuwahi kuwa na rais anaitwa Maguguli
Hizo taasisi zilizokuwa Huru kwa miongo mitatu/ minne Mbona ndio zimetufikisha hapa, TTCL kuuzwa , tpa na manunuzi mabovu, Mikopo hewa wafanyakazi hewa, mishahara hewa, inflation ya cost of purchases of goods and services yaani upuuzi wa kila aina , sasa wewe unataka huyu wa sasa aendele kuachia Hayo mambo. Tulikuwa tumefikia Hali mbaya hivyo tulikuwa tunahitaji drastic measures amasivyo ingetuchukua muda mrefu
 
Miaka michache kabla Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama aliitembelea Afrika, Tanzania ikiwemo. Nakumbuka alisema Afrika haina tatizo la kukosa watu shupavu (Strong people) bali ina tatizo la kukosa taasisi imara (Lack of strong institutions). Akasema viongozi wengi wa Kiafrika wanakazana kujijengea umaarufu wao binafsi na hawajishughulishi kujenga taasisi imara. Tatizo hili limepelekea kila anayeingia madarakani anaanza upya. Hakuna mwendelezo wa agenda za kujenga nchi kitaasisi. Hili ndilo tatizo tunalokumbana nalo sasa Tanzania. Hebu fikiri jambo la ajira ya madaktari kwenye utumishi wa umma kwenye sekta ya afya. Waziri wa afya hajui hata ni kwa nini Rais kaagiza kuajiriwa nchini kwa madaktari waliokuwa waende Kenya. Anasema
anachokijua yeye ni kwamba wizara haina fedha za kuajiri lakini Rais kaagiza waajiriwe. Waziri anakiri wazi kwamba ni Rais pekee ndiye anayejua hao madaktari watalipwaje. Ina maana hapo hakuna utendaji wa kitaasisi bali wa mtu mmoja. Tunajua bunge hupitisha bajeti ya ofisi ya Rais na bajeti ya wizara ya afya ambayo pamoja na mambo mengine hutumika kuwalipa madaktari na watumishi wengine wa wizara mishahara na malipo mengine wanayostahili. Kwa hiyo waziri atakuwa anawaongoza na kuwasimamia madaktari ambao wanawajibika kwa Rais anayewalipa mshahara. Hapa hatujengi taasisi imara bali tunamjenga mtu mmoja. Huyu akimaliza muda wake anayekuja anakuta taasisi zipo hoi, na anaanza upya. Naye, kwa tabia za viongozi wa kiafrika ataanza kujijinga yeye. Ndiyo maana nchi zetu hizi za dunia ya tatu zinaendelea kuwa kichekesho kila kukicha. Ndiyo maana Bashite kila akisimama kuongea lazima aanze kumsifia 'mzee' wake. Maana ndicho mzee anachokipenda.
 
Tumsaidie Rais kufanya kazi kuliko kulaumu kila kitu na isitoshe kila mtu ana mapungufu yake halafu watanzania tulilizwa sana na wajanjawajanja acheni airekebishe nchi.
 
Back
Top Bottom