Rais Kikwete safarini UK na China

Rais Kikwete safarini UK na China

safiri baba safiri tu usiwe na wasiwasi maendeleo tunayaona waache wenye akili iliingia mdeli waseme kitu wasichokijua
 
Kenya,Rwanda,Uganda,S.Sudan, wanajenga reli, bomba la mafuta,na barabara pamoja kuwaunganisha kibiashara Kikwete hana habari kutwa kiguu na njia kutembeza bakuli la marehemu Matonya, kwa utawala huu TZ itabakia masikini milele. Hana mshawasha kujua mahindi yaliyo wadodea wakulima nchini yataenda wapi ilhali soko lipo S.Sudan. pathetic
 
Watu wanatafuta pesa za kampeni ,mkiuliza mtaambiwa safari za raisi zina tija kwa taifa .
 
Ndo tujifunze sasa, mambo ya kuchagua Rais eti kisa ana sura ya kike au eti ni kijana mwenzetu hapana tena!!!

Mkuu labda tuwe na utaratibu wa kuangalia hobbies za viongozi kwenye cv zao kabla ya kuwachagua.. Nasikia ya Jk kwenye Hobbies ameandika anapenda kusafiri..
 
Maisha yenyewe mafupi niacheni mi nile ujana!!!
Wana niita popoo nakesha nakula ujana!!!
Kujirusha daily sina weekend, nakula ujana!!!!
 
Acha utani kasafiri tena sasa hizo safari kwanini asimalize zote kbs.Akimaliza UK aende China akitoka aende na Siera Lione na Liberia kbs.Daaah huyu rais wangu namsamehe bure tuu sababu nadhani ni kosa langu pia kuchagua vimeo sirudiii tena.
 
Sina hakika akishatoka UK anaunganisha China au anarudi kisha china

Nimeona kwenye Africa news 24

Naona hizi ni farewell trip tena maana kabakisha miezi 12 tuu

utafiti wa siku za nyuma ulionyesha kwamba kiongozi pekee aliyemzidi jk kwa kusafiri duniani alikuwa MKE WA CLINTON ( AMBAYE SERA YA NCHI YAKE INASEMA NI LAZIMA WAZIRI WA MAMBO YA NJE AWEPO POPOTE PENYE MASLAHI YA USA ) , LAKINI KWA SASA BILA SHAKA JK AMESHIKA USUKANI , MAANA HILLARY ALISHASTAAFU .
 
"Msafiri" anaenda kupiga kambi ya miezi mingapi huko?
 
Kila la kheri rais wetu mtukufu na mpedwa sana kuliko wote.
Lakini safari hii jitahidi upate jibu la kwa nini Tanzania ni masikini na utueleze katika hotuba yako ya mwisho wa mwezi.
 
Wasanii wetu wa Bongo Movie wasingekuwa makuwadi wa itikadi za ki-CCM, wangetutolea picha moja kamambe yenye title: PRESIDENT: the da GAMA! (of course, maudhui yangewasilishwa kwa Kiswahili). Hii ingekuwa kibwagizo cha da Gama kuhitimisha mihula yake miwili.
 
Hata hivyo hatushangai kwa vile kazoea kuishi kama popo

dah, naomba maisha marefu kidogo ili nimshuhudue huyu vasco da gama kama atayaweza maisha ya kijijini kwake msoge, jinsi alivyozoea kwenda mbele kila siku.
 
Back
Top Bottom