Rais Kikwete ni extra ordinary

Rais Kikwete ni extra ordinary

jina lako tuuu(MALISA) linatosha kumjulisha mtu kuhusu andiko lako kabla hata hajalisoma. vipi jamhuri ya kaskazini bado mnaendelea na mikakati ya kuiunda???
risala ya kikwete ni hotuba bora kabisa kwa vigezo vyoote na amewazima vibaya nyie wajinga mnaotaka mwanya ili mumsakame kuwa ametoa ahadi hewa. sisi tunasubiri chochote kitakachoamuliwa na wao tunaenda pamoja

Mbona kuna watu katika chama chake hawakuta mchakato huu wa katiba mpya lakini yeye alishikilia bango ? au msimamo upi mnaoutaka? kuhusu hatua ya upigaji kura alisema jambo hilo linahitaji kufanyiwa mabadiliko ya sharia iliyounda tume ya mabadiliko ya katiba na BMK.alisema UKAWA walismahuri kuvunja BMK wakati hao hao ndiowalipendekeza Rais asiwe na mamlaka ya kuingilia BMK au tume ya jaji warioba.
 
Kikwete ni kigeugeu...

mtu atakaemuamini kikwete ktk maneno yake, atakuwa ni mtu wa ajabu sana....

Atakuwa anafuata nyayo za UKAWA maana kila kukicha wanakuwa na madai mapya, ebu ona toka wametoka mjengoni madai mangapi wameyatoa! wajumbe waliowengi wana matusi, kundi la 201 wamepewa rushwa na pinda, ccm wanarasimu yao nyingine inayojadiliwa,BMK livunjwe kwa sababu pesa za wananchi ziznaliwa bure,BMK halikuwa na uhalali wa kisheria ,.......na yanazidi kutolewa madai mapya kila kukicha je wana msimamo hawa?
 
Kwani sisi wananchi tuna shida zaidi ya kuona maisha bora kwa kila mTZ alivyoahidi 2005? Waje na katiba sijui ya wapi, apangue baraza la mawaziri mwananchi anachotaka ni kuona mabadiliko chanya katika maisha yake elimu afya miundo mbinu na makazi viboreke tu basi na kinyume na hapo tunawapa upinzani hii nchi tuone na wao watatupeleka upande gani.
 
KIKWETE baba lao, kishawanyamazisha tayari, mliobaki ni mavuvuzela tu. Wengine tumeshamuelewa tunasubiri kumwaga kura za ndiyo kuikubali Katiba iliyopendekezwa

Craaaap!
 
KIKWETE baba lao, kishawanyamazisha tayari, mliobaki ni mavuvuzela tu. Wengine tumeshamuelewa tunasubiri kumwaga kura za ndiyo kuikubali Katiba iliyopendekezwa

Kama katiba hii ni ya kupigiwa kura ya ndiyo basi hakuna haja ya kura hiyo kupigwa maana matokeo tayari yanajulikana. tutakuwa tunapoteza muda tu.
 
Kwa mtazamo huu nina kuheshimu na ninakupenda; Uishi na udhihirishe hivyo.Wewe umeanza na mimi niko nawe mpaka ukamilifu wa dahari
 
Malisa Godlisten, asante kwa uchambuzi makini umejitahidi na umeweza.

Ila kubwa ambalo umezunguka sana katika kulibainisha ni kwamba Rais wetu kwa hakika kabisa anasumbuliwa na kikubwa ambacho kwa kweli hawezi kukiepuka kwasababu ni asili tangu kuzaliwa kwake hivyo hata aende shule gani ya kujifunza ujasiri hawezi kufaulu tatizo hili linalomkabili. Tatizo kubwa kwa Presidentt wetu ni UDHAIFU,DHAIFU na UDHAIFU, hakuna kingine

Mtu ambaye haelewi anahitaji nini kwa wakati gani na kuhitaji kila kitu kwa wakati wote!! Huyo kwa asili ni Mdhaifu kwasababu anatamani kila kitu asichokuwa nacho na kutaka kufanya kila kitu asichokuwa na uwezo wa kukifanya sawia na hata wale wanaotaka kukifanya sawia hataki wakifanye. Anaishia kuvulunda kila mahali anakopita na kwasababu ya UDHAIFU wake haoni ajabu KUVURUGA hata lile alilokwisha VURUGA kwakuwa kila kitu yeye kinawezekana

BACK TANGANYIKA

umenena. hako kaugonjwa amewaambukiza na watendaji wake karibia wote, including na wale ambao watu wanadiriki kuwaita eti ni "wasafi" na "wachapa kazi". my foot!!

sikiliza. hela ya mradi wa barabara "fulani" ili ikamilike inahitaji bilioni 200:

1. mr "john pombe" anawaza kumalizia lile "banda" lake "kule" kwa bilioni 10;

2. wakati huohuo "ile account" yake nyingine "kule" offshore inahitaji top up ya kama bilioni 15;

3. "ile" small house yake inayoishi "pale" karibu na "nanihii" inahitaji kama bilioni 1 hivi;

4. kufanikisha haya, midomo yote ya "juu" na "chini" lazima izibwe; ipi na vipi??

5. midomo ya "juu" ni "bosi" wawili - size ya mgao ni siri yake mwenyewe "mr john pombe";

6. midomo ya "chini" ni watendaji wizarani na idarani ambao wako kama 10 - nusu bilioni kila mmoja inatowatosha hawa;

so, barabara yenye mahitaji yasiyopungua bilioni 200 inajengwa kwa bilioni 150. halafu mtu unashangaa viraka vinaanza kuonekana baada ya miezi 6, kwani ulikuwa hujui kuna UDHAIFU?
 
Last edited by a moderator:
Hawezi kuwa wa kawaida hata siku moja kwa sababu kuwa Rais tu sio kitendo cha kawaida toka uhuru tuna Marais wangapi? Pili ujue kichwani kwako jamaa amezaliwa siku moja na Putin, na wote ni Marais, kitakuwa kichwa cha kawaida?
 
Ukweli ni kuwa CCM hawawezi kukubali kura ipigwe kabla ya Uchaguzi kwa sababu kubwa mbili, kwanza, 1. wanajua wananchi hawajaridhishwa na huu mchakato na pia sasa hivi ukinzani ni mkubwa mno hata ndani ya chama kwenyewe, hivyo wanahitaji kuzua jambo jingine hapa kati kati ili kuhamisha public attention kutoka kwenye katiba kwenye huo upuuzi mwingine, tunaweza sikia rais anataka kupangua baraza la mawaziri (Lukuvi kesha lianzisha kwa Nyalandu), na sababu ya pili,2. hawana fedha ya kuhonga na kununua kadi za kupigia kura, hivyo they need time kukwapua fedha za kufanikisha uharamia wao.

CC Malisa Godlisten

Naunga mkono haja zako 100%, wanajua kila kitu ila wanajitoa ufahamu tu, tena kuhamisha mada wanaweza fanya kitu cha ajabu zaidi ya kupangua baraza la mawaziri.
secondly, hela ya uchaguzi wanazo kibao, sema tu kwa sababu ya tamaa zao hawaridhiki wataendelea kuvuta kila kona wawezayo. Jiulize kwa miezi sita iliyopita bei ya mafuta haijashuka tena, inazidi kupaa, nafikiri mpaka uchaguzi ufikie lita ya petrol itakuwa imepita Tshs. 2500/= -bei ziko kwenye mwendo mdundo, wanazikusanya kama hawana akili nzuri
 
Mimi nina swali: hivi haya mapendekezo yatapigiwa kura na wananchi au ndo imepita hivyo?

Yatapigiwa kura na wananchi mkuu ila wazungumzaji wote walikuwa wanafanya kampeni ya tupige kura ya ndio na nadhani ndio lengo la hiyo event kufanyika maana sidhani kama kwenye mpangilio ilitakiwa kuwepo na kama ilitakiwa kuwepo nadhani ilikuwa ni kumkabidhi Rais na kutuambia wananchi tupige kura bila kuanza kuipigia chapuo especially kwa rais (kwa wajumbe wa bunge maamlumu sina shida nao sana maana wao ndio waliijadili na kuifikisha hapo)
 
Usimung`unye maneno.....sema Kikwete ni "mnafiki" baaaasi!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom