Malisa Godlisten
JF-Expert Member
- Jan 20, 2010
- 202
- 1,588
Jana wakati akipokea Katiba pendekezwa ambayo inasubiri kwenda kupigiwa kura na wananchi, Rais Kikwete alisema hivi "Hatuwezi kusema kama tutaendelea na mchakato kwa sasa, au tatasitisha hadi mwakani kwa sababu mazungumzo bado yanaendelea."
Rais Kikwete aliitangazia dunia jana kuwa hata yeye hajui mchakato unaendelea lini, kama ni sasa au ni baada ya uchaguzi mwakani. Wengi walidhani Rais yupo sahihi kuwa hajui lini mchakato unaendelea. Ukweli ni kwamba Rais alitoa kauli ile ili kuondoa sintofahamu iliyopo kwny jamii kuhusu lini mchakato huu unaendelea.
Sintofahamu hii inatokana na kupingana kwa kauli za watu wawili ambao wote wanadai wametumwa na Rais Kikwete.
Wa kwanza ni Waziri, AshaRose Migiro aluyesema "Mchakato unaendelea kama kawaida, waTZ wajiandae kupiga kura ya maoni."
Wa pili ni Mzee John Cheyo aliyesema bungeni kuwa "Mchakato utasitishwa hadi baada ya uchaguzi mkuu mwakani".
Baada ya kauli ya Migiro na ya Cheyo kupingana, Rais Kikwete ameshindwa kuwa na msimamo. Ameogopa kuegemea upande wa Cheyo (aliyefanya nae mazungumzo Ikulu) au wa Migiro (aliyemteua). So ameamua kuwa "neutral" kwa kusena hajui mxhakato utaendelea lini, ili asimkwaze Migiro wala Cheyo.
MY TAKE.!
Miongoni mwa hasara kubwa tulizonazo watanzania ni pamoja na kuwa Rais asiye na msimamo. Sifa kubwa ya kiongozi bora ni kuwa na MSIMAMO na kuutetea msimamo huo hata kama utapingwa na wengi. Kama ni msimamo wenye maslahi kwa umma usimamie na usiyumbeyumbe. Hii itakujengea heshima kubwa hata utakapoondoka madarakani.
Mao Tse Tsung ni miongoni mwa viongozi waliokua na misimamo mikali sana. Na bahati mbaya misimamo yake mingi ilipingwa na wananchi wengi wa China.. lakini hakubadili misimamo yake licha ya kupingwa na wengi.. maana alijua ni misimamo yenye tija kwa taifa.. na leo China inanufaika sana na misimamo ileile ya Mao Tse Tung waliyoipinga zamani.
Hapa kwetu Rais Kikwete hana misimamo kwa sababu anapenda kuonekana mzuri kotekote. Hapendi kukwaza upande "A" wala upande "B". Anataka kote aonekane mwema.
Rais Kikwete wakati anahutubia jana alijua kabisa kuwa Waziri wake wa Sheria, Migiro alishasema mchakato unaendelea. Na alijua pia kuwa vyama vya siasa kupitia kwa mzee Cheyo vilishasema hadi mwakani baada ya uchaguzi.
Sasa Kikwete jana akaona akisema mchakato unaendelea ataonekana mbaya kwa kina Cheyo, na akisema unasitishwa hadi mwakani atatofautiana na waziri wake Migiro. Kwa hiyo eti akaamua kukaa katikati kwa kusema "mazungumzo yanaendelea". Ajabu sana hii. mazungumzo yapi? Na nani? Na yataendelea hadi lini?
Lakini tabia hii ya Rais Kikwete ya kupenda kuwa Padri na Imamu kwa wakati mmoja si ya jana wala juzi, nadhani ni ya kuzaliwa (inborn character). Maana mambo mengi sn amekuwa katikati hata yale ambayo alitakiwa kuonesha msimamo wake kama kiongozi mkuu wa nchi.
Wakati wa sakata Dowans Rais Kikwete aliwahi kusema "suala hili tulishaanza kuona lina walakini tangu mwanzo". Lakini Dowans hiyohiyo ilipojibadili jina kuwa Symbion, ni Kikwete huyohuyo aliyemualika Rais Obama na kwenda kuzindua mitambo. Akazindua mitambo ya watu walewale aliosema ameona wana "walakini" tangu mwanzo.
Tunashindwa tumueleweje Rais wetu. Si moto, si baridi. Si mweupe si mweusi. Hakubali wala hakatai. Rais asiye na msimamo.
Mwanafalsafa Plato aliwahi kusema "nothing can be and not be, at the same time in the same context"... Yani kitu hakiwezi kuwepo halafu tena kisiwepo kwa wakati huohuo na kwa namna hiyohiyo.
Yani huwezi kuwa mnene halafu tena ukawa mwembamba kwa wakati huohuo. Huwezi kuwa mweupe halafu tena ukawa mweusi kwa wakati huohuo...Mtu pekee duniani aliyeweza kuwa mnene na mwembamba kwa wakati mmoja... akawa mweusi na mweupe kwa wakati huohuo ni Rais wetu mtukufu Jakaya Kikwete. Our President is Extra Ordinary.!!
JIPU LIMEPASUKA, SIWEZI KUWA ADUI KWA KUSEMA UKWELI.!
Malisa GJ || Your Partner In Critical Thinking.!