Rais Kikwete "NAKUSHAURI UJIUZULU"

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Wakati unaingia watu walikuwa na imani sana na wewe lakini huenda ukaondoka
wakati watu (Watanzania) wamejenga chuki kubwa sana kwako. Yanayojitokeza
ni mengi na hayajawahi kutokea awamu yoyote ya uongozi katika nchi hii, huenda
washauri wako hawana nia nzuri na wewe kwa kukutumbukiza katika majanga mabaya
ambayo mwisho wa siku yameifanya nchi yetu kuondoka katika sifa ya kuwa kisiwa
cha amani.

Huenda CHADEMA Wanakuhujumu ili usitawale vizuri.

Huenda WAPINZANI wanakufitini kwa kukitaka kiti chako.

Huenda ni MAADUI ZAKO NDANI YA CHAMA wanakufanyia yote haya.

Huenda wananchi umeshindwa kuwatekelezea ahadi yako ya maisha bora

Umeleta kaulimbiu ya kujivua gamba nafikiri ni muda muafaka sasa kama mwenyekiti
wa Chama kuonyesha mfano kwa wenzako. JIVUE GAMBA mkuu yasijekutokea yale
ya misri kwani kuna kitu kina fukuta chini kwa chini.

Mimi sipendi utoke, napenda kukuona ukiwa ikulu lakini kwa hali jinsi ilivyo
ni Bora umkabidhi nchi Magufuli, Mwakyembe au hata NAPE sio mbaya kwa
muda tu wakati tunasubiri katiba mpya na uchaguzi mwingine.

Watanzania naona kama wanavuta Bangi siku hizi wasije kukung'oa kwenye
kiti kwa upuuzi wao wanaouita nguvu ya Umma.

Ni hayo tu.

Wako mdau wa gesi.
(NAUNGA MKONO MATUMIZI YA GESI KWA WATANZANIA WOTE)

Joseph A Chinamkalava
box........
Mnyambe
Newala
 
Unadhani viongozi wa Afrika wanaachia madaraka kiulaini hivyo hizo ni ndoto za alinacha mkuu. Mshauri atekeleze ahadi zake kwa kipindi kilichobaki ulimsikia nani ktk serikari yake alijiuzuru huo si utaratibu wa Afrika lujiuzuru ni utaratibu wa huko majuu mkuu unamwonea tuu.
 
Zinatekelezeka?
 
Mkuu tumefunga ndoa ya kikristu, tena katoliki! Mwenye mamlaka ya kuitengua ni Papa pekee. Vuta subira hadi 2015!
 
Wakati unaingia watu walikuwa na imani sana na wewe lakini huenda ukWaondoka wakati watu (Watanzania) wamejenga chuki kubwa sana kwako.
Mimi sipendi utoke, napenda kukuona ukiwa ikulu lakini kwa hali jinsi ilivyo
ni Bora umkabidhi nchi Magufuli, Mwakyembe au hata NAPE sio mbaya kwa
muda tu wakati tunasubiri katiba mpya na uchaguzi mwingine.

Unapaswa kuielewa katiba ya Tanzania kabla ya kutoa ushauri kama huu. Hata JK akijiuzuru, au kufa, si kwamba kina Nape au Mwakyembe ndio watachukua nchi. Makamu wa Raisi, Dr Bilali, ndiye atakayekuwa raisi hadi uchaguzi mkuu 2015.

Sasa tafakari, JK atoke na Bilali aingie kuwa Raisi wa Tanzania hadi uchaguzi mkuu 2015.
 
kweli umechoka kufikiri au hujui serikali yake ina fanya nini au na wewe upo kwenye kundi lile la wandishi wa habari ambao huhama wote kuelezea habari moja na kusahau singine hata sisi tuki kuanagalia wewe tunaona una busara kumbe hovyoooo
 
Mods ondoeni hii ni utumbo mtupu. Lazima atakuwa mtu wa CHADEMA huyu.

Why CDM umetumia kigezo gani? maana huenda akawa wa chama chochote kikiwemo cha mkulu wa kaya kwani nao si walikuwa hawamtaki awe mwenyekiti wao, au mi ndo nimesahau? maana nilimsikia Nape analalamika kuwa watu wanataka kumpindua Mwenyekiti kwenye chama, so mkuu usikimbilie kuhukumu bila utafiti.
 
kweli umechoka kufikiri au hujui serikali yake ina fanya nini au na wewe upo kwenye kundi lile la wandishi wa habari ambao huhama wote kuelezea habari moja na kusahau singine hata sisi tuki kuanagalia wewe tunaona una busara kumbe hovyoooo

1. Red - Ninyi kina nani?
2. Green - Ahsante.
 
Unapaswa kuielewa katiba ya Tanzania kabla ya kutoa ushauri kama huu. Hata JK akijiuzuru, au kufa, si kwamba kina Nape au Mwakyembe ndio watachukua nchi. Makamu wa Raisi, Dr Bilali, ndiye atakayekuwa raisi hadi uchaguzi mkuu 2015.

Sasa tafakari, JK atoke na Bilali aingie kuwa Raisi wa Tanzania hadi uchaguzi mkuu 2015.
Usijali Mkuu nafahamu sana hiyo ni aina tu ya Lugha.
 
amalizie kipindi chake ila asisaini mkataba wa aina yeyote mpaka aondoke madarakani, hata wa uchimbajin wa uranium hatuutaki uendelee, nashangaa majitu yamekaa kimya tu sehemu ambazo wakoloni wanakuja kuchimba uranium yenye madhara kwa binadamu bila kusema chochote, NAPONGEZA watu wa MTWARA kwa msimamo wao
 
Back
Top Bottom