Rais Kikwete na ukomo wa Chama Cha Mapinduzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete na ukomo wa Chama Cha Mapinduzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Nov 9, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,656
  Trophy Points: 280
  Na Julius Samwel Magodi

  INGAWA baadhi ya wanasiasa ndani ya CCM wanasema malumbano makali yanayoendelea katika chama hicho ni ya kukiimarisha; ukweli ni kwamba. sasa kinaelekea kufikia kwenye ukomo wake.

  Wanasiasa hawa ambao bado wanatamba kwamba, chama chao bado kina nguvu na mshikamano kama zamani, hawajui kuwa sasa chama hicho kinateketea kikiwa bado madarakani mithili ya mshumaa ambao unakwisha huku ukitoa mwanga.

  Inaonekana makundi mawili ndani ya chama hicho yanayohasimiana, yaani kundi la watuhumiwa wa ufisadi na kundi linalopinga uchafu ndani ya chama hicho, yameamua kuonyeshana ubabe kama mmoja kamwaga mboga basi mwingine anamwaga ugali ili kila mmoja akose.

  Vita hiyo ndani ya chama hiki kikongwe nchini ambayo sasa inawahusisha wabunge hadi mawaziri, ilizidi kupamba moto zaidi wiki hii baada ya Kamati ya rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi kuanza kukutana na wabunge mjini Dodoma.

  Tayari mawaziri wawili wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete wameshajitoa kuonyesha upande wao katika makundi haya, ambao ni Sophia Simba (Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora) na Dk Makongoro Mahanga (Naibu Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana) ambao waliamua kusimama kidete kuwatetea aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa aliyeachia ngazi kutokana na kuibuka kashfa ya Richmond na Mbunge wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge kwamba, maneno yanayosemwa juu yao ni wivu tu.

  Lakini pia Waziri Simba mbali ya kumsafisha, Lowassa na Chenge akisema ni watu safi, alikwenda mbali zaidi na kumshambulia Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango na mumewe, mzee John Malecela.

  Simba alidai kuwa wawili hao sio watu wasafi kama wanavyojinadi kwani Malecela amewahi kuchukua Sh200 milioni za kampeni zake za kuwania urais ndani ya CCM na kwamba hata fedha za harusi yake na Kilango zilitoka kwa mtuhumiwa wa ufisadi, Jeetu Patel.

  Hata hivyo, Mzee Malecela amemjibu kwa kueleza kuwa Waziri Sophia ni mgonjwa wa akili ambaye anapaswa kupelekwa Hospitali ya Mirembe mjini Dodoma kutibiwa, kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam.

  Wakati Malecela akisema hayo mkongwe mwingine katika chama hicho amekaririwa katika kikao hicho cha Mwinyi akisema kwa njia yoyote ile Spika Samuel Sitta anapaswa aondoke katika chama hicho kwa madai kuwa analeta machafuko.

  Kwa hakika, ukiachia matusi hayo ambayo yamekuwa yakiporomoshwa kutoka kila upande, katika uhai wake CCM hijawahi kufikia katika mvutano mkali wa kutishia uhai wake kama ilivyofikia hivi sasa.

  Inaonekana wazi kwamba moto ulioanza kuwaka ndani ya chama hicho, kamati ya Mwinyi haitaweza kuuzima, unahitaji kikosi cha zima moto sio kuuzima kwa kutumia ndoo za maji.

  Swali ni nani atasimama kuzima moto huo kwa sasa katika CCM, iwapo wazee wanaoheshimika ndani ya chama hicho kama Malecela wameingizwa katika vita hii? Je, Rais Jakaya Kikwete ataweza kuuzima moto huu?

  Bila shaka sasa Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM taifa, anapaswa kusimama na kuonyesha uwezo wake wa kukinusuru chama kumeguka. Kile ambacho alikuwa akikiogopa siku zote kukifanya sasa anatakiwa kukifanya apende asipende.

  Anatakiwa kuonyesha kuwa amesimama upande upi kati ya makundi haya, haijalishi awe upande wa watuhumiwa wa ufisadi au upande wa wapambanaji wa ufisadi. Wananchi tunataka kujua rais wetu yuko kundi gani ili kama atagombea urais tena mwakani tuweze kujua kura yetu tunampa ama ala.

  Lakini Rais Kikwete kuendelea kutaka kuyafurahisha makundi haya yote, ni kuichimbia kaburi CCM yake na yeye mwenyewe kuhatarisha nafasi yake ya urais.

  Nasema hivyo kwa sababu kama atakubali chama hicho kimeguke kikiwa mikononi mwake, huenda akajikuta hana chama na kubaki mwenyekiti wa chama ambacho hakipo kwani vitazaliwa vyama vingine vya CCM wasafi na CCM watuhumiwa nakadhalika.

  Endapo hali hii ikitokea nchini Rais Kikwete atakuwa amefuata nyanyo za Rais Gobachev wa iliyokuwa Jamhuri ya Kisoviet ya Urusi ambaye baada ya kusambaratika kwa dola hiyo kubwa duniani akajikuta ni rais asiyekuwa na taifa kwa vile majimbo yote yalibadilika na kuwa nchi ambazo zilikuwa na marais wake.

  Ukomo wa CCM unajionyesha wazi kutokana na ukweli kwamba, hata mawaziri wa serikali ya Rais Kikwete wamegawanyika kila mmoja anashabikia upande wake.

  Kama waziri wa serikali iliyopo madarakani anadiriki kueleza kuwa hakuna mtu msafi nchini wote ni mafisadi na kwamba watuhumiwa wa ufisadi nchini wanaonewa wivu; ni hatari sana.

  Imefikia mahali baadhi ya mawaziri hao wanadiriki kusema kwamba kwa hali hii ya mgawanyiko uliopo ni bora CCM isambaratike ili makundi haya yaunde vyama vyao vya siasa.

  Inaonyesha sasa wabunge wa CCM wameamua sasa kuisambaratisha serikali yao, wakisahau kwamba, atakayeumia zaidi ni Rais Kikwete ambaye atakosa chama na hatimaye kukosa sifa za kuwa kiongozi wa nchi.

  Kwa upande mwingine, kusambaratika kwa CCM kunaweza kuwa ni faraja kwa Watanzania kwa sababu kutasaidia kufanyika kwa mabadiliko ya uongozi kirahisi pale ambapo wananchi wanachoka na serikali iliyopo madarakani. Kwa sababu hakutakuwa na chama chenye nguvu kubwa na mizizi kama kilivyo CCM, karibu vyama vyote vitakuwa na nguvu sawa. Kuwa na vyama vyenye nguvu sawa ni nzuri kwani hata Bunge litabadilika kutoka kuwa mhuri na kuwa la kuibana serikali kutekeleza wajibu wake.
   
 2. Nemesis

  Nemesis JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2009
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 3,833
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  angalia katuni hii, ina ujumbe murua kabisa, thanks to Kipanya.


  [​IMG]
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,656
  Trophy Points: 280
  Teeeeeeeeeeeeeehhhhh teeeeeeeeeeeeeeehhhhh

  so nice
   
 4. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  hiyo itakawa bomba. Mie natamani hata kesho CCM isambaratike angalau tutaona mwanga kwani wakisambaratika njia za wizi zote zitajulikana kuanzia kwenye kura na mengineyo mengi. Pia kura zao nao zitagawayika kwa hiyo hii itapelekea kuwa na bunge zuri ambalo halitapitisha ujinga. Kama wa kwenda kuchimba dhahabu kwenye mbuga za wanyama na nyinginezo. Hakika rais atakayekuwa madarakani atahenyeka sana.
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,656
  Trophy Points: 280
  lile sio BUNGE....LILE NI VIKAO VYA HARUSI NDIO MAANA WANAAIRISHA KILA MARA ...UNAJUA KWENYE KIKAO CHA HARUSI UKIONA HAKUNA DALILI ZA MICHANGO MNASOGEZA MBELE NDIVYO LILIVYO BUNGE LETU LA MAFISADI
   
 6. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #6
  Nov 10, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Kwi! kwi! kwi! hii kali....
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  We we we we... Mungu aepushilie mbali. We hujui kwua CCM ikisambaratika na nchi itasambaratika! CCM ndio Mungu wetu, hatuna ujanja bila yenyewe
   
 8. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Ni matumaini yangu kuwa hii ni kauli ya utani na si si kwamba unamaanisha haswa!!! Otherwise...
   
 9. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ni utani ambao una ukweli ndani yake. We huoni CCM ilivyotushika?
   
 10. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #10
  Nov 10, 2009
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Ina ukweli mkubwa nashangaa pamoja na madudu yote bado wapo watu tena wengine wamechoka balaa wanaimba No 1
   
Loading...