Ni wapiga kura ndio watakoamua kama tatizo la ufisadi ni kubwa kiasi gani,jambo ambalo REDET wangeweza kuwauliza wananchi kwa kufanya poll. Je,wananchi wanaliona tatizo la ufisadi ni tatizo kubwa kiasi gani? Inawezekana wapiga kura wakaitosa CCM,kwa sababu ya ufisadi,au wakaitosa CCM ikimweka Kikwete kugombea? Je kuna wananchi ambao hawaamua watampgiai kura nani,isipokuwa wameshaamua kwamba hawampigia kura Kikwete?
Kama wananchi wanaona hitilafu katika Serikali ya sasa,je wana imani kwamba mabadiliko ya uongozi yanaweza kuleta Serikali bora zaidi?