Rais Kikwete mgeni rasmi Tamasha la Pasaka

Rais Kikwete mgeni rasmi Tamasha la Pasaka

Jk kafute dhana ya udini. Manake ulianzisha mwenyewe.
 
Sihitaji malumbano, nadhani unafahamu vyema maana ya platform, sasa ikiwa kila mtu atakuwa anapost thread yake kwenye jukwaa la siasa kutakuwa na maana gani ya kuwa na platform? au hii ni habari ya siasa? naomba unieleweshe wewe maana labda mimi sielewi.

Kwa kweli mimi sihitaji malumbano yoyote kutoka kwako, nadhani tunatofautiana mitazamo tu, kuna Thread za Cardinal Pengo sijasikia umesema Mods peleka Jukwaa la Dini, hili la Kikwete kuhudhuria Tamasha la Pasaka ni la kisiasa zaidi kwa jinsi nionavyo mimi ni mtazamo wangu
 
Wizi mtupu....BIASHARA(MSHAMA and co) / SIASA(JaKAYA) VS IMANI(WAUMINI) ni vitu tofauti.
Hii yote ni promosheni ya kusaka pesa/kujisafisha kwa mbinu zozote, tamasha la Pasaka? ingelikuwa kiingilio ni bure na wachague mahali watakapofika watu wa rika zote za kipato....hapo tungesema kweli walioandaa na mkuu wa kaya wanataka kweli kufufuka na kristu, lakini hii ya Diamond then kiingilio ma TZS...,000/=?hakika kujisafisha kuna njia nyingi.
BINADAMU TUNAFANANA LAKINI TUNATOFAUTIANA
 
Nilikuwa na mpango wa kwenda lakini kwa sababu ya huyu MPINGA UKRISTO KIKWETE SIENDI TENA.
 
Hivi huyu msanii ana ujasiri kiasi hiki? Siasa zake za udini alizosiasisi baadaya ya zile za maji taka kufail zimeacha makovu mengi, na moja wapo ni mauaji ya mwinjilsti aliyeuawa huko Mto wa mbu leo hii anathubtu kufika kwenye shughuli za Kikristo bila hata ya kuwaomba radhi wakristo? Hana aibu kabisa huyu mkwere
 
Pengine neno litamuingia na kukumbuka wajibu wake kwa Watanzania...tuongeze maombi jamani maana Yesu anasema amekuja kwa ajili ya waliopotea.
 
Msama ni mjasiriamali kiingilio shilingi ngapi vile? Ndo maana maaskofu mashuhuri kama pengo, malasusa, laizer huwezi kuwaona hapo! Msama kapewa kitu kidogo ili amualike jk, kwenda kuona mauno ya kina rozi mhando!
 
Naomba kuuliza.
Lengo la hilo tamasha ni nini?
Na kwanini JK asiwe mgeni rasmi ktk tamasha hilo?
 
Naomba kuuliza.
Lengo la hilo tamasha ni nini?
Na kwanini JK asiwe mgeni rasmi ktk tamasha hilo?

Kwa sababu JK ni adui wa ukristo hapa Tanzania.Angalia wasemaji wake hapa JF wanavyouchukia ukristo.
 
Hawa waandaaji nao wako kimaslahi zaidi,jk ana upako gani wa kubariki tamasha.JK ni mwanasiasa,hapo wangemwalika kiongozi wa dini.
 
It really does disgust me,ndo hawa hawa shughuli ya kikanisa unashangaa mgeni rasmi rostam aziz..kama si kutafuta maslahi kupitia mgongo wa neno la Mungu ni nini? Mnafanya biashara nyumbani mwa Mungu,Yesu angepindua meza zenu...
 
Awepo asiwepo siendi, kwanza posibility ya kutokwenda inazidi kwa kutuhahakikishia JK atakuwepo!!

The guys likes dancing while the economy sucks!!! Shame on you Mr. Prezidaa.
 
Naomba kuuliza.
Lengo la hilo tamasha ni nini?
Na kwanini JK asiwe mgeni rasmi ktk tamasha hilo?

Wamesema lengo la Tamasha hilo ni kuwasaidia waathirika wa mabomu ya Gongo la Mboto, pamoja kusomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane
 
rais jakaya mrisho kikwete atakuwa mgeni rasmi wa tamasha la pasaka litakalofanyika aprili 24 kwenye ukumbi wa diamond jubilee jijini dar es salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya tamasha hilo ambae ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya mshama promotions, alex msama aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa rais amethibitisha kubariki tamasha hilo.
Napenda kuwaambia kwamba rais wetu mpendwa wa jamhuri ya muungano wa tanzania, jakaya kikwete amethibitisha kuwa mgeni rasmi katika tamasha letu mwaka huu.
Amekubali kushirikiana na wakristo wote kusherehekea sikukuu ya pasaka diamond jubilee, alisema msama aliyeambatana na mshauri wa kamati ya maandalizi, askofu rashid matigisa, askofu philemon. Wainjilisti john benjamin na elia mashaka pamoj na shemasi benjamin.
Mshama alisema kwa niaba ya kamati namshukuru rais kwa kukubali mualiko wa kuhudhulia tamasha hilo, wasanii mbalimbali wa muziki wa injili wamethibitisha kushiriki ni pamoja na rose muhando. Anastazia kutoka kenya.
Mwananchi march 14, 2011

ahsante kwa taarifa njema. Mungu ambariki sana rais wetu mpendwa ambaye hana udini wala nini. Haleluyaaaaaaa
 
Unakuja na matunguli yako pale unajikuta chali!! Aibu tupu!!
 
nilitarajia kabisa ashiriki huyu mtu, kwanza kujisafisha kwamba yeye sio mdini, pili hana kazi za kufanya na yeye ni mpenda matamasha. juzi swahiba wake Lowasa nae walimualika kwenye haya matamasha ya dini. kwa hakika yameanza kupoteza credibility kabisa, hamna dini tena bali siasa tu
 
Back
Top Bottom