Mjomba wa taifa
JF-Expert Member
- Apr 20, 2012
- 231
- 161
Kumekuwa na taarifa mbalimbali toka pembe zote nchini Tanzania kuwa Rais Jakaya Kikwete anatarajia kuchukua "MAAMUZI MAGUMU" ya kuwafukuza kazi Mawaziri walitaojatwa katika sakata la ESCROW pia kuwapumzisha kazi Mawaziri wote ambao wametajwa kuwa ni Mizigo kama vile Christopher Chiza.
Sidhani kama wanaosema maneno haya wametafakari zaidi kuhusu Raisi Kuchukua Maamuzi Magumu. Hivi kweli ndugu zangu, wabadhilifu waliotajwa mpaka leo bado wapo Ofisini wengine wanasafiri nje za nchi bado wanakula posho za nchi, Rais mpaka leo anajivuta kuchukua uamuzi?
Kwa mujibu wa sheria za kazi za nchi, mfanyakazi anapotuhumiwa kwa ubadhilifu ama wizi wowote kazini, husimamishwa kazi (SUSPENSION) huku akiendelea kulipwa mshahara wake kama kawaida ili kupisha uchunguzi ufanyike kubaini ukweli wa tuhuma. Na ndivyo imekuwa ikifanyika kwa watumishi wote Sekta binafsi na za Umma. Sasa mpaka leo mabwana hawa bado wapo ofisini licha ya tuhuma zinazowakabili ili waendelee kupiga dili zingine kumalizia miezi 9 ya JK kuwa madarakani.
Kinachosaidia hapa ni mashinikizo mbalimbali toka mataifa ya Magharibi ya kuinyima Tanzania misaada ya kifedha ndo maana matamko toka Ikulu chini kwa chini tunasikia Rais anatarajia kufanya MAAMUZI MAGUMU. Sitampinga Mbunge wa Ubungo John Mnyika aliposema tumefika hapa kwa kuwa RAIS ni dhaifu iwapo CCM na Ikulu bado itaamini kuwafukuza mafisadi uwaziri ni "MAAMUZI MAGUMU".
Kama hatujui UAMUZI MGUMU ni bora tukae kimya au tusome historia ya baadhi ya MAAMUZI MAGUMU ikiwemo kutaifisha taasisi zote za watu binafsi uamuzi uliofanyika baada ya Uhuru. Maamuzi mengine Magumu ni yale ya Wazi, ri Mkuu Marehemu Sokoine ya kukamata Wahujumu uchumi, hali iliyopelekea wahujumu uchumi kukimbia mali zao.
Kwa hili la kuwafukuza mawaziri wezi si MAAMUZI MAGUMU hata kidogo, na hata kama itatokea Raisi akawafukuza wezi hawa wala hatoingia katika orodha ya viongozi waliowahi kufanya MAAMUZI MAGUMU TANZANIA. Labda afanye kwa kujiburudiasha tu. Alikuwa na Uwezo wa kufanya MAAMUZI MAGUMU toka alipochaguliwa mwaka 2005 ambapo wananchi wengi nikiwemo mimi tuliingia mkenge kwa kuhadaika na mwonekano wake tukadhani atakuja kufanya MAAMUZI MAGUMU kumbe anakuja kutafuta udaktari na uprofessor wa kutembelea nchi nyingi duniani kama Vasco Dagama.