Rais Kikwete ateua bodi mpya ya TANESCO

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Posts
55,030
Reaction score
59,684
Mwenyekiti ni Mboma....
je kutakuwa na mabadiliko yoyote? au kama jana tu

..........................................................................................................................................................................................................................
TAARIFA KWA UMMA
​

YAH: UTEUZI WA BODI YA WAKURUGENZI YA SHIRIKA LA UMEME TANZANIA (TANESCO)​
​



Napenda kuwajulisha wananchi na wadau wote kuwa kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma Sura 257 kama ilivyorekebishwa mwaka 2002 (The Public Corporations Act, Cap. 257 of R.E. 2002) Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jenerali Mstaafu Robert P. Mboma kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuanzia tarehe 27 Oktoba 2011 baada ya Bodi iliyokuwepo kumaliza muda wake tarehe 26 Oktoba 2011.


Pamoja na uteuzi huo, Mheshimiwa William M. Ngeleja Waziri wa Nishati na Madini kwa Mamlaka aliyonayo amewateua wakurugenzi wanane wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania kuanzia tarehe 27 Oktoba, 2011. Walioteuliwa kuwa Wakurugenzi wa Bodi ni pamoja na:-


1. Bw. Baruany Elijah A. T. Luhanga
2. Bw. Ridhiwan Ali Masudi
3. Bw. Leonard R. Masanja
4. Bw. Vintan W. Mbiro
5. Bw. Beatus P. Segeja
6. Bw. Hassan Ally Mbaruk
7. Mhe. Victor K. Mwambalaswa (Mb.)
8. Bw. Abdul Ibrahim Kitula


Imetolewa na:
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

............................................................................................................................................................
Anawaweka sawa ili Dowans wajilipe bila mkwaruzo.

​
​
 
Pamoja na uteuzi huo, Mheshimiwa William M. Ngeleja Waziri wa Nishati na Madini kwa Mamlaka aliyonayo amewateua wakurugenzi wanane wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania kuanzia tarehe 27 Oktoba, 2011. Walioteuliwa kuwa Wakurugenzi wa Bodi ni pamoja na:-
Bw. Baruany Elijah A. T. Luhanga
  1. Bw. Ridhiwan Ali Masudi​
  2. Bw. Leonard R. Masanja​
  3. Bw. Vintan W. Mbiro​
  4. Bw. Beatus P. Segeja​
  5. Bw. Hassan Ally Mbaruk​
  6. Mhe. Victor K. Mwambalaswa (Mb.)​
  7. Bw. Abdul Ibrahim Kitula​
[/LEFT]
 
..huyo Mwambalaswa siyo yule mwenye kampuni ya umeme akiwa na ubia na Dr.Mwakyembe?

.
 
Nchi hii viongozi wetu ni nazi tupu! Haaaa!
 
Mboma tena du, nchi hii, halafu mbona wabunge bado wanachaguliwa kwenye bodi za mashirika, watayasimamia vipi hawa?
 
Ingekuwa vyema angewapa Jeshi waendeshe TANESCO maana hawa ndugu zetu wa uraiani wameshindwa kabisa.

Nakubaliana na wewe 100% Bora Fisadi Kikwete akaikabidhi na Nchi Jeshini vilevile sio Tanesco pekee, Madudu yanayoendelea katika nchi hii bora Wakina Shimbo waimalize, wameshindwa kuilinda nchi wataweza kuiongoza? Ingawa wapo Wengi Serikali lakini hawana hata maana yoyote hao wanajeshi zaidi ya Kuendeleza Ufisadi kama alivyo Kikwete.

Jeshi la Tanzania lipo kwa ajili ya kulinda Ufisadi sio kutetea taifa
 
Jeshi la Tanzania ni lakifisadi halina maadili kwa Watanzania, Jeshi letu limegeuzwa kuwa kitengo cha kukwapua kodi zetu. CCM mnatuharibia nchi yetu kila sehemu, tumewakoseeni nini sisi Watanzania? au Upole wetu ndio mtaji wenu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…