Rais Kikwete atakiwa Kujiuzulu

sasa nani awe rais tz?

achen hizo huyo jamaa ana kibarua kigumu sana kufunika na kukalia mabaya yaliyofanywa na mkapa!!!!!
na ndo kazi pkee anayoifanya tu! vinginevyo basi mkubali mkapa apelekwe kizimbani ili maovu yake yote jamaa ayatue na ndipo twaweza kusema anaweza au la maana hadi hivi sasa hakuna kitu JK ameshawahi kufanya kikubwa hapa nchini zaidi ya safari na ufunguzi wa majengo na kualikwa kuwa mgeni rasm kwenye majukwaa mbali mbali.
 
Kujiuzulu Rais Tanzania inawezekana Wabunge na Wananchi wakiwa sirious,ni muda tu bado na akiendelea kukaidi atakuja kushitakiwa baadaye kama wanavyofanywa marais wengine wastaafu.
 
Kwani si aliisha-jiuzulu? kwani Kikwete rais?

Una maana gani alishajiuzulu wakati yeye bado yuko Ikulu na anaendelea kutoa maagizo nini cha kufanya,japo kwamba hana meno lakini ndiyo hivyo sijawahi kuona Rais ambaye hana mamlaka kama huyu.Je huyu ndiye aliyechaguliwa kwa asilimia 80 kweli au kiini macho?Au inawezekana yeye yuko tuu kama kanya boya lakini wanaoendesha nchi ni watu wengine.

Na kama ni watu wengine wamepata wapi ridhaa yetu wananchi kutuongoza?
 
wakichafuka, wanachafua halafu wanasafishwa

Huu mchezo wa kusafisha watu waliochafuka na maji taka umeanza lini kwenye serikali yetu.Na kwa kutumia mtundo huu kweli tutaleta maendeleo Tanzania,si tunacheza tuu.
 
Ndiyo maana RA anadharau watanzania na kusema mijinga hii haina akili ukiangalia jinsi mambo yanavyopelekwa ni kweli.
 
Back
Top Bottom