Rais Kikwete atakiwa Kujiuzulu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais Kikwete atakiwa Kujiuzulu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kachero, Aug 3, 2009.

 1. K

  Kachero JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  KIONGOZI wa Upinzani bungeni Hamad Rashid Mohamed, amemtaka Rais Jakaya Kikwete, kujiuzulu kutokana na kile alichosema ni serikali yake kushindwa kufanya kazi hivyo kukosa imani kwa wabunge wa chama chake Chama Mapinduzi (CCM).

  Shinikizo hilo la upinzani linakuja wakati hali ya kisiasa nchini ikiwa tete huku Bunge na serikali ya Rais Kikwete, zikiwa katika msuguano wa utekelezaji wa baadhi ya mambo mazito ikiwemo hatua za kuchukua kwa watumishi waandamizi wa umma waliotajwa katika sakata la mkataba wa kifisadi wa Richmond.

  Ikulu kupitia Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo tayari imemkingia kifua Rais katika sakata la Richmond ikisema alichukua hatua madhubuti ikiwemo kuzuia malipo, Hamad akizungumza mjini Wete juzi, alisema kwa jinsi mjadala wa Richmond ulivyokwenda na wabunge hasa wa CCM kuikosoa serikali yake, mkuu huyo wa nchi hana budi kuachia ngazi kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea kwani serikali yake imeshindwa kazi.

  "Kikwete amepandikiza mpasuko Zanzibar badala ya kuushughulikiaÂ… itamtapikia nyongo..." alitahadharisha na kusema kwa lolote litakalotokea atabeba lawama kwani ameshindwa kuchukua hatua mbalimbali zinazostahili katika matatizo yanayotokea nchini.

  Hamad akitoa mfano, alisema nchini Uingereza pindi kiongozi wa serikali akipata matatizo kama yanayotokea nchini na watu wa chama chake wakakosa imani na serikali huamua kujiondoa ili kuwekwe serikali mpya na kuongeza: "Na hili ndilo anatakiwa kufanya Kikwete."

  Kauli hiyo ya kiongozi wa upinzani inakuja pia katika kipindi ambacho wabunge wa CCM ndiyo wamekuwa mstari wa mbele kuisulubu serikali ya Rais Kikwete, katika mambo mbalimbali ya ufisadi huku wakionyesha dhahiri kutoridhishwa na hatua za kupambana na tatizo hilo.

  Ingawa Hamad hakutaja majina ya wabunge, lakini Mbunge wa Kyela Dk Harrison Mwakyembe, Christopher Ole Sendeka (Simanjiro), Anne Kilango Malecela (Same Mashariki), Fredi Mpendazoe, John Shibuda (Maswa), Herbet Mtangi (Muheza), ambao wote ni kutoka CCM juzi wakiongozwa na Spika Samuel Sitta, wamekuwa wakiibana serikali bungeni kuhusu mambo mbalimbali ya ufisadi na kutaka hatua zichukuliwe kwa watuhumiwa.

  Juzi wakati wa mjadala wa Richmond, baadhi ya wabunge waliibana serikali katika sakata hilo na kuhoji iweje serikali ishindwe kuwachukulia hatua watu kama Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Dk Edward Hoseah, Mwanasheria Mkuu (AG) Johnson Mwanyika, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Athur Mwakapugi, Kamishna wa Nishati Bashir Mrindoko na wajumbe wote wa Timu ya Ushauri katika Mikataba ya Serikali (GNT) kutoka Benki Kuu (BoT) Ofisi ya AG na Shirika la Umeme (Tanesco).

  Wadadisi wa mambo ya kisiasa wanachukulia moto uliowashwa juzi na wabunge wa CCM katika sakata la Richmond na azimio la Bunge kuipa serikali muda hadi Novemba, iwe imeshughulikia watumishi wote waandamizi, ni ishara mbaya kwa serikali ya CCM na Rais Kikwete.

  Udadisi huo wa hali tete ya kisiasa na udugu wa mashaka kati ya wabunge na serikali, unadhihirishwa na kauli ya Ikulu ambayo ilitolewa na Luhanjo ghafla jioni, baada ya Bunge kuazimia huku wabunge wa CCM wakiwa vinara waliowasha moto huo wakiongozwa na Spika kwa ushirikiano na baadhi ya wabunge wa kambi ya upinzani.

  Ikulu ilitaja mambo manne ya msingi ambayo Rais alishiriki katika Richmond, ikiwa ni pamoja na kuzuia malipo kwa kampuni hiyo baada ya kutiliwa mashaka. Hamadi akizungumzia zaidi hali hiyo kati ya wabunge wa CCM na imani yao kwa Rais, alisema kwa uadilifu kiongozi huyo alipaswa kujiuzulu ili uchaguzi ufanyike.

  Kuhusu uchaguzi Tanzania kutarajia vitambulisho vya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), alisema hilo ni kosa kubwa na ukiukwaji wa sheria.

  Hamad alikuwa akieleza wananchi hao kwamba, chaguzi zote zinazofanyika kwa kutumia daftari la Zanzibar ni batili na kuongeza kwamba, Rais Kikwete anajua hilo, lakini amekuwa akilifumbia macho kwa maslahi ya chama chake.

  "Tunachohitaji ni daftari tofauti kwa Zanzibar na Muungano ili watu wapige kura kwa haki kinyume cha hapo watamuunganisha Kikwete na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa ambaye anaandaliwa mashtaka katika Mahakama ya Kimataifa ya The Hague."

  Tangu Rais Kikwete kuingia madarakani mwaka 2006, serikali yake imekuwa ikikabiliwa na misukosuko ambao mmoja mkubwa unaoitikisa hadi sasa ni mkataba wa kifisadi wa Richmond, uliotiwa saini Juni 23 mwaka huo.

  Richmond ambayo ilimfanya Edward Lowassa kujiuzulu Uwaziri Mkuu imekuwa ikiitikisa serikali tangu Mkutano wa 10 wa Bunge la mwezi Aprili, mwaka jana.

  Bunge lilitoa maazimio 23 kutaka serikali itekeleze ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua kwa maafisa hao waandamizi wa serikali, lakini wiki iliyopita serikali ilitoa taarifa bungeni ambayo iliwasafisha.

  Hali hiyo iliibua upya moto wa Richmond huku wabunge wa CCM wakiongozwa na Spika wakiwa mwiba kwa serikali ya Rais Kikwete, huku mbunge wa Maswa Shibuda akitaka iwepo sheria itakayolipa Bunge meno zaidi ya kuing'ata serikali hasa inaposhindwa kuwajibika kwa Bunge.

  Source:
  Mwananchi Newspaper
   
 2. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2009
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Anatakiwa kujiuzulu lakini hilo halitatokea Tanzania kwa hivi karibuni.
  Labda wananchi walale barabarani siku tisini halafu wafadhili walazimishe hata hivyo linaweza lisitokee kwani kenya walitaka kumalizana au Zimbabwe wametoana macho bado viongozi wao wapo.

  Afrika inamatatizo makubwa ya uelewa ya maana ya kuwa kiongozi na kuwajibika kwa sheria na kiapo.
  Kikwete uwajibikaji wake sio tu kwamba haueleweki ila hata yeye mwenyewe hajielewi. Hivyo inakuwa vigumu sana hata kuelewa wananchi na bunge lake linataka nini.

  Tanzania maisha ni kanyaga twende, mambo kupandiani, kama alivyo sema Profesa J mwenye cheni bandia kauza na akapewa fedha bandia.
  Ila Nchi inauza madini halisi nasi tunapewa fedha bandia chini ya viongozi bandia wanaoongoza watu bandia kwenye nchi bandia.

  Sasa chini ya Raisi na uelewa wa Mkuu wa nchi wenyewe tunamwita jemedari JK tumeuziwa mitambo bandia na akakubali na hata tulipo piga kelele kwamba hilo ni fafa yeye kasema waachie wote walionunua hiyo fafa walikuwa wamesinzia tu ndio maana hawakuona ikiingizwa, ila kwa sababu imeingizwa kifedhuli basi mpeni dowans naye atupige hivyohivyo kwani hawa watu bandia hawatajua. akijua kwamba hata bungeni kumejaa mazuzu wengi ambao watapiga kelele wiki moja au mbili halafu watasinzia wakiamka watasema ilikuwa poa ipite kama ilivyo.

  Nchi isiyo na majasiri waliotayari kulinda uhuru kama tulivyo upata kwa damu. Yupo wapi Kuli, wapo wapi wale mama wauza mandazi waliotawanya ujumbe kwa karatasi za kufungia mandazi, wapo wapi wale mashujaa. kama watu wa miaka ya sitini na hamsini waliweza kuwa na akili ya kupambana na mkoloni ambaye aliwazidi kwa kila kitu inakuwaje leo Tanzania hatuwezi kupambana na mijizi isiyojua abc. Kweli akili ya akina makamba inatuburuza au Rostam anakuwa ndiye aliyeshika mpini kweli leo hata watu ambao hawajui ni wapi jua linachwea wanatunyima usingizi.

  Mwisho wa kuandika unakaribia nasi twende tukadai fungu letu kabla halijaisha, nasi tukadai urithi wetu kabla hatujaachiwa mashimo na yenye sumu ya zebaki.
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Ni vizuri akajiuuzuru tuu kwa sababu aliingia kwa kutufanya watanzania tuamini kabisa kwamba ndie atakuwa jibu la umaskini wetu ,tuliamini ataturejeshea mali zetu au kudhibiti uporwaji wa mali,tukajua ataaimarisha upatikanaji wa demokrasia,tulimpenda tukijua hatutaona kamwe wanafunzi vyo vikuu wakizurura na mabango ,wahadhiri chuo kikuu wakitoroka madarasa kwenda kubembereza kazi za kufanya tafiti,tulijua mpaka sasa ajira milioni moja kwa vijana zingekuwa bwelele,mapesa ya jakaya yangewalenga wanyonge, na mengine na mengine hakuna hata moja amelitimiza mfumuko wa bei huo,watu tunakula mlo mmoja tumekonda na wengine tunautapiamlo na damu kidogo maradhi yametuzidia hakuna utawala wa sheria kila mtu anasema vyake hata huko kwake ikulu watu wanakurupuka ,nakubaliana na Hamad aitishe uchaguzi mapema akichagulia tena sawa lakini wengi hatuna imani naye ameipoteza nchii haina mwelekeo hatujui siasa gani ya kiuchumi tunafuata sasa.
   
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  the nchi apewe Sefu ?

  another day another idiot haishi kubwabwaja

  infact JF inafanyakazi nzuri kuliko that bunch wanajiita wapinzani ambao wanaongozwa na huyu mvaa suti za chon lai
   
 5. LazyDog

  LazyDog JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2009
  Joined: Apr 10, 2008
  Messages: 2,478
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135

  Malengo yako nini kwa namna ulivyoandika?

  Kilichofanywa na wananchi wa Kenya, Iran.... unadhani hakijazaa matunda yoyote?
   
 6. K

  Kachero JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Suala ni uoga tuu lakini Katiba ya Tanzania ibara ya 46A imeainisha wazi mamlaka Bunge iliyonayo ikiwa ni pamoja na kumshitaki Raisi aliyeko madarakani.Endapo mashitaka yatadhibitika basi Raisi anaweza kuondolewa madarakani na hii nafikiri ndiyo Mhe.Rashid alikuwa amelenga kwa wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imani na Raisi.Naiweka hapa sehemu hii ya katiba ya Jamhuri ya Muunganoi wa Tanzania ili iwe rahisi kwa watu kuiona na kuijadili jinsi inavyowezekana Raisi aliyeko madarakani kuondolewa.

  46ABunge laweza kumshtaki Rais Sheria Na. 20 ya 1992 ib. 8; 12 ya 1995 ib. 4
  (1) Bila ya kujali masharti ya ibara ya 46 ya Katiba hii, Bunge linaweza kupitisha azimio la kumuondoa Rais madarakani endapo itatolewa hoja ya kumshtaki Rais na ikapitishwa kwa mujibu wa masharti ya ibara hii.

  (2) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya ibara hii, hoja yoyote ya kumshtaki Rais haitatolewa isipokuwa tu kama inadaiwa kwamba Rais–

  (a) ametenda vitendo ambavyo kwa jumla vinaivunja Katiba au sheria ya maadili ya Viongozi wa Umma;
  (b) ametenda vitendo ambavyo vinakiuka maadili yanayohusu uandikishwaji wa vyama vya siasa yaliyotajwa katika ibara ya 20(2) ya Katiba; au
  (c) amekuwa na mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano, na haitatolewa hoja ya namna hiyo ndani ya miezi kumi na miwili tangu hoja kama hiyo ilipotolewa na ikakataliwa na Bunge.


  (3) Bunge halitapitisha hoja ya kumshtaki Rais isipokuwa tu kama–

  (a) taarifa ya maandishi, iliyotiwa sahihi na kuungwa mkono na Wabunge wasiopungua asilimia ishirini ya Wabunge wote itawasilishwa kwa Spika siku thelathini kabla ya kikao ambapo hoja hiyo inakusudiwa kutolewa Bungeni, ikifafanua makosa aliyoyatenda Rais, na ikipendekeza kuwa Kamati Maalum ya Uchunguzi iundwe ili ichunguze mashtaka yaliyowasilishwa dhidi ya Rais;

  (b) wakati wowote baada ya Spika kupokea taarifa iliyotiwa sahihi na Wabunge na kujiridhisha kuwa masharti ya Katiba kwa ajili ya kuleta hoja yametimizwa, Spika atamruhusu mtoa hoja kuiwasilisha hoja hiyo, na kisha Spika atalitaka Bunge, bila ya kufanya majadiliano, lipige kura juu ya hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi na kama ikiungwa mkono na Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote, atatangaza majina ya wajumbe wa Kamati Maalum ya Uchunguzi.

  (4) Kamati Maalum ya Uchunguzi, kwa madhumuni ya ibara hii, itakuwa na wajumbe wafuatao, yaani–
  (a) Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano, ambaye atakuwa ndiye Mwenyekiti wa Kamati;
  (b) Jaji Mkuu wa Tanzania Zanzibar; na
  (c) Wabunge saba walioteuliwa na Spika kwa mujibu wa Kanuni za Bunge na kwa kuzingatia uwiano wa uwakilishi baina ya vyama vya siasa vinavyowakilishwa Bungeni.

  (5) Endapo Bunge litapitisha hoja ya kuunda Kamati Maalum ya Uchunguzi, Rais atahesabiwa kuwa hayupo kazini, kisha kazi na madaraka ya Rais yatatekelezwa kwa mujibu wa masharti ya ibara 37(3) ya Katiba hii hadi Spika atakapomfahamisha Rais juu ya azimio la Bunge kuhusiana na mashtaka yaliyotolewa dhidi yake.

  (6) Ndani ya siku saba baada ya Kamati Maalum ya Uchunguzi kuundwa, itakaa, ichunguze na kuchambua mashtaka dhidi ya Rais, pamoja na kumpatia Rais fursa ya kujieleza, kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

  (7) Mapema iwezekanavyo, na kwa vyovyote vile katika muda usiozidi siku tisini, Kamati Maalum ya Uchunguzi itatoa taarifa yake kwa Spika.

  (8) Baada ya Spika kupokea taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi, taarifa hiyo itawasilishwa Bungeni kwa kufuata utaratibu uliowekwa na Kanuni za Bunge.

  (9) Baada ya taarifa ya Kamati Maalum ya Uchunguzi kuwasilishwa kwa mujibu wa ibara ndogo ya (8), Bunge litaijadili taarifa hiyo na litampa Rais fursa ya kujieleza, na kisha, kwa kura za Wabunge wasiopungua theluthi mbili ya Wabunge wote, Bunge litapitisha azimio ama kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika, na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, au kuwa mashtaka hayo hayakuthibitika.

  (10) Endapo Bunge litapitisha azimio kuwa mashtaka dhidi ya Rais yamethibitika na kwamba hastahili kuendelea kushika kiti cha Rais, Spika atawafahamisha Rais na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi juu ya azimio la Bunge, na hapo Rais atawajibika kujiuzulu kabla ya kuisha kwa siku ya tatu tangu Bunge lilipopitisha azimio hilo.

  (11) Endapo Rais ataacha kushika kiti cha Rais kutokana na mashtaka dhidi yake kuthibitika, hatakuwa na haki ya kupata malipo yoyote ya pensheni wala kupata haki au nafuu nyinginezo alizo nazo kwa mujibu wa Katiba au Sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.

  Je hayo yaliyoanishwa hapo juu yanawezekana kwa hali ilivyo Tanzania sasa hivi?
   
 7. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,652
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Kuvaa suti ya "chon lai" kunahusiana vipi na hoja ya Hamad Rashid Mohamed?

  Chambua yaliyomo katika hoja aliyotoa mhusika siyo kumshambulia wasifu wake na kumtukana.
   
 8. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Walisema Dalili ya mvua ni mawingu!!!!!!!!!!!!!!!!

  I like this game!!!!
   
 9. I

  Ilongo JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 292
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0


  Hamna kitu hapo. Kama kweli wako seriuos si wangeanza na wabunge wenzao walio mafisadi. Wawalazimishe wajiuzulu huo ubunge tuone kama kweli wanaweza. Siasa tu.
   
 10. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hii haiwezi kutokea katika siasa za bongo wangapi wamechafuka na wanazidi kubebwa?
   
 11. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ukweli unabaki pale pale kuwa nchi hii ni kubebana tuu mpaka mwisho,nashindwa kuelewa watu wenyewe wanafahamika jamani au kuwajibishwa ni klwa watu fulani tuu?kwanini tunafanywa kama malimbukeni? imagine mambo ya Kiwira,Dowans with richmond,EPA cases zinafanyiwa nini? au wananunua mda til 2010?kina mramba, yona,na yule katibu mkuu fedha? nothing and nothing will ever change this country kwa huu mwendo, njia pekee apatikane rais mwehu, mwehu kwa maana ya utendaji wa bila kuangalia uso wa mkosaji, nadhani naeleweka hapo!! hatusongi mbele,kila siku wachache kujifanyia ubadhirifu kwa migongo yetu?maisha daily yanapanda juu hakuna wa kukemea, wachache tu wanafaidi bila jasho,why?why?
   
 12. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2009
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,503
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Seriously nafikiri Seif ana uwezo mkubwa kuliko mkulu wetu ila tu yuko on the wrong side of the game!!!!!!!!!!!!!!
   
 13. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2009
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  inakuwaje anaongelea akiwa nje ya bunge kama si unafiki? mbona akiwa bungeni sijamwona akiwa mkali kwa serikali hasa kwa Wazili Mkuu?
   
 14. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ukweli pia huyu jamaa kaenda kubwekea nyumbani wakati pahala muafaka hakusema jambo la hivyo, ni jambo zuri lakini nae kaonyesha woga, angekuwa yeye ni presidaa pia asingeweza kumwajibisha mtendaji wake yeyote! hatuna viongozi tunao watawala mazee!! JK lakini angepata push nzuri toka chini angefanya vizuri, tatizo ni kuwa amezungukwa sana na rattle snakes!!
   
 15. K

  Kachero JF-Expert Member

  #15
  Aug 3, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa nini kifanyike ili apatikane huyo Rais mwehu ambaye ataleta mabadiliko na uwajibikaji serikalini kwa kuwa hali ilivyo ikiruhusiwa kuendelea miaka mingine mitano tutakwa tumeiingiza nchi katika matatizo makubwa sana.

  Hali katika nchi kama Ivery Coast,Liberia, Sierra Leon zilianza hivi hivi,kwa kuwa na minung'uniko na kutokuridhika kwa sehemu kubwa ya jamii.Yet wale waliopewa ridhaa na wananchi wakazibaka hizo nchi,wakajilimbikizia mali,kuziba masikio yao na kuwadharau waliowapigia kura.

  Mwisho wa mambo hayo ni machafuko makubwa sana ambayo yamewagharimu uchumi,maisha yao bado hayajatengemaa mpaka sasa.Je huko ndio twataka kuelekea Tanzania kama nchi, au nini kifanyike ili mabadiliko ya dhahiri yaweze kutokea.
   
 16. Jiwe Linaloishi

  Jiwe Linaloishi JF-Expert Member

  #16
  Aug 3, 2009
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 3,736
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Mimi nafikiri silaha kubwa kwa bunge ilikuwa kutokupitisha ile budget mpaka yale maazimio ya bunge yametekelezwa na serikali ipasavyo kama bunge lilivyoagiza. wakati wanapitisha ile budget walikuwa wanajua kabisa kuwa yale maazimio ya bunge hayajatekelezwa kwahiyo wangekwamisha ile budget kwanza mapaka kieleweke.
   
 17. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #17
  Aug 3, 2009
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  tuendelee na mfumo wa sensitization kwanza, watanzania wengi hawajajua nguvu ya kura yake moja namana inaweza kuleta mabadiliko makubwa,tuelemishane, na kulaumu na kuonyesha kutoridhishwa na hii system,eventually out of it tutapata solution, yaweza isiwe ka Ivorycast, iberia,rwanda etc but tukapita smoothly, namnini watz ni watu tukiwa na umoja kwa pamoja tutaleta changes, esp hiki kizazi kinachoingia utawalani sasa, naamini hakitacheka na fuvu!!
   
 18. M

  MpendaTz JF-Expert Member

  #18
  Aug 3, 2009
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 1,579
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160

  Sina hakika lakini kuna kipengele ambacho kinamruhusu Raisi kuvunja Bunge na kuitisha uchaguzi upya kama Bunge likishindwa kupitisha bajeti. Kama ni hivyo kweli na tukiangalia muda uliobaki kabla ya uchaguzi na pia katiba kama ilivyoelezwa hapo juu na K'ro basi huu umekuwa mchezo wa watoto kung'atana meno. Nani aanze na wakati anajua mwenzake pia anayo na ana uwezo wa kung'ata. Zipo kazi za kufanya Tanzania, tena nyingi kabla ya kuingia kwenye ile barabara ya maendeleo ya Taifa letu.
   
 19. K

  Kachero JF-Expert Member

  #19
  Aug 3, 2009
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tukiwaelimisha wananchi wetu tuwafundishe pia namna ya kulinda kura zao si unajua kuna wataalam wa kuiba kura.Pia kuna jambo ambalo nimekuwa nikilionakwa muda sasa,watanzania walio wengi huwa wanajiandikisha kwenda kupiga kura.Lakini siku halisi ya kupiga kura unakuta ni nusu tuu ya waliojiandikisha ndio waliojitokeza kwenda kupiga kura.Haya yamekuwa dhahiri kwenye chaguzi nyingi za hivi karibuni.

  Natumaini uelimishaji utakwenda pamoja na kuwafundisha umuhimu wa kura ya kila mmoja wetu.Hiki ndicho kipindi cha mabadiliko na kasi iliyoshika hivi sasa ndiyo engine ya mabadiliko yenyewe.Wananchi wali wengi tena wa vijijini wakielimika tutarajie mabadiliko makubwa kutokea kama ilivyokuwa Tarime na huko bukoba hivi karibuni.

  Sina uhakika sana na kizazi hiki kipya kinachoingia madarakani,tumeona kina Masha,Ngeleja,adam malima,Nchimbi na kadhalika hawajaleta chachu ya kizazi kipya iliyotegemewa sana sana ndio wanaotumika kuendeleza ufisadi kwa ari mpya,nguvu mpya na kasi mpya.Je kwa mwendo huu tutafika?
   
 20. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #20
  Aug 5, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,590
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Kwani si aliisha-jiuzulu? kwani Kikwete rais?
   
Loading...